Barua ya wazi kwa Rais Samia kuhusu tazizo la huduma ya maji nchini

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutupatia uhai na afya njema. Pili, namshukuru Mungu kwa kutupatia rasilimali lukuki ambazo kwa kutokufahamu kwetu nadhani tushatumia si zaidi ya asilimia 30% kwasababu hatujui tuzitumieje ili zitunufaishe!

Nafahamu hapa Mh.Rais hawezi kuwepo ila naamini kuna watendaji wa serikali ambao kila kukicha wanazurura hapa jukwaani kutafuta wakosoaji ili wawashughulikie,sasa naomba wote mlioko humu ndani (POLISI, TISS, JWTZ, JKT, UHAMIAJI, RC,DC, WAKURUGENZI, RAS, DAS, WENYEVITI, WAKUU WA IDARA) naomba mumfikishie ujumbe huu Mh. Rais.

Mimi ni mtanzania ambaye nakerwa sana na haya mambo yanayoendelea kwasasa kwenye nchi yetu ya Tanzania.

Mambo yenyewe ni 1. Ukosefu wa maji salama ya kutumia majumbani 2. Mgao wa umeme unaoendelea Kote nchini.

Mh. Rais nchi yetu imebarikiwa rasilimali maji kila ukanda,Kanda ya pwani (Tanga, Dar, Pwani, Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Morogoro) hawa wana bahari kubwa ya Hindi.

Kanda ya ziwa (Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Kagera) hawa wanalo ziwa kubwa la Victoria.

Kanda ya Magharibi(Kigoma, Rukwa, Katavi, Songwe) hawa wanaloziwa kubwa ambalo ni Tanganyika.

Kanda ya kusini(Mtwara ingawaje sehemu ipo bahari, Ruvuma, Njombe) hawa wana ziwa Nyasa na mto mkubwa unaotenganisha Tanzania na msumbiji.

Kanda ya Nyanda za juu kusini (Mbeya na Iringa, na sehemu ya morogoro)hawa wapo jirani na ziwa Rukwa pamoja ziwa Nyasa.

Kanda ya kati (Dodoma, Singida, Manyara)Hawa wana ziwa Manyara, Ziwa Singidani n.k

Kanda ya Kaskazini(Arusha na Kilimanjaro)Hawa wanabwawa la nyumba ya Mungu,ziwa jipe, n.k

Swali.

1. Sasa pamoja na Rasilimali maji hizi. Je, ni kwanini hatuna maji?

2. Ni kiasi gani cha fedha hicho ambacho tumeshindwa kukipata kama taifa kwa miaka yote tangu tumepata uhuru ambacho kinapaswa kuondoa hii kero ya maji?

3. Je, kipaumbele cha serikali yako kwa watu wake ni kipi?

4. Je, ni furaha ya serikali yako kuona watu wanahangaika na ukosefu wa maji?

5. Ni lini tutegemee hii kero ya maji kuisha kabisa kwenye Taifa letu na ibaki historia?

Hivi ni kitu gani kinakwamisha mambo haya? Huwa najiuliza maswali nakosa majibu Mh. Rais, tafadhali nisaidieni ili nielewe. Je,ni kitu gani kinafanya tunakosa maji ya uhakika wakati nchi kama Dubai ambayo ni nchi ya jangwa wao wanapata maji ya uhakika?

Hapa ninapokaa, hii ni siku ya 14 leo hakuna maji,sasa kama jiji kubwa kama Dar es salaam linakosa maji kwa muda wa wiki mbili huko mikoani hali ikoje?Je, Watanzania tusizungumzie haya? Je, tunaposema viongozi wetu akili za utatuzi wa shida za watanzania zimefika mwisho tutakuwa na makosa?

Hao wasaidizi wako wanaosimama kwenye majukwaa na kutamka bila aibu ya kwamba tuombe Mungu mvua zinyeshe ili uhaba wa maji uishe, nitakuwa na makosa kusema hawana akili? Mh. Rais naomba unijibu pengine mimi ndiye sielewi.

Pia hili suala la umeme limekuwa kama hisani na wakati ni jukumu la viongozi kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika. Je, ni lini hili suala la umeme litaacha kusumbua? Ni kwanini mnajenga bwawa la matrilioni ya shilingi kama mnajua umeme wetu unategemea maji ya mvua ambayo mvua isiponyesha tunarudi kulekule? Hayo matrilioni kwanini msingewekeza kwenye vyanzo vingine vya umeme?.

Hivi ni kwanini mnatufanyia watanzania hivi? Ninafahamu Mh. Rais wewe hutishwi na porojo za Watanzania kwasababu unalo jeshi, polisi na vyombo vingine kwa ulinzi ambavyo unaweza kuagiza tu fulani ashughulikiwe na vikatekeleza agizo, lakini kwanini serikali yako haina huruma na maisha ya mateso wanayopitia Watanzania?

Ninafahamu serikali yako na chama chako mtaongoza milele, lakini kwanini msitatue kero za muda mrefu za watanzania?

Hiyo mikopo ambayo serikali yako inaenda kukopa kwa niaba ya Watanzania huwa inawanufaishaje watanzania kama umeme na maji ni kero? Hiyo mikopo inafanya kazi ipi? Je, ni kitu gani kama nchi tunanufaika nacho kupitia hiyo mikopo kama hatuna umeme na maji ya uhakika?

Kwanini mnatufanyia hivi watanzania? Nyie viongozi nafahamu kabisa hamuwezi kukosa maji na umeme hapo Ikulu na majumbani mwenu na ndiyo maana haya matatizo wanayopitia watanzania kwenu ni marashi mazuri na yenye harufu nzuri!

Mh. Rais naomba watendaji wako wanijibu. JE, NI LINI SERIKALI YAKO ITAONDOA HAYA MATATIZO KWA WANANCHI?

NAKEREKA SANA!

Kwa leo ni hayo tu!
 
Sio kosa lake yeye kaingia juzi tuu kakutana na hili balaa..
Mpeni kumi mingine atamaliza hii shida.mumre
 
Hapo daslam mambo ni magumu kwel.

Mikoani wananchi wa kipato cha chni chini njaa inampango wa kufanya mauaji, sijuwi polisi kama wataweza hilo pambano!
 
Nipo siti namba 12 na madumu yangu nawahi mtoni kwenye foleni alafu jua kaaali, mvua zinanyesha Mwanza & Geita tu
 
Sisi tumeunganishiwa maji mwezi huu, namshukuru mama kwa kweli ,tumekula msoto wa muda mrefu maji chumvi hata chai hayafai tuliishi nayo kwa gharama ya sh mia mbili kwa ndoo. Subira yavuta heri

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom