Nani Katuloga watanzania??Dawa imepatikana na ni hii hapa

Jamani ndo hali halisi, watu wamelala njaa lakini wanaamka asubuhi wanakuja kushangilia mzee wa vijisenti kwa kuwa yeye ni CCM na wamemwambia lazima aende. Kazi kubwa bado hipo ya kuwalimisha wananchi wa kawaida umuhimu wa kuachana na ushabiki wa kisiasa ambao CCM inacapitalize hapo.

Mimi nakwambia hata balali akirudi leo akagombea uraisi kupitia CCM watu watampa kura.
 
chengesafisha.jpg

wananchi wa kijijini wakimpigia makofi chenge jana.hawa ndio ambao hawajui tulipo na wanatutegemea sana sisi kuwaleza wapi tulipo na tunaelekea wapi​
Wanajua wanafanya nini, Kuna kitu kinaitwa mapenzi na hao wananchi bado wana mapenzi na mbunge wao. Sasa unapowahukumu kuwa hawajui chochote ni kufanya waendelee kuwa na mapenzi zaidi na mbunge wao.

Hakuna mtz ambae hajui nini maana ya ufisadi... Iwapo Bosi wake angemtimua kazi ya uwaziri kabla ya yeye kutamka kuwa anajiuzuru, na kuwepo kwa mapokezi ya namna hiyo kidogo kauli yako ingekuwa na nafasi. Lakini kwa sasa umeamua kuhukumu tu kwa utashi wako binafsi.
 
Jambo ambalo naweza kusema,Hawa wananchi wana mapenzi na chama chao na sio mapenzi na Bwana Chenge.

Na kwa mfano mdogo tu,unaweza kupata mwanamke mzuri aliyeumbika na mwenye akili nyingi sana au mwanaume mwenye sura nzuri na rijali na akawa mpenzi wako wa muda mrefu ila baada ya muda ukasikia amepata ugonjwa mbaya zaidi ya hata gonjwa la ukimwi,na wewe haujaathirika na ugonjwa huo,na ukagundua kwamba jamaa ambaye unampenda kaugua ugonjwa huo na wewe ukawa haujaathirika na ugonjwa huo na kama ukeindelea kujamiiana naye utaupata ugonjwa huo na utakuathiri kisailojia.Je utaendelea kushirikiana naye kimapenzi??utanedle akuwa na mpenzi huyo..Je utaendelea kuwa na huyo FISADI.No way kibunango!!

wananchi wanampenda chenge sababu hawataki kumbagua,wana mapenzi kama ndugu yao tu ila siyo kwasababu yeye ni fisadi,na kama asingekuwa ndugu yao kichama hata Wasingemfurahia hivi.,

Mie nina kuhakikishia,toka Dar es salaa,nenda mbali kidogo katika vijiji vya nyamatara,nyamageni huko kanda ya ziwa ndani ndani au nanyumbu huko Mtwara ambako hawajawahi kusoma gazeti kama Mwanahalisi,nakuambia utashitushwa na mapenzi yao kwa Lowassa hata huyu Muungwana wamsifiaye .
 
Jamani ndo hali halisi, watu wamelala njaa lakini wanaamka asubuhi wanakuja kushangilia mzee wa vijisenti kwa kuwa yeye ni CCM na wamemwambia lazima aende. Kazi kubwa bado hipo ya kuwalimisha wananchi wa kawaida umuhimu wa kuachana na ushabiki wa kisiasa ambao CCM inacapitalize hapo.

Mimi nakwambia hata balali akirudi leo akagombea uraisi kupitia CCM watu watampa kura.
Jamco,
Unafahamu Bwana cheneg alishinda vipi,katika watu ambao walishinda kwa taabu sana kupitia tiketi ya CCM ni huyu Andrew.alitumia pesa nyingi sana kushinda na nakwambia 2010 ndiyo mwisho wake sababu watu watamtoa kwa kishindo.

Na huu ukaribu wa waandishi wa habari na wanasiasa ndio unakatisha tamaa,wakati mwingine huwa natamani hata kuacha kuzunguzmia mambo ya nchi hii,ila hapan...oh No nitasema mpaka nitakapoona wamebadilika.
 
