Naomba Mnipe ushauri kuhusu huyu mke wangu

Jan 24, 2012
32
21
wapendwa wana jamii naomba msaada wenu
mi nilioa tangu mwaka 2007,nina watoto wawili na mke wangu, wakati na funga naye ndoa aliniambia yule x-boyfriend wake aliekuwa naye alikwenda UK kusoma na hana mawasiliano naye tena na ameamua aanze maisha na mimi upya.
siku mmoja ilikuwa tarhe 24 december 2007 mnamo saa sita usiku simu ya mke wangu iliita na akawa anaongea kwa wasi wasi sana lakini mi nikajifanya nimelala usingizi fofo,akanyanyuka nakwenda sebuleni kuongea na simu,mi sikutaka kujua walienda kuongea nini.
tarehe 31/12/2007 ilipofika mnamo saa nane usiku ilipigwa simu tena akaondoka akaenda kuongelea sebuleni pia,mi sikutaka kujua ni kitu gani waliongea.
mwaka 2008 mke wangu akiwa na ujauzito wa miezi saba aliletewa zawadi kwa EMS nilipoisoma adress ilikuwa ikitokea UK na zawadi hiyo zilikuwa ni nguo za ndani na perfume mbili koja ya kike na nyingine ya kiume,nilipomuuliza akaniambia kuna rafiki yake wa kike anasoma huko kamtumia zawadi.
miezi sitta baada ya kujifungua aliniambia amepata short courses kwenda UK kusoma hivyo ataniachia mtoto then atarudi baada ya wiki tatu,nikamuomba details za chuo na admission zote nilipewa na zilikuwa genuine.
baada ya wiki moja kuna simu ilinipigia ya mkaka akaniambia samahani broo mi hunijui na wala mi sikujui ila nimepata uchungu sana baada ya kuona mke wako anachokifanya huku UK, akaniambia jpe email adress yako ntakutumia picha leo.
kweli zilipotumwa zile picha sikuamini macho yangu kabisa na zilikuwa mbay na za utupu pia.
aliporudi mke wangu nikamsomea mashitaka akakiri kweli na akaomba msamaha kwa kweli nilimuomba Mungu anisaidie katika uamuzi na nnikamsamehe.
alichokifanya mwaka jana december mpaka sasa nashindwa nifanyaje,aliniambia tena kapata course UK, alikwenda december na amerudi january15,lakini ana ngeo usoni na kovu kubwa kifuani na lama za kuumwa na meno mkononi.nimejaribu kumbana kwa kila njia haniambiii chochote.
wapendwa naomba ushauri wenu
 
aah hii ume2nga tena bila kujipanga, kwa hali ya kawaida usingemruhusu mara ya pili aende uk wakat at first alikudanganya na ukapata ushahid tena akakiri, labda uwe *****.
 
Pole sana braza, ngoja waje wenye busara zaidi wakupe ushauri mzuri, hold on..
 
Mbogoshi, nimeshusha pumzi
Pole sana aisee. Duh huyu mwanamke mwenzetu kama ni kweli anayatenda hayo mbona ana mambo? je mlifahamiana naye kwa muda gani kabla ya kuoana hiyo 2007?
 
Pole mwenyezi mungu akupe Moyo huo huo wakusamehe, hapa inabidi usikilize Moyo wako aunataka nn.
 
Aligombania Bwana,mambo ya kwa malikia si mchezo,watz wengi wananyang'anyana mabwana
 
Hivi kumbe dunia kuna wanaume wa hivi mpaka karne hii,km ni upendo kweli wako utakua wa agape kweli!cjui mambo ya ndoa kiivo subiri wenye uzoefu waje.
 
Haya mambo yanafanyika sana mkuu, sema kinachotusaidia ni kutokujua ama kuwa na taarifa za juu juu ambazo huishia kuwa tetesi.
Unajua mara nyingi wanawake huwa hawaachani moja kwa moja na maboyfriend wao, hasa inapotokea hawakutengana kwa ugomvi. We mzalishe tena na tena. Akichuja kidogo na kuwa na umbo la kimama, jamaa watapoteza apetite na utakuwa na uhakika wa kula peke yako!
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Ndio mitihani ya maisha. Kwa kweli mimi siwezi kukupa ushauri kuhusu hili maana mambo ya ndoa mm nayaogopa.
 
mm kifupi nashauri nenda kampime afya yake

pili mchunguze huenda ana tabia za ziada ambazo anashindwa kukwambia afanyeje kutokana na mahusiano mliyonayo?

tatu usimruhusu tena kwenda UK kwasababu yoyote ile

je huyo ni mke wako wa ngapi? je ulifuata hatua gani hadi kufikia kuoana 2007? je mlifahamiana vipi? nikipata maelezo zaidi naweza kukushauri zaidi
 
Mie kwa mtazamo wangu naona kama we ndio umeolewa, hauna say kwa wife wako!
kabisa yan, kaka embu behave kama wanaume wenzio uko ndoan jaman.
yan mwanamke anakupeleka peleka huna say kbs ndio maana anakufanyia yoote hayo.
sina lingine zaid ya kukupa pole.
 
Mwanaume kweli, mke wako anatoka kitandani kwenda kuongea na simu sebuleni wewe
unajifanya umelala, au wewe mtoto siyo riziki,
Kama ulimruhusu kwenda mara ya pili mimi mama yako nakushangaa sana,
vinginevyo na wewe una matatizo ya akili. Mwambie yule rafiki yako akutumie
picha kama zile za kwanza ili uongeze kwenye albamu yako, hata akienda trip ya tatu
usisahau kumwambia alete picha.
 
Back
Top Bottom