Chakula Kibaya
JF-Expert Member
- Sep 19, 2022
- 482
- 1,037
Habari ya usiku ndugu wanajamvi, natumai sote tuko salama na tunaendelea vizuri ujenzi wa taifa. Niende kwenye mada Moja kwa moja.
Mimi ni mjasiriamali ambaye kwa kudra za Mwenyezi Mungu nimebahatika kujenga kaboma na Sasa nimefikia hatua ya kupaua. Kuna mambo mawili naomba kufahamishwa kutoka kwenu kwani naamin humu Kuna wazoefu na wataalamu. Mambo yangu ni haya;
1. Aina zipi za mbao ambazo ni nzuri kuezekea: Kama mnavyojua Kuna aina nyingi za mbao ambazo hutumika kuezekea hivyo naomba kuelimishwa ni aina gani ya mbao ambayo ukiitumia huwa inadumu Sana bila ya kuliwa na wadudu.
Mfano Mimi Niko Mwanza mjini na nasikia wauzaji wengi wanasema Kuna mbao za BUHINDI na mbao za IRINGA. Hii kitu inanichaganya sijui wanamaanisha nini na sijui Kati ya hizo mbao zipi ni nzuri.
2. Dawa ya kutibu mbao na ufanisi wake; Hapa pia naomba kupewa elimu na ushauri juuu ya dawa zinazotumika katika hatua ya awali ya kutibu mbao kabla haijaenda site. Huwa naona Kuna baadhi ya dawa hazina rangi na Kuna dawa nyingine inabadilisha rangi ya mbao Hadi kuwa ya kijani. Swali je Kuna tija ya kutibu mbao na ni dawa ipi nzuri ya kutibu mbao?
Nitashukuru sana endapo nitapewa msaada katika hili. Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app