Naomba anayejua procedure za kukata rufaa matokeo ya ualimu necta

Hayo matokeo nimeyaona hata mdogo wangu. Akipata F ualimu hata km yote ana A atakuwa amefeli. Na njia ni kuresit tu pale chuoni aliposoma. Kuappeal ni kupoteza hela na muda. Hilo somo sio gumu sema ni dharau ndio wengi wanafeli.
 
Ahsante bwana kiumbo kwa maelezo yako mazuri,umenifungua macho,vizuri na ahsante sana,lakini nasikitishwa na wana jamiiforum wenye lugha za kejeli na majigambo,nimefedheheshwa sana na wanaoniuliza upuuzi badala ya kujikita kwenye tatizo langu,kama kuna kitu muhimu tunakosa watanzania ni adabu na kuwa serious..
 
Jf imevamiwa na watu wa facebk na itakadi. Tujenge tz moja kwa fikra chanya na pevu. Wao wakienda mwezini na anga la juu sisi twendeni vijijini tukaboreshe kilimo na ufugaji. Mwl.Nyerere.
 
ninachojua mimi ni kulipia ada ya rufaa, kama elfu 20 hivi, ila kwa taarifa zaidi fungua www.necta.go.tz utapata taarifa kamili. pole sana heri angefeli somo lingine tofauti na somo la ualimu hyo ni total disqualification.
 
Ahsante ndugu yangu fikirini,nimedownload fomu yao ina kurasa tatu,masomo yote ana B isipokuwa somo la ualimu,ngoja nimsaidie ni binti mpwa angu na kwa dunia ya leo wasichana wanakosa mwelekeo kwa kukosa kitu kitakachomfanya awe bize,ni bora awe mwl wa primary kuliko ungemwacha akazubaa mtaani akiwa tegemezi maisha ake yote,pia nitaangalia uwezekano wa kurisiti
 
Back
Top Bottom