Naomba shauri

Jan 2, 2012
43
6
Ndugu zangu wapendwa wa Jamii Forums naomba ushauri wa mawazo kwani naumia sana. Nina mpenzi ambaye nimekaa nae kwa muda mrefu sasa toka tukiwa chuo mpaka sasa ni wafanyakazi. Mwanzo sikuwa na mpenda sana lakin alinishawishi mpaka nikaanza kumpenda haswaaaaaaa, yeye ndiye alinishawishi alete barua kwetu kwaniaba ya kufunga ndoa nikakubali lakn toka siku niliyo mkubalia alete barua kwetu mambo anayoyafanya simuelewi kila muda yupo busy unapiga cm hapokei anapokea muda anaotaka yeye. Lakini nikitumia cm nyingine anapokea muda huohuo. Naombeni ushauri nifanyaje bado nampenda sana tena sana.
 
kwanza naomba kukuuliza ulipomkubalia kuleta barua kwenu alileta? kama hajaleta achana nae nakama alileta fanyauchunguzi wa kina utagundua vitu vingi kwa huyo mpenzi wako
 
Kaa nae chini akufanulie kwa nini anakuwa busy na kuchunia simu yako LABDA ULIMUUDHI AU KASIKIA MAKITU MAKUBWA KUHUSIANA NA WEWE.
 
Tafuta mda muonane live, then muulize tatizo ninini, achana na mawasiliano ya cmu.
 
pia kumbuka kuwa mume mwema mtu hupewa na bwana kama ndie mume mungualiye kuandalia atakuoa tu endelea kumuomba mungu.
 
ameshagundua kuwa we umekufa/kuoza kwake. Sasa tulia usimfuatefuate tena. Kaza roho kama ni wako ni wako tu hakuna atakayezuwia.
 
Kwani mdada we unatumia simu gani?mi nahisi havutiwi na simu unayotumia ndo maana ukimpigia na simu nyingine anapokea fasta,mi nilijua labda ukitumia lyn tofauti na ya kwako ndo anapokea fasta cha maana hapo inabidi umuulize anapenda utumie cm gan?ni hayo tu
 
Hata umpende vipi mtu bado unaweza kuishi bila yeye. Kama anakupotezea na wewe punguza kidogo usijiumize bure... ni ngumu lakini ndiyo njia sahihi, kama ameamua kuachana na wewe, hata ungepiga simu vipi haisaidii, na kama ni wako ni wako tu.. Mimi najipenda binafsi kabla ya kumpenda binadamu mwingine, mambo ya kujitesa kwa kisingizio cha eti nampenda sana hayana mashiko kwangu... Watu wengine wanajitia hamnazo, yeye anapeta huko wewe unajitesa kwa sababu ya 'kumpenda' sana! Wapi na wapi?!
 
wanaume ni wanafiki na wanyama tumia akili usiweke kichwa sehemu moja
hope umenielewa
kutulia ni siku umewekwa ndani
unatakiwa ukipiga upande huu simu isipopokelewa unabipu upande wa pili unapigiwa
akili kichwani mwako
 
hata kama hujui kusoma basi ona picha!! kijana anataka kukata kamba huyo kwa jinsi ninavyoona.... Ila pia utueleze ukweli mana huwa nnaficha nyinyi kuvutia kamba kwenu, una hakika hujamfanyia kitu mwenzio kibaya cha kumkwaza mpaka akawa hivyo? kama umefanya mwanga yote ili watu wakushauri bila kuwa biased

Au labda alipokuja kutoa posa kweli aliona mambo au kusikia mambo ambayo yamemkatisha tamaa, jaribu kupeleleza na kwenu ujue kama kuna chochote kilijiri alipokuja...inawezekana majirani au mtu alimuuma sikio juu ya posa aliyoleta kwa kumwambia kuna jambo flani baya katika familia yenu...pole sana tena sana tena.

Ushauri: kama hapokei simu yako tafuta simu ingine na mpigie, ukipiga usifoke au kuonyesha kukasirika, akipokea muulize kwa upole kabisa kwa kuanza kumuuliza kama kuna jambo lolote umemkwaza akusamehe na umueleze unavyojisikia kwa jinsi anavyokuanyia saizi...narudia ukitaka mambo yawe mazuri jishushe na uwe mjinga, usifoke na kupayuka wakati unampigia ila ongea kwa upole na taratibu na kimahaba zaidi....na ukiona amekata simu ujue hakutaki huyo so anza mbele tu, utaumia lakini utafanikiwa tu..
 
wanaume ni wanafiki na wanyama tumia akili usiweke kichwa sehemu moja
hope umenielewa
kutulia ni siku umewekwa ndani
unatakiwa ukipiga upande huu simu isipopokelewa unabipu upande wa pili unapigiwa
akili kichwani mwako

Acha kumfundisha dada yetu umalaya wewe!
 
wanaume ni wanafiki na wanyama tumia akili usiweke kichwa sehemu moja
hope umenielewa
kutulia ni siku umewekwa ndani
unatakiwa ukipiga upande huu simu isipopokelewa unabipu upande wa pili unapigiwa
akili kichwani mwako

Huh! nimeipenda hii akili kumkichwa lol ukizubaa umeachwa feli. mamie 2 b honest huu ushaur ni mzuri sana ukiutilia maanani. hawatakuumiza kichwa kbs.
 
pole sana kwa hilo, kuna uwezekano kapata badilisho la mawazo au shetani mbaya kaingilia hapo, na pia kuna possibility unamganda sana, nakushauri punguza kumtafuta, let him miss u, kama vipi futa namba yake kwa mda ili usiweze mtafta, be expensive muache yeye ndo ahangaike kuwa anakutafuta, na kama ukiona ahangaiki basi huyo hakufai achana naye
 
wanaume ni wanafiki na wanyama tumia akili usiweke kichwa sehemu moja
hope umenielewa
kutulia ni siku umewekwa ndani
unatakiwa ukipiga upande huu simu isipopokelewa unabipu upande wa pili unapigiwa
akili kichwani mwako
Hapo kama sijakosea kuna wengi wanaweza kuwa wametukanwa.

Usisahau hata kwenye family yako wapo wanaume....Ungesema baadhi ya wanaume, hapo ingekuwa super.
 
My dia pole sn,yan haya mapnz hayana mwenyewe,
Jaribu kumtafuta ana kwa ana ongea nae,
Mweleze namna hali hiyo inavokuumiza na km kuna mahali umekosea omba msamaha wa dhati kwa machozi na magoti hakika km anakupenda Atakusamehe na hali itakua shwari,
Jitahidi kufait kwa njia zote kwa umpendae uckubal kushindwa na kukata tamaa bila kufanya jitihada!
Ila km atakwambia hakupendi tena na amebadili mawazo mshukuru mungu amin huyo hakua wako jipe moyo kwan ni lzm yy aondoke ili aliyeubwa kwa ajili yako apate kuingia.
 
Back
Top Bottom