Naomba kwa yeyote anayefahamu kuhusu biashara ya matunda anisaidie

Zabron Hamis

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
6,514
10,421
Naomba kwa yeyote anayefahamu kuhusu biashara ya matunda katika nyanja zifuatazo anisaidie.

Mtaji wa chini kabisa kupata mzigo

Aina za matunda yanayopendwa zaidi

Maeneo ambayo nikifungua ninaweza kutengeneza faida angalau 10 kwa siku (pwani/dar)

Kiwango cha chini cha posho kwa msimamizi

Masoko ambapo naweza kupata matunda husika
Kodi/ushuru wa eneo

Gharama za kutengrneza meza kwaajili ya kuwekea bidhaa.

Kulingana na idadi ya mzigo, usafiri naoweza kutumia na gharama yake kwenda site.

Matunda yanayobaki njia gani hutumika kuyahifadhi ili yasioze.

Kwenye posho najua ni makubaliano ila napenda kujua walau makadirio ya chini kwa mwezi ili nisipate hasara na asione kama namnyanyasa

Na mengine ambayo sijayaorodhesha lakini ni muhimu. Natanguliza shukurani.
 
Hayo majibu unatakiwa kuwa nayo wewe! Ina maana umekurupuka kufanya biashara ya matunda????

nimecheka sana! Hivi kweli unauliza Hadi eneo la kufanyia biashara????
Kwa Hali hiyo akili yako haina tofauti na mtoto wa miaka 12
 
Kuuliza si ujinga.
 
Back
Top Bottom