Naomba mwenye link ya matokeo ya kachaguliwa kidato cha kwanza mwaka 2024 atume

Sasa subiri nakuwekea matokeo ya mtoto aliyepata wastan wa A zikiwepo hesabu na sayansi na bado akapangwa shule za kata mwaka huu,ndugu usikatae haya mambo yametukuta na watu wanalia hapa.
 
Screenshot_20231218-200813_Chrome.jpg
 
Sawa sio tatizo,ishu inakuja kwanin sio wote hawa ambao nao wana wastani wa B alafu wamepangiwa shule za bweni ikoje hii??
Jambo la msingi ni kukomaa na mwanao, unatakiwa uwe Tuition yake kwa asilimia mia moja. Usikubali aanguke, kwa matokeo aliyopata kwenye mtihani wa Taifa wa darasa la Saba mwaka huu mpongeze alafu kazia afaulu form four.
 
Hii nchi ya kijinga sana,yani nakumbuka kipindi tunasoma sisi ukifaulu karatasi za kwenda shule unazifata wilayan,
basi nilivyofika wilayan kuchukua karatasi wakanambia taja shule uliyofaulu nikataja,
Kucheki jina halipo kwenye listi,baada ya kurupushan kumbe jina limefanywa kuchomekwa kwenye shule B baada ya kunikata kwenye shule A.mtu mmoja akanipa siri kilichofanyika nikashukuru mungu maana sikua najua lolote,hivyo nikaripoti shule B bila karatasi ila kwasababu ilikua shule ya kitaifa na ufaulu wangu ulikua mkubwa wakashindwa kunifukuza,mkuu wa shule akanambia wewe umeandikwa kuja hapa lakin karatasi zako za tsm 9 hazipo.
Cha ajabu nilisoma pale mpaka nikamaliza na nikatoka na matokeo yangu freshi tu
N.B shule A ilikua TABORA BOYS na shule B ilikua GALANOS.
Mbna zote nzuri tyuuh
 
Mwaka huu 2023, vijana waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kufanikiwa kupata wastani wa daraja 'A' ni 53,943 (3.98%) ya wataihiniwa wote.
Kwa akili ya haraka haraka huyo wa kwako amepata wastani wa daraja "B".
Shule za sekondari bweni (za serikali) kwa nchi nzima ni 38 tu na zina uwezo wa kubeba wanafunzi 4,300 tu kwa mchujo maalumu wa hao 53,943 waliopata daraja A!
Hawa 49,643 waliobaki kwa waliopata A (53,943-4,300), wazazi wao (baadhi - wenye uwezo) hawajabwata maana watoto wao watawapeleka shule nzuri tu za private.
Alafu wewe kenge unakuja hapa na kubwatabwata na hiyo B yako!
 
Alafu ishu ya eti shule zipo 38 sio kweli mzee,
Jaribu kufuatilia upya,kumbuka kila mwaka kuna shule mpya zinaanzishwa nyingi sana,ndani ya miaka ya samia zipo shule za bweni kwa ajili ya kudato cha kwanza zaidi ya tano zimeshaanzishwa,shule unazosema wewe labda kipindi tunasoma sisi miaka ya 1990s
 
Mkuu unaweza kuwa sahihi,kuna ushubwada mwingi sana kwenye elimu yetu..
 
Hizi zote ni public schools of Tanzania
Moshi ufund,old mosh,lyamungo,kifaru,kilakala,msalato,tanga ufund,bwiru,minaki,pugu,kibaha,ilboru,mzumbe,kisarika,kisimiri,jokate mwegelo mlingano,kantalamba,azania,jangwani,toangoma,ashira girl,weruweru,balangdalau,tumaini.

Kuna shule mpya zaidi ya kumi ndiomana kila mwaka wanaokua selected wanaongezeka kiidadi,hizo ni chache ninazozifahamu,zipo nyingi sana za o level.

Alafu kama wewe unao uwezo wa kuwapeleka wanao private ni wewe brother unafikiri kwanini zipo hizi shule kama ilboru,kibaha,moshi ufundi,ifunda kilakala,korogwe,kama ungejua usingeweza kuongea hivi eti watawapeleka watoto wao private nzuri tu.
Usilete stori za yohana mjinga hapa aliyetumwa na mama yake kwa msisitizo akanunue mafuta ya kupikia huku akiambiwa hakikisha unaweka hela mfukoni ili isipotee,yohana akakariri kwamba ili mafuta yasipotee ngoja niyamimine mfukoni nicheze mpira nikifika nyumbani nayatoa nampa mama apike.
 
Hakuna cha rushwa wala nini hebu acheni ujinga ninyi mtoto wa dada yangu kapata wastani wa B ila kachaguliwa shule ya ufundi na hatukutoa rushwa
 
Leo hii kafanyiwa mwanangu dah,mwanangu kapiga A za hesabu,sayansi,kiswahili na kingereza zingine B cha ajabu kapangwa shule ya kutwa.kwani wanatumia vigezo gani?naomba mnisaidie kujua.
Unataka tukose hata wa kuchangamsha darasa mkuu!?
Usihofu huku mwakani tumepanga kufanya makubwa dogo atafika mbali
 
Hakuna cha rushwa wala nini hebu acheni ujinga ninyi mtoto wa dada yangu kapata wastani wa B ila kachaguliwa shule ya ufundi na hatukutoa rushwaishu ni kwamba wanatumia vigezo gani??yani suala sio wastani wa B au A suala ni je kwanin yupo aliyepata wastani wa A na akiwa na A ya hesabu bado amepangwa day school.
 
Hakuna cha rushwa wala nini hebu acheni ujinga ninyi mtoto wa dada yangu kapata wastani wa B ila kachaguliwa shule ya ufundi na hatukutoa rushwa
Ipo namna ndugu,wewe usiseme eti hakuna cha rushwa,sawa hatujakataa kwamba hakuna rushwa ila tungefafanuliwa wanatumia vigezo gani kuwapanga hawa watoto kwenda kidato cha kwanza?mimi ninao watoto mapacha wamemaliza msingi hizi za serikali,mmoja amepiga wastani wa A na Hesabu ana A bado kapangwa day school,doto amepiga wastani wa B nae kapangwa day school sasa sijui naomba nifafanulie nielewe ndugu.
 
Back
Top Bottom