Naomba msaada wa KARO kwa Master's Course

mkys

Member
Apr 3, 2012
31
18
Mie ni mkazi wa hapa Dar es Salaam. Nimepata nafasi ya kusoma "MSc in Development Policy and Practice for Civil Society" Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es Salaam. Masomo yanaanza mwezi ujao wa November. Karo ni TSh 4,800,000. Nina kiasi kidogo tu kisichozidi 1,000,000.
Mwenye kuguswa na ombi langu na ana nafasi ya kuniungisha niweze kuziba hili pengo, namuomba awasiliane na mie kwa namba 0764530660. Account No. yangu ni 5011740008 UMOJA Bank. Nitashukuru kwa atakayenisaidia.Aksante
 
kwann ucngefanya kaz kwanza ujipange? First degree mkopo masters msaada,hv hz elimu zinatukomboa fikra kwel?
 
kwann ucngefanya kaz kwanza ujipange? First degree mkopo masters msaada,hv hz elimu zinatukomboa fikra kwel?

Mkuu wengine huwa wanafikiria kwa kutumia MEYA WA DAR
Elimu haikomboi watu
 
mkuu hapo mi naona ungefanya namna ya kuongeza kipato zaidi kuliko kuongeza vyeti,kumbuka vyeti vingi sio ishu ishu ni kipato.
 
Mie ni mkazi wa hapa Dar es Salaam. Nimepata nafasi ya kusoma "MSc in Development Policy and Practice for Civil Society" Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es Salaam. Masomo yanaanza mwezi ujao wa November. Karo ni TSh 4,800,000. Nina kiasi kidogo tu kisichozidi 1,000,000.
Mwenye kuguswa na ombi langu na ana nafasi ya kuniungisha niweze kuziba hili pengo, namuomba awasiliane na mie kwa namba 0764530660. Account No. yangu ni 5011740008 UMOJA Bank. Nitashukuru kwa atakayenisaidia.Aksante

Kwa kuwa mzumbe pale wanaingia jioni,na una fedha zisizopungua 1M nakushauri usipaniki,fanya yafuatayo:tafuta kitu kinachopendwa sana Msumbiji hapo Dar,nunua kwa hela yako hiyo uliyo nayo kisha bakisha nauli tu ya kuendea msumbiji,ukifika uza hzo bidhaa Msumbiji halafu utapata fedha ya kwao inayoitwa New Met,ukizipata hzo zibadilishe kulekule Msumbiji ziwe Dola za kimarekani,ukuija hapa utakuwa umepata faida ya kukuwezesha kufanya shahada yako ya uzamifu bila shida kwani kila ukipata fursa utafanya hivyo mpaka utamaliza ada yote unayodaiwa na pia unakuwa umeweza kujiajiri.
Ila ukijiona wewe ni mwoga wa kuthubutu endelea kuomba ila ss tumezoea kuwasaidia wagonjwa zaidi kuliko wenye kusoma tena ngazi ya juu kama hiyo.
 
Tutakuaminije?
Ndugu yangu nimetoa namba yangu ya simu ili niweze kupatikana kwa urahisi na ikihitajika kuthibitisha utarajiwa wa uanafunzi wangu hapo chuoni basi nifanye hivyo kwa aliyetayari kwa ombi langu.
 
Mie ni mkazi wa hapa Dar es Salaam. Nimepata nafasi ya kusoma "MSc in Development Policy and Practice for Civil Society" Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es Salaam. Masomo yanaanza mwezi ujao wa November. Karo ni TSh 4,800,000. Nina kiasi kidogo tu kisichozidi 1,000,000.
Mwenye kuguswa na ombi langu na ana nafasi ya kuniungisha niweze kuziba hili pengo, namuomba awasiliane na mie kwa namba 0764530660. Account No. yangu ni 5011740008 UMOJA Bank. Nitashukuru kwa atakayenisaidia.Aksante

Ndugu yangu kwanza nakupongeza kwa ujasili wako wa kuiabisha first degree yako, inaonesha ni kiasi gani haijakukomboa. Pili nakupongeza pia kwa kutokuwa na malengo endelevu, Serikali haitoi mikopo kwa wanafunzi wa masters kwa sababu kama hii ya kwako kutojitambua na kujiona masikini kuliko baba yake Pinda (mkulima huko kwao nayeishi chini ya shilingi 200 kwa siku).
 
ndugu yangu nimetoa namba yangu ya simu ili niweze kupatikana kwa urahisi na ikihitajika kuthibitisha utarajiwa wa uanafunzi wangu hapo chuoni basi nifanye hivyo kwa aliyetayari kwa ombi langu.
umefikaje mpaka hapo kielimu?
Hiyo mil moja umepataje? Kwanini usiendelee kutafuta upate hizo mil tatu? Wengine unaotuomba hizo mil moja yenyewe hatuna
 
Kwa kiasi fulani nyerere amechangia kutulemaza! Kwanza ni dhambi kulipiwa masters na wazazi wako pia, unless ni mama-baby.
Kama unatafuta mtu wa kukuoa sema wazi. Mi nitakulipia kodi ya nyumba.
 
