Naomba Guta la mkataba Njombe

Bongo Trust

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
252
241
Wakuu kama post inavyo jieleza, mimi ni dereva wa Bajaj na Guta mkoa wa Njombe wilaya ya Makete na leseni ninayo. Ninauhitaji na guta la mkataba aina ya Sinoray Q7 kama hili nililoweka kwenye picha.

Dukani Guta hili linauzwa million sita na laki saba (6.7M) Mkataba utakuwa wa muda usio zidi mwaka mmoja na miezi mitano, marejesho yanakuwa ya kila wiki , yaani kila mwisho wa wiki (jumapili) nitakuwa napaswa kurejesha shilingi laki mbili ambapo inakuwa sawasawa na shilingi million 12 baada ya mkataba kuisha.

Kwa wale wanaotoa mikataba ya Bajaj njombe au mdau mwingine yeyote naomba anisaidie nipate Guta hili.

NB. Service zote ndani ya kipindi cha mkataba zitakuwa juu yangu.

Natanguliza shukran 🙏.

images - 2023-11-18T112229.837.jpeg
 
Ni pm
Kuna Bajaj jamaaa yangu anayo mafinga kama hajapata mtu naeza kukuunganisha, nitampigia.
Angalizo:uwe tayari kuandikiana kwa mwanasheria, polisi, pia mahakamani
 
Hilo guta mpaka likaa barabarani kila kitu bei gani jumla maana umeweka bei ya kununua tu.
 
Kweli boss hapo inaongezeka bima 95000 na Sumatra 22000 kwahiyo jumla inakua 6,817,000
Halafu mbona mahesabu yako ni kama hayana uhalisia; umesema makadario ya kika siku ni shs 29000/=. Hii ukizidisha kwa siku saba (wiki), unapata shs 203000/=, na umesema kila wiki unapeleka kwa bosi shs 200000/=, ina maana kwa kila wiki wewe utaambulia shs 3000/=! Je, ulikusudia kusema hivyo au umekosea kuandika?
 
Halafu mbona mahesabu yako ni kama hayana uhalisia; umesema makadario ya kika siku ni shs 29000/=. Hii ukizidisha kwa siku saba (wiki), unapata shs 203000/=, na umesema kila wiki unapeleka kwa bosi shs 200000/=, ina maana kwa kila wiki wewe utaambulia shs 3000/=! Je, ulikusudia kusema hivyo au umekosea kuandika?
Sina maana hiyo mkuu nilicho kadiria kwenye 29000 ni hela ya marejesho ila maana hata ukigawa 200000 kwa 7 unapata 28571.42.. ndio nikapiga approximation ya 29000.

Ila kama muulizaji alitaka kujua jumla ya kipato nachopata kwa siku, jibu ni siku hazi fanani, kuna siku naweza laza 40,50 au zaidi au kukiwa kubaya sana napata 20,25 nk.

Ila nikizichanga kwa wiki kupata 200k ni uhakika. Maana ni kazi ambayo nimeifanya na ninauzoefu nayo kabisa.

Karibu boss
 
Wakuu bado sijapata Guta, naomba aliye na uwezo wa kulinunua anisaidie anunue anikabidhi tufanye hii biashara, hatakama kuna mtu unajuana nae na anaweza kunipa mkataba basi tusaidiane kuniunganisha nae ili tuweze kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom