Naomba kujibiwa maswali haya kuhusu kanisa la KKKT

naan ngik-kundie

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,766
2,420
Habari ndugu?

Kwa kipindi kirefu sana nimeshindwa kuwa mshirika wa dini, iwe Kristo/Islamic, niliamua tu niwe mpagani na kuitumia siku ya Jumapili Kama siku ya kufanya mambo yangu mengine kuliko kwenda kanisani, lakini siku zote wakati hausimami imefikia wakati sasa wa Mimi kumrudia Mungu wangu na kutii maagizo yake na kushiriki na ndugu zangu wengine katika meza ya bwana.

Nimeamua kuwa mshirika wa kanisa la KKT lakini kabla ya kushiriki huko kuna mambo machache nilitaka kuyajua kuhusu hili dhehebu kabla ya kuanza kutii uamuzi wangu wa kushiriki Ibada kila siku, maswali yenyewe ni Kama ifuatavyo:-

1. Hili kanisa lilianzishwa mwaka gani?

2. Hili kanisa lilianzishwa na nani (Kikundi cha watu, Kiogonzi wa Koo fulani au kiongozi wa nchi au mtu fulani aliyekuwa na umaarufu Duniani.

3. Nini mchango wake katika Jamii zetu?
Kuna huduma zozote ambazo washirika wake wanafaidika na uwepo wa hili dhehebu?

4. Nini mapokeo yake katika jamii?

5. Hakuna ule ujanja ujanja kama tunavyoona kwa jirani zetu wengine,
Na wewe km muhumini wa dhehebu ili au mshirika wa dhehebu lingine una lipi unalolifaham jema au baya kuhusu KKKT?

Ahsanteni na samahani kwa uandishi mbaya.
 
Hayo maswali ni simple tu

Nenda kwenye kanisa lolote la kkkt utapata majibu ya uhakika yasiyo na uzushi wowote

Sawa mkuu lkn ninajua hapa JF nitapata majibu mazuri tu pia na ninajua siku zote wadau ndiyo wanajua zaidi kuliko wahusika, kumbuka mwamba ngozi uvutia kwake.
 
1. Lilianza mwaka 1500's
2. Alianzish Martin Luther baada ya kutofautiana na viongozi wake wa dini. roman catholic kuhusu wokovu.
3. Kusema kwa huduma za jamii wanajitahid baada ya rc wanafuatia wao kwa madhehebu wana shule hospital na vyuo vikuu
4. Ni dhehebu kubwa linapokelewa vizuri na jamii baada ya RC wanafuatia kuwa na waumini wengi
5. Ujanja unategemea na eneo ulipo ila wana regulation nzuri sadaka sio mali ya mtu ni ya kanisa na mnasomewa mapato na matumizi

Japo mie mpagani naamini nimekusaidia kujibu
 
Habari ndg?

Kwa kipindi kirefu sana nimeshindwa kuwa mshirika wa dini, iwe Kristo/Islamic, niliamua tu niwe mpagani na kuitumia siku ya Jumapili Kama siku ya kufanya mambo yangu mengine kuliko kwenda kanisani, lakini siku zote wakati hausimami imefikia wakati sasa wa Mimi kumrudia Mungu wangu na kutii maagizo yake na kushiriki na ndugu zangu wengine katika meza ya bwana.
Nimeamua kuwa mshirika wa kanisa la KKT lakini kabla ya kushiriki huko kuna mambo machache nilitaka kuyajua kuhusu hili dhehebu kabla ya kuanza kutii uamuzi wangu wa kushiriki Ibada kila siku, maswali yenyewe ni Kama ifuatavyo:-

1. Hili kanisa lilianzishwa mwaka gani?

2. Hili kanisa lilianzishwa na nani (Kikundi cha watu, Kiogonzi wa Koo furani au kiongozi wa inchi,au mtu tu furani aliyekuwa na umaharufu Duniani.

3. Nini mchango wake katika Jamii zetu?
Kuna huduma zozote ambazo washirika wake wanafaidika na uwepo wa hili dhehebu?

4. Nini mapokeo yake katika jamii?

5. Hakuna ule ujanja ujanja Kama tunavyoona kwa jirani zetu wengine,
Na wewe km muhumini wa dhehebu ili au mshirika wa dhehebu lingine una lipi unalolifaham jema au baya kuhusu KKKT?

Ahsanteni na samahani kwa uandishi mbaya.
Mungu ndo mwanzilishi wa kanisa kupitia kwa Yesu Kristo, haya unayoyaona leo sijui RC, Lutheran, Pentecostal n.k ni madhehebu na yameanzishwa na wanadamu, sasa sijajua unataka kujua kanisa limeanzishwa lini halafu na nani!!? Au unataka kujua dhehebu la Lutheran limeanzishwa na nani na lini!? Pia kama umeamua kumrudia Mungu wako usifungamane na madhehebu maana madhehebu wanapenda sana kufuata kanuni wakati kanisa linafuata neno, yaani namaanisha popote kwenye dhehebu utakaloenda iwe Lutheran au RC usifungamane na kanuni zao bali neno
 
1. lilianza mwaka 1800's.
2. alianzish martin luther baada ya kutofautiana na viongozi wake wa dini. roman catholickuhusu wokovu.
3. kusema kwa huduma za jamii wanajitahid baada ya rc wanafuatia wao kwa madhehebu wana shule hospital na vyuo vikuu
4. ni dhehebu kubwa linapokelewa vizuri na jamii baada ya rc wanafuatia kuwa na waumini wengi
5. ujanja unategemea na eneo ulipo ila wana regulation nzuri sadaka sio mali ya mtu ni ya kanisa na mnasomewa mapato na matumizi

japo mie mpagani naamini nimekusaidia kujibu

Ahsante sana mkuu kwa mchango wako mzuri, ahsante kwa kuendelea kunishawishi.
 
1. lilianza mwaka 1800's.
2. alianzish martin luther baada ya kutofautiana na viongozi wake wa dini. roman catholickuhusu wokovu.
3. kusema kwa huduma za jamii wanajitahid baada ya rc wanafuatia wao kwa madhehebu wana shule hospital na vyuo vikuu
4. ni dhehebu kubwa linapokelewa vizuri na jamii baada ya rc wanafuatia kuwa na waumini wengi
5. ujanja unategemea na eneo ulipo ila wana regulation nzuri sadaka sio mali ya mtu ni ya kanisa na mnasomewa mapato na matumizi

japo mie mpagani naamini nimekusaidia kujibu
Usimpotoshe mwenzako hujui lolote nenda kanisa lolote la KKKT utapata majibu
 
Mungu ndo mwanzilishi wa kanisa kupitia kwa Yesu Kristo, haya unayoyaona leo sijui RC, Lutheran, Pentecostal n.k ni madhehebu na yameanzishwa na wanadamu, sasa sijajua unataka kujua kanisa limeanzishwa lini halafu na nani!!? Au unataka kujua dhehebu la Lutheran limeanzishwa na nani na lini!? Pia kama umeamua kumrudia Mungu wako usifungamane na madhehebu maana madhehebu wanapenda sana kufuata kanuni wakati kanisa linafuata neno, yaani namaanisha popote kwenye dhehebu utakaloenda iwe Lutheran au RC usifungamane na kanuni zao bali neno

Nimekuelewa vizuri sana, lengo langu siyo kufungamana na dhehebu lolote maana yangu ni njema kabsa, kaka inapendeza kujua haya mambo maana kesho watoto watakuuliza jambo kuhusu dhehebu unaloahudu na utashindwa kujibu, inapendeza Kama ukikijua unachokiamini.
 
Back
Top Bottom