Askofu Bagonza acha kulichafua Kanisa la KKKT

CRISTA

Member
Aug 5, 2012
78
24
Hivi karibuni hapa Jamii Forum tumeshuhudia Tamko kutoka kwa Askofu Bagonza likimshutumu Aliyekuwa Askofu Mkuu wa KKKT Dr.Fredrick Shoo.

Kauli hii inasikitisha sana ikizingatiwa ni Kiongozi Mkubwa sana wa Kanisa la KKKT.

Maswali ya muhimu kwako

1.Kwa Nini uliamua Kutoa Mambo ya KKKT mitandaoni!?Hakuna taratibu sahihi za kufikisha Ujumbe huo kwa Wana KKKT tofauti na hiyo njia uliyotumia!?

2.Tunafahamu kuwa wewe na Dr.Fredrick Shoo hampatani na hii ilitokana na na ujuaji wako,Je hii ni njia sahihi ya kumkaanga dr.fredrick Shoo Mitandaoni

3.Tunafahamu KKKT Ina vituo vya kazi za umoja ikiwemo Viziwi Njombe na Mwanga pamoja Junior seminar Morogoro na wewe ni mmoja wapo ambaye upo kwenye Halmashauri kuu ya KKKT ambapo mnachangia Mambo mbalimbali ya ustawi wa vituo hivyo.Swali langu ni kwamba a)Mpaka Vituo hivyo vinaingia kwenye madeni hayo ulikuwa Wapi!? Kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu!?

b)Vituo vya kazi za Umoja Vinaongozwa na Bodi ya Shule inayoongozwa na ASKOFU wa Dayosisi, inayochaguliwa na Halmashauri Kuu ambapo wewe umo ndani Vipi kuita wengine wazembe

C)Kanisa la KKKT linaye katibu Mkuu ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kanisa kulikoni hasira kuishia kwa kwa Dr.Shoo

4.Vipi kuhusu Dayosisi yako una uhakika hauna malalamiko na wafanya kazi wako,je wanafurahia uongozi wako!?

Mwisho Dr.Fredrick Shoo ni Askofu aliyerudisha heshima ya kanisa letu pendwa,na hasa katika kipindi chake kilichokuwa ma mitikisiko mingi.

Tunakusihi Ask.Bagonza usitugawe kama kanisa kwa sababu tuu ya Chuki binafsi na Dr.Shoo badala yake kaeni myamalize na kuleta upendo katikati yetu waumini wa KANISA letu Pendwa.

Lidumu Kanisa letu KKKT
 
Askofu Bagonza japo Mimi muislamu ila anaonekana yupo desperate na kitu ambacho yeye mwenyewe hajui kitu Gani anataka. Anahangaika sana japo anajifanya mwana philosophy.
 
Back
Top Bottom