Naomba kuuliza, cement huharibika baada ya muda gani?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,320
Kama ukinunua cement, ukaihifadhi vizuri, bila ya kuifingua, inaweza kuwa useful kwa mda gani? Naomba wataalamu wanijulishe.
 
Baada ya muda mrefu au mfupi!

Hilo jibu kazi kueleweka.

Hata ukiitunza vizuri, ikiwa katia mifuko hii ya kilo 50 tuliyoizoea, katika mazingira ya joto na unyevu, sementi huanza kupoteza nguvu taratibu baada ya miezi kama mitatu. Bada ya miezi 6 uwezekano wa kuwa ina nguvu kidogo sana ni mkubwa. Inategemeana sana na hali ya unyevu.

Iwapo unahitaji kuhifadhi sementi kwa muda mrefu jitahidi kutokupanga zaidi ya mifuko nane kwenda juu na pia isiguse kuta wala sakafu.

Dalili inayoonekana wazi ya kuharibika kwa sementi ni kugandamana kama jiwe. Inashauriwa kwamba iwapo kuna vibongebonge unavyoweza kulainisha kwa vidole - bado unaweza kuitumia, lakini ukihitaji nguvu zaidi kuipondaponda- hapo haifai.
 
Ikitunzwa mahara pakavu na isiwe juu ya sakafu lets say juu ya pallet inaweza kaa ata mwaka
 
Kawaida cement hasa aina ya "Portland cement" na "Portland pozzolana cement" inatakiwa itumike ndani ya miezi mitatu tangu itengenezwe kiwandani. Aina hii ndio inayozalishwa hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom