Inasikitisha namna cement inavyotumika kutunyonya; serikali mpo kimya kwa manufaa ya nani?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mfuko wa saruji (cement) kampuni ya NYATI wa 50kg unauzwa Sh20,000. Katika kila kilo moja ya saruji serikali inachukua kodi ya Sh20. Hivyo katika 50kg ya saruji kodi ya serikali ni Sh1,000 (5%).

Kiwandani Mfuko wa saruji (cement) kampuni ya NYATI wa 50kg unauzwa kwa wastani unaoanzia Sh11,000 hadi Sh13,000. Hapa tukifanya hesabu za kutoa, mfanyabiashara anabaki na Sh8,000.

Gharama za usafirishaji ni Sh4,000. Posho za vibarua wa kushusha ni Sh100. Hapa inabaki ni Sh3,900 hii ni faida ya wafanyabiashara wa kuuza saruji (cement). Nitaomba kurekebishwa popote nilipokosea.

Serikali imeeleza kwamba uzalishaji wa saruji umefika tani milioni 11 kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni tani milioni 7.5 kwa mwaka. Kwa mantiki ndogo uzalishaji ni mkubwa kuliko uhitaji.

Tatizo linakuja kwa wananchi wa kawaida, tulitataraji baada ya porojo hizi za serikali kuona bei ya mfuko wa 50kg ya saruji unashuka chini, kwanini bei imeendelea kupanda? Anaathirika nani?

Wazalishaji wakubwa wa saruji wanasema hawawezi kupunguza bei ya bidhaa wakati gharama za uzalishaji wake zimeongezeka. Hii taarifa ya meneja masoko wa Tanzania Portland Cement (Twiga Cement)

Wazalishaji wanasema uagizwaji wa vipuri kutoka nje kunachangia gharama za uzalishaji kuongezeka. Kutokana na uhaba wa dola. Wazalishaji wanauza kwa shilingi wati vipuri wananunua kwa dola.

Wazalishaji wanasema kukosekana kwa umeme wa uhakika ni sababu nyingine ya gharama za uzalishaji kuongezeka. Wanalazikika kuwa na vyanzo mbadala vya nishati ambavyo ni gharama.

Vyovyote, wazalishaji watajipangia bei ambayo itawapa faida. Hakuna mwekezaji anataka kuendesha biashara yake kwa hasara. Hapa mzigo wote atahamishiwa mnunuzi wa mwisho (mtanzania).

Hoja ya msingi, wazalishaji wa saruji hawapati hasara maana wanapanga bei ya mfuko. Serikali pia haipotezi chochote kwa kuwa wanakusanya 5% ya kodi katika kila mfuko wa 50kg wa saruji.

Wizara ya viwanda na Biashara ipo kama marehemu. Haikereki na maumivu ambayo watanzania wanapitia. Kujenga Tanzania imekuwa ni jambo la anasa. Mnataka wote tuendelee kudaiwa kodi?

From MMM (MTIKILA)

Brigedia Mtikila, MMM.
 
hiyo formula ya mahesabu ulotumia ndiyo inaitwa BODMAS eee mwalimu 🐒
 
Nchi hii sio kwamba hatumjui mchawi wetu, FISIEM shida nani atamfumga paka kengele.. We li MWAMBA WA LUSAKA toka uhuru mpaka leo linatawala lemyewe na hakuna maendeleo ya maana ukilinganisha muda wa uhuru na maendeleo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom