macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,846
- 39,710
Mimi sifahamu kuhusu hii bishara lakini bado ninaweza kukupa ushauri na sitasubiri tu kama unavyotaka. Kama uko Dar tenga siku nenda Kariakoo. Kwanza chunguza vyombo wanavyouza watu wengi vikoje na bei yake ikoje (rejareja). Hili ni rahisi sana kwani utajifanya mnunuzi. Ukimaliza hili zoezi basi ndenda kwenye maduka ya vyombo (kama huyajui unaweza kuulizia kwa ujanja). Nenda na listi yako ulizia bei ya jumla ya kila chombo unachotaka.Habari Wana jamvi muhimu kwa vijana.
Natanguliza salamu za dhati kwenu...
Suala naloleta mezani ni kwa wenye uzoefu wa biashara ya vyombo vya ndani.
Nikimaanisha
Bakuli, vikombe
Mabeseni
Majaba
Na KADHALKA
Kwa wenye uzoefu tafadhali nina mambo naomba kuyajua na kama kuna mambo ya
Umuhimu mtaya analyse.
Kwa kuanzia nina capital ya 1m
Vyombo vya plastics mfano vikombe vyupa
Vya chai bakul na kadhalka naweza pata wapi kwa bei nzuri kariakoo pia kuna
Vijana wenzetu wanaofanya hii biashara utakuta wamevimwaga wanauza 200 kila kitu au 500 pia wao wananunua kwa bei ipi
Mpaka wanaeza fanya vile au pia mpangilio upi unawawezesha kupanga katika price zile na profit inakuaje kwa wale ( to which ukiwauliza hawasemagi, wengine watakuambia tu nimeshikiza ya mtu ).
Angalizo: kama hufaham kaa tusubiri mawazo pengine nawe utafaidika au mtag unaejua anafaham wote tufaidike.
Ahsanteni.
"business is life"
Zamani maduka mengi ya vyombo yalikuwa around soko la Kariakoo ila sijui mpangilio wa sasa. All ni all, kujua maduka yalipo ni rahisi sana. Fanya utafiti wako mpaka ujiridhishe ndipo ubebe fedha za manunuzi. Wakati wa kuulizia usiende umevaa vizuri na uonekane una fedha au ubebe fedha. Nenda kimachinga style.