Songwe: Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Iwalanje ahukumiwa kwa Ubadhirifu, Ufujaji na matumizi mabaya ya Madaraka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,029
1,646
Juni 21, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, imetolewa hukumu ya kesi ya Uhujumu Uchumi No.05/2023 iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mhe. Shangwe

Mshtakiwa katika kesi hii ni Bw. Jisenge Salum ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Iwalanje Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya Matumizi mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 na ufujaji na ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28 (1) vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Mshtakiwa alikiri kosa na kutiwa hatiani hivyo mahakama imeamuru Mshtakiwa kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka Minne (4) Jela kwa makosa yote mawili au kulipa faini ya Shilingi 2,300,000/=.

Hukumu hii inaenda sambamba na kutakiwa kurejesha kwa Mwajiri wake (Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi), kiasi alichoiba cha Shs. 5,849,900/= ambacho Mshtakiwa amesharejesha kwa Mwajiri.

Waendesha Mashtaka katika kesi hii walikuwa ni Simona Mapunda akishirikiana na Conrad Kabutta.

Chanzo: TAKUKURU
 
W
Wanawaonea tu hao.
Watu siyo Wahasibu na wala hawajasomea taaluma ya Uhasibu, Je, inakuwaje wapewe majukumu ya kufanya kazi za ki-hasibu nje ya Majukumu yao ya msingi ktk kazi ya Uafisa Mtendaji wa Kijiji au kata??
Kwa nini Halmashauri za Wilaya zisiwaajiri Wahasibu ktk Ofisi za Kijiji na kata ili wafanye kazi hizo za Uhasibu??
 
Back
Top Bottom