Kiwango cha kusaidia wenye matatizo ya kielimu ni kuanzia shule ya msingi mpaka first degree kwa wale wenye matatizo ya dhahiri tena kutoka familia maskini. Bila hivyo itakuja mijitu inayotaka kwenda masters na phd na bado itataka kusaidiwa.

Kama tayari mtu alishapata first degree na anataka tena msaada wa MA ina maana ameshindwa kuitumia hiyo degree yake kujikomboa! Huu ni msiba! Wapo vijana kama sisi wameanza kwa shida na mitaji ya elfu 50 tena wakiwa na elimu ya msingi tu, leo wako mbali sana kimaendeleo kwa sababu walithubutu.

Wewe mwenye Degree unaye taka msaada wa MA katafute shule ya kata ukafundishe kule watakulipa mpaka laki na nusu kama part timer na ukipata ajira kamili take home itafika laki nne na kama themanini hivi, hapo utapanga lini ukasome hiyo MA yako, kwa sasa acha tusaidie wadogo zako wengine wenye uhitaji wenye kuwaza angalau kumaliza o-level.

Think or think.
 
ongera sana kwa kupenda elim ya juu.mm ni mwalim wa s/msingi nliyesoma msc-hrm mzumbe tawi la morogoro 210-2011 kwa kujlpia mwenyewe.binafsi niliaandaa gunia 100 za mkaa na nkaziuza kpind cha maska pia nlikuwa nmelma alizet hekari 20 zilizonpatia gunia 120 na @ gunia nliliuza kwa sh.40,000.binafs naomba ufanye maandariz kwanza ya kupata pesa ndo usome hyo masters. kuomba misaada nikujizalilisha mbele za ndugu na jamaa wanaokuzunguka.nadhan umefka wakat vyuo vyetu vfundshe ujasiriamal kwa kila course angalau wasom tuwezeze kujiajir kulkokuwa ombaomba. vjana tulioweng tunapenda vy kunyoka kulko kutumia akir na nguvu zet tulzojaliwa na molla ...samwelambrose@yahoo.com
 
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Bob Marley Quote ;I'm not educated; I'd be a damn fool if I was (educated)! ;
[/FONT]
 
Sasa dada angu hata ukilipiwa hyo ada huko chuo utaishi vp?na kwanin ucfanye kwanza kaz kulko kukimbilia hyo masters ambayo ukimalza km huna ela pia utateseka2 huko mtaani
 
Tafuta kazi ufanye ndugu yangu! Kuna rafiki yangu aliamua kuendelea na Shahada ya Pili na akafanikiwa kumaliza, baada ya kumaliza, kila akitafuta kazi anaambiwa je unao uzoefu? Wengine "hatuna hela za kukulipa mshahara". Pia kumbuka ya kwamba, kwa mtu anayeanza kazi atalipwa kwa kigezo cha Shahada ya Kwanza.
 
Mama yangu! ukikosa tena kazi baada ya hiyo masters ukasome Phd !!!!!!!!!!!!!! mi naona kama ni msaada tuchangie watoto wa secondari wanaokosa hata elfu 20 ya karo. Yaani umekosa hata utendaji wa kata? Dar hakuna kazi bila experence.
 
Pole sana kwa kuhangaikia elimu yako ya juu, ila ninachokiona mbele yako lazima utakuja kuvuliwa hiyo pichu yako uliwe then upate hiyo pesa.
Ningeshauri jiajiri kwanza ili upate mtaji then endelee kusoma.
 
Kapige shule mkuu kama future yako unaiona kupitia iyo shule,wewe ndio unaejua unafanya nini kwa malengo gani,na plan zako za maisha unaziandaa wewe..mtu akupe ushauri ila usiruhusu akupangie na nini ufanye kwenye maisha coz mwisho wa siku wewe ndio utakuja kuishi ayo maisha sio yeye.

Na wasaidiaji hapa huwa hawana maneno mengi sana,achana na hawa wengine...mtu kaomba msaada kama huna kaa kimya usijenge mazingira na ya wengine wampuuze...roho mbaya ingekuwa utajiri bongo ingekuwa superpower..

Ushauri:nenda ubalozi wa Netherlands pale huwa wanatoa sapot kwa watu wa postgraduate kama wewe..kama deadline bado lakini.
 
mkuu naomba unijulishe biashara gani inalipa huko msumbiji, nataka nifanye hiyo business, naomba unijuze mkuu.
 
mkuu naomba unijulishe biashara gani inalipa huko msumbiji, nataka nifanye hiyo business, naomba unijuze mkuu.

mkuu ni vyema ukafanya utafiti mwenyewe uko mtaani..mabandiko mengine hapa ni ya kufikirika tu.
 
Back
Top Bottom