Kamanda Gembe:
Katika risala yao wamesema bayana kuwa wanapinga kauli ya Umoja wa Vijana(CCM) Tanga kwa kuwataka wale wote waliotuhumiwa na ufisadi wajiuzuru katika nafasi zao za ubunge. Hili unalichukulia vipi na aina ya mapokezi hayo?

Uoni kuwa kuwa tatizo katika kutekeleza majukumu kwa kiongozi wa juu kabisa ambae uteua mawaziri wake kukaa kimya kwa wamaziri hao kiasi cha kuwapa nafasi ya kujiuzuru na baade kwenda kujinadi upya kwa wapiga kura wao kuwa wamechukua hatua hizo kwa manufaa ya umma ilhali ni watuhumiwa?

Wananchi na hasa wanaoshiriki kwenye kupiga kura, mara nyingi wanaongozwa na mapenzi binafsi ya mgombea wao. Jinsi anavyojieleza na jinsi anavyoweza kutatua matatizo yao. Na Iwapo inatokea huyo walie mchagua kukumbwa na matatizo na akajiwahi kujitetea mbele yao mapenzi kwake uongezeka licha ya maneno ya chinichini kuwa wanakuwa mameandaliwa kufanya hivyo.

Kama kutojua kinachoendelea ni vema lawama hizo zikaelekezwa kwa bosi wake mkuu kwa kumpa nafasi ya kujiuzuru badala ya kumtimua kazi. Sidhani kama JK angetamka kuwa amemfukuza kazi kungekuwepo na mapokezi ya namna hiyo.
 
Kibunango,
1.Jk ni mtu mmoja wa ajabu sana kwa maoni yangu sababu ameshindwa kuyatolea majibu maswali magumu,watawala na wasaidizi wenzake wanamuita na kusema ni Mvumilivu,Ansbert ngurumo anasema ukitaka kumjua mtu angalia rafiki zake,atakuwa anafanana nao,Mie naungana na Ngurumo katika Hili,yeye ni kama wao ndio maana ina mchukua muda yeye kuwachukulia hatua sababu ni rafiki zake.Tabia ya Unafiki.

2.UVCCM na CCM ya mkoa wa Tanga ndiyo CCM ile ambayo iliachwa na Mwalimu,CCM ambayo ina fuata misingi ya Utu na ndio maana kila siku huwa wanampinga makamba katika mambo mengi,wanataka haki kwa ajili ya wafanyakazi na walimu.kwa maana nyingine hawataki CCM ya wafanya Biashara.wamejaribu kuwalazimisha wajiunge nao ila wameshindwa na kama unakumbuka ndio maana niliwahi kushinikiza makamba ajiuzuru. watu wakamtetea,ila hawa watu wa mfano wa makamba ndiyo wanawakumbatia hawa wala rushwa na Mafisadi.Kumbuka ni nani alimtetea Lowassa sisulubiwe mbele ya JK??
 
Kamanda Gembe;
Nakubaliana na wewe juu ya misimamo ya UVCCM-Tanga, Nikiingia kichama(CCM) nafasi ya Katibu Mkuu wake hivi sasa inasimama katika kusimamia mipasho, hii ni sawa na aliyekuwa bingwa wa mipasho katika medani ya siasa ya vyama vingi Rais wa Awamu ya Tano huko visiwani. Katibu Mkuu wa sasa amewekwa pale ili kujibu tuhuma mbalimbali kwa staili ya mipasho ambayo hupendwa katika masikio ya Watz wengi (chunguza kasi ya kupanda chati kwa magazeti ya udaku leo hii Tz).

Hata hivyo kwenye ukweli ni lazima usimamiwe kwa gharama zote, Bosi kubwa kwa namna moja ama nyingine anaanzisha namna mpya ya kuwatetea mafisadi kwa kukaa kwake kimya. Iwapo kweli tuna uchungu na haya yanayoendelea sasa ni vema kumbana bosi mkuu kuliko kurusha lawama kwa watu wa vijijini. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumekata mzizi wa fitina.
 
watanzania siku zote tumekuwa tukiongozwa na ushabiki, si kwenye siasa, si kwenye michezo, si kwenye kuiga mila mbovu za kigeni.
na hii tabia ndio imetufikisha hapa tulipo.

as long as kiongozi ni ccm na alichaguliwa na JK, basi lazima msafi japo kama amejiuzulu kutokana na kutuhumiwa ufisadi.

watu wanakubali kuamini kwamba ni propaganda za upinzani zinazotaka kumharibia.

upinzani have a long way to go, kwa kuwafunza watu kwanza kuacha ushabiki na kuangalia facts kuanzia ngazi za uchaguzi wa viongozi wa kata, mpaka rais.
 
