Nani anapaswa kuwa na muhuri wa Serikali ya Kijiji kati ya Afisa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji?

Wababa13

Senior Member
Dec 27, 2017
105
70
Naomba kufahamishwa kwa uchache tu.

Je, ni nani anapaswa kuwa na muhuri wa Halmshauri ya kijiji kati ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kijiji? Muhuri huu ni tofauti na Mihuri ya Afisa Mtendaji au ule wa Mwenyekiti.

Kuna Mihuri special huwa inaitwa Mihuri ya Halmshauri ya Kijiji, ambayo huwa inakuwa na namba ya Kijiji (namba ya usajili wa Kijiji).

Majibu tafadhari 🙏🏾.
 
Mwenye mamlaka na serikali ya kijiji ni mwenyekiti wa kijiji

Hivyo yeye ana takiwa kuwa na muhuri huo, japo siku hizi wana pewa kwa mashart sababu wana fanya mambo tofauti kupelekea migogoro kwa maslahi binafsi

Mwenyekiti wa kijiji ni Boss katika kijiji, ni kiongozi wa wananchi

Ana wawakilisha wananchi hivyo ndio mwenye serikali yake

Ni kama diwani katika kata ambaye anaweza muwajibisha mtumishi wa kuajiriwa

Na baraza la madiwani wana weza chukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wa kuajiriwa

Hivyo kuwepo kwa hawa watu wa kuchaguliwa na wananchi ni kwa makusudi mazima ili waweze kuisimamia serikali kama walivyo wale wabunge pale bungeni wanavyo isimamia serikali na ndio wana wawakilisha wananchi

Serikali ni ya wananchi kumbuka hilo kwa nazani katiba 1977 imenena vyema
 
Mtendaji ndo official anaetambuliwa na serikali mkuu hawa wenyeviti wahuni wahuni tu
Wote wana tambulika na serikali na wana madaraka yanayo tambulika na wamepewa hiyo mihuri

Mwenyekiti wa kijiji ana wake
Mtendaji wa kijiji ana wake pia

Hivyo wote wana tambulika na wana fanya kazi ktk eneo Au mamlaka inayo tambulika chini ya sheria za serikali za mitaa na nchi kwa ujumla wake
 
Mwenye mamlaka na serikali ya kijiji ni mwenyekiti wa kijiji

Hivyo yeye ana takiwa kuwa na muhuri huo, japo siku hizi wana pewa kwa mashart sababu wana fanya mambo tofauti kupelekea migogoro kwa maslahi binafsi

Mwenyekiti wa kijiji ni Boss katika kijiji, ni kiongozi wa wananchi

Ana wawakilisha wananchi hivyo ndio mwenye serikali yake

Ni kama diwani katika kata ambaye anaweza muwajibisha mtumishi wa kuajiriwa

Na baraza la madiwani wana weza chukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wa kuajiriwa

Hivyo kuwepo kwa hawa watu wa kuchaguliwa na wananchi ni kwa makusudi mazima ili waweze kuisimamia serikali kama walivyo wale wabunge pale bungeni wanavyo isimamia serikali na ndio wana wawakilisha wananchi

Serikali ni ya wananchi kumbuka hilo kwa nazani katiba 1977 imenena vyema
Una uelewa mdogo mhuri Unatakiwa kuepo kwa mtendaji wa kijiji. Sio mwenyekiti yupo tuu pale Kwa mambo ya kisiasa tuu ila kiutendaji ni mtendaji wa kijiji tuu . Mtendaji kaajiliwa na serikali ni mtumishi wa serikali kosa lolote lile anawajibishwa Kwa kutumia Sheria na kanuni za kiutumishi......
 
Siwezi bishana na mtu mwenye uelewa mkubwa...

Level zangu ni kwa wenye uelewa mdogo, wanao tambua mamlaka za serikali za mitaa kwa sheria zake

Wanao tambua majukumu ya kila mmoja katika kijiji

Pia wanao fahamu agizo la waziri wa tamisemi simbachawene kipindi hicho kwanini alilitengua? Sababu alikuwa kinyume na sheria, Ali kosa nguvu kisheria kufanya hivyo

Kuwa mtumishi wa umma wewe mtendaji hakukupi mamlaka ya kumiliki muhuri wa shule ya msingi Au kituo cha afya

Nipo hapa kuwa eleza wenye uelewa mdogo sipo hapa kubishana ewe mwenye uelewa mkubwa ambaye unaelewa ni vyema ukabakia hivyo hivyo na huo uelewa

Ila nakushauri, pata muda wa kujielimisha kuhusu serikali za mitaa, ili eneo usije kwa kukurupuka siku nyingine wakati hakuna unacho kifahamu
 
22 Basi, tuambie kama ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”
23 Yesu akawaambia, 24 “Nionesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?” 25 Nao wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
 
90F6EADA-3176-468D-BF5D-66170474ACC9.jpeg

Huu ni muhuri wa afisa mtendaji, umejieleza vyema kabisa ni mtendaji na kijiji chake na wilaya yake...

11C85953-F5FC-4AF0-86DF-3A4FACE58153.jpeg

Huu ni muhuri wa mwenyekiti wa mtaa/kijiji ambao umejieleza vyema kabisa ni muhuri wa mwenyekiti wa mtaa/kijiji fulani katika wilaya fulani

Shida ni kuona wenyeviti ni kama wapo tu hawana maana yoyote kisa sio waajiriqa wa kudumu kwa kuwa nafasi zao zina tokana na nafasi za kisiasa

Elimu ndogo sana kwa wadau, sababu Kila mtu ana muhuri wake hivyo kutaka kuchukua muhuri wa mwingine ni kuonesha una tatizo sehemu
 
Back
Top Bottom