Wana JF naona kama seriousness inaanza kuwepo. Tunapohama toka katika kulalamika na kupanga mikakati. Tena kugundua lile ambalo mafisadi walilifahamu zamani na ku take advantage. Ukweli ni kuwa watanzania wa kawaida kijijini hawaelewi yote haya yanayoendelea maana yake nini na tafsiri yake kwa maisha yao ni ipi? Kulaumu wanavyopewa bia na khanga wakanunuliwa katika uchaguzi ni kuwaonea. Hawajui tafsiri yake kwenye maisha yao ya kila siku ni ipi. Hawajui kuwa kuna athari yoyote kwao. Wanadhani wamemkomoa mhesh. Mgombea. Na mbaya zaidi nguvu ya watu wa vijijini maskini wameiwekeza kwa vijana wao wakawasomesha baadhi yao nao wanapofanikiwa hawakumbuki lolote la kuwasaidia wazee na jamii zilizojitoa mhanga kuwatafutia elimu. Wasomi wetu wako wako Ulaya na Marekani wanakula kuku wakati waliohangaika kuwatafutia ulaji huu wamesahaulika. Ndiyo MH Gembe kampeni irudi kjijijini kuwaelimisha maana ya demokrasia ya vyama vingi ni nini. Vuguvugu lirudi huko kueleza kuwa wao ndio wenye nchi na sio watawala. Mfumo wa kichifu waliozoea uliwaweka wananchi kuwa mali ya watawala na raslimali zote zilikuwa za mfalme. Akifurahi anawagawia raia wake. Wananchi wengi wanadhani mfumo huu bado unaendelea...
 
Omulangi,
Nakumbuka maana yake ni kiongozi kama sikosei,karibu JF,
Hoja zako ni nzuri,na mkakati ndio huo tumeanza kuuweka kuanzia mwezi huu kuelekea 2010,kung'oka kwa watu ambao ni utouchables ndio lilikuwa lengo kuu la kwanza,pili ni kuhakikisha wanapata anguko linginine la tatu.

Dhumuni letu ni kutoa wale wote ambao wameshalewa mvinyo kwa madraka na kuweka watu wanaotaka maendeleo na wanaopenda kuona jambo gumu linawezekana.Tunahitaji Rais ambaye atamtumia mkurugenzi wa kurugenzi ya mawasialiano ikulu kumsaidia kuongea na waandishi wa habari kuhus mabo muhimu yanayohusu watanzania
 
Nani katuloga!

Sisi hatujalogwa ila ni wapuuzi na hasa ambao tuna macho tumekuwa wapuuzi sana. Mpuuzi hapa sio tusi ila ni namna mtu anavyoacha kufanya kitu cha maana na kuammua kufanya kile ambacho hakina maana

Ni kweli kabisa tunashabikia mambo ya kipuuzi na tukipewa kidogo tunakula na kulala bila kutambua kuwa tukiamka tumbo litadai halali yake.
Elimu iongezwa ndiyo jibu sahihi na hii itolewe na Mwalimu Mkuu

Tumerogwa, dawa zikiisha muda wake tutarudia fikara zetu
 
Obe,

sidhani kama tumefikia levela ya siye kuwa wapuuzi,jamba ambalo naweza kukubaliana nalo ni kwamba ttumekuwa washabiki wa mambo ya kipuuzi.

Siku zote kama mali ikipatikana kwa kutumia uchawi ni jambo baya sana na huwa ina athari mbaya sana huko mbeleni,nahisi kama kuna jambo nisilololijua ila ni uwkeli ninaoufikiri siku zote,

Natamani kwenda kuongea na babu aniambie Tanzania tumetoka wapi na kwanini tuko hivi mpaka leo,Ujinga Umasikini bado uko pale pale,hata isasa safi imetushinda sababu imeingiwa na warohgo wa madaraka wanaopenda kuona wao kila siku wanawataabisha watanzia wengine.
 
Back
Top Bottom