Nani anaiongoza CCM?

Mzee MMJ,

Kwa taratibu za ccm, huwa hakuna mwanachama anyeruhusiwa kutoa malalamiko yake nje ya vikao vya chama, kwa hiyo hakuna kiongozi wa ccm anyeweza kufanya hicho kitendo, na kuna mifano miwili aliyotokea karibuni, kwanza ni DR. KITINE, halafu ni Mzee Sozigwa, ambao walijaribu kuvunja hiyo ilani wakaishia kukaripiwa sana na cccm, na mpaka leo sidhani kama tumeshawasikia tena!

Mzee Lunyungu,

With all respect, kazi ya makamu wa ccm, ni kupambana na upinzani na ikiwezekana hata kuuvunja kabisaaa, ccm ni chama cha siasa sio cha upadri, na hakuna mwananchi yoyote mjinga anyefikiri kuwa watawala kama ccm ambao wamekuwa kwenye power for 44 years, wanaweza kuachia madaraka hivi hivi tu, na kama huamini muuulize Mrema.

Sasa ni mategemeo yangu kuwa vyama vyote vya siasa nchini vitakuwa either na kiongozi mmoja katika system yake ambaye kazi yake itakuwa ni ku-deal na mbinu za kupambana na vyama vingine, ambazo ni within na outside ya legal system, ndio maana Nixon alikamatwa na watergate, au kitengo maalum ndani ya chama cha kupambana na vyama vingine, kwa maneno yako hapo juu inaonekana kuwa huenda vyama vyetu vya siasa havina hiyo kitu, na ndio maana matokeo ni yale yale kila siku, pamoja na uozo wote tulionao bado ccm hushinda tu, tena ilimfanya mpaka mwenyekiti wa chadema ashindwe kuwaelewa wananchi kutokana na matokeo ya uchaguzi wa rais uliopita,

Kuanza kuongelea atakapoacha kazi hiyo, ni dalili za kusihiwa hoja na kwenda low za unafiki, majungu, na uzandiki, yaani aliye juu mngoje chini, wakati siku hizi huwa tunamfuata huko huko juuu, tunapotaka cha uvunguni siku hizi huwa hatuinami ila tunabenua kitanda, kwa hiyo lets talk the influencial na what is the influence na where the line is drawn, na faida na hasara zake kwa taifa letu, badala ya akiacha kazi itakuwaje hivi huoni kuwa hiyo ni very low thinking kuwepo kwenye hii forum tukufu?

Kuna anayesema kuwa Mama Sitti naye pia husafiri, man! huyu Mama ndio husafiri lakini kwa nauli yake binafsi sio hela za serikali kama makamu wa ccm ambaye husafiri 1st Class na entrouge yake, Mama Sitti hulipiwa na serikali pale tu anaposafiri na mumewe kwenda kwenye matibabu au safari za kiserikali, otherwise hana hela za kulipa 1st Class, na mimi binafsi sina tatizo na serikali yetu kuwakarimu viongozi waliolitumikia taifa letu kwa mpaka kutufikisha hapa tulipo, unajua mara ya mwisho Kaunda alipokuja bongo alisema kuwa he was impressed na tabia yetu as a nation ya kuwatunza viongozi wastaafu, ambao aliwakuta pale uawanja wa taifa kwenye lile gwaride muungwan kuchukua power! Na ndivyo taifa la watu wastaarabu linavyopaswa ku-behave, halafu kumbuka kuwa hata Mzee Seif naye huwa anaipata,

Mzee 70M,

Kwa kawaida huwa nipo hapa kukata ishu yoyote ile ambayo ninaielewa, na huwa sijali inamhusu nani, ni muda mrefu sana nimekuwa nikijionea baadhi yetu wakitaka kuwadanganya wengine hapa wasioelewa kinachoendelea katika nchi yetu, hapo ndipo utanipata, sasa wakishindwa hoja as usual hukukimbilia matusi, huwa sina noma na huko pia tunavutana nako, lakini one thing ni kuwa hatutakubali kuruhusu hao watu kushusha hadhi ya hii forum kwa kusema uongo wa makusudi, huuu sio mgahawa au kijiweni, no! hapa ni forum ya kimataifa na inasomwa na dunia nzima, kwa hiyo ni muhimu sana tukasimamia credibility, ndio maana tunao mpaka viongozi muhimu sana wa taifa hapa, sasa tunataka kuwafahamisha wanaotaka mchezo kuwa hapa sio mahali pake,

Nafikiri pia umejonea kuwa kuna wanaotaka kutugeuza wote hapa kuwa waliaji tu wa bila sababu, yaani kila kukicha ni kulia tuuu na kuwalaumu viongozi wa taifa na serikali, ili mradi kulaumu tu kila mtu lakini never hata siku moja kubeba responsibility za matatizo yao, wewe angalia ishu ya Mzee Zeee, sasa anyelaumiwa ni en, na sio Zee wala ac, tena kuna mpaka maneno ya "Free Amina" hapa ndipo ninaposema kuwa Wa-Tanzania, tusipoamuka tuatishia kutawaliwa na ccm for the rest of our life, Mwalimu alimuweka Mwinyi, akamuweka bm, na bm akamuweka muungwana, bila ya kujali matakwa ya wananchi Millioni 35! Wote tukalazimishwa kufuata matakwa ya mtu mmoja, na here we are confused hatujui tunakotoka wala tunakoenda! Muuungwana atakapotoka guess what? naye atamuweka mtu wake, kwa sababu siku zote tunamshangilia Mwalimu as if the man was a semi-God, kwamba hakuwa na makosa kabisaaa ambayo tulihitaji kuyaangalia na kuyarekebisha ili angalau tuuone mwanga mwisho wa tanuru, lakini wapi?

Ukiisoma hii mada kwa makini sana utajionea mwenyewe kuwa sio tu kwamba tuko confused, NO! bali pia ni taifa la wananchi waliokata tamaaa kabisaaa kwamba kuna siku itatokea miujiza vviongozi wa ccm watatoweka, upizani watachukua power, na basi nchi itakuwa safi wananchi wataneemeka na kuwa matajiri au serikali itaondoa matatizo yao mara moja, na wananchi wote tutakuwa sawa!
 
Mzee Es,

Maneno mazito sana... umenifanya nizunguke chumbani kwa muda kutafakari maanake kweli Watanzania sasa hivi tumekwisha kama vile wana wa Esrael walipofika ukingano mwa bahari...Walimtukana Mussa hadi Mungu wake.
 
Bila ya shaka sasa baada ya Uchaguzi wa CCM tunaweza kusema wazi kuwa baadhi ya tuliowadhania kuwa ni vigogo, siyo vigogo tena..!
 
John Malecela - Yes
Rashid Kawawa - Yes
Jackson Makweta - Nope.
Chrisant Mzindakaya - May be.
Joseph Warioba - Not really. Too much of an outsider.
Salim Ahmed Salim - Not really.
Salmin Amour - Amesusa.
Kingunge Ngombare Mwiru - Yes
Cleopa David Msuya - Yes
Dr. Abdalah Kigoda - Nope.
Getrude Mongella - Mmh, may be.
Pius Msekwa - On procedural matters, yes
Joseph Mungai - Nope
Brig. Gen (mstf.) Hassan Ngwilizi - Absolutely not
Anna Makinda - Sometimes
Philip Marmo
- Nope.

A good idea will be to take from the members of Central Committee, then hapo utapata who is who ndani ya CCM.

Zamani kulikuwa na Mzee Masudi Mtandika (Pwani), Daudi Semkiwa (Tanga) na wengineo, it was hot kwenye NEC.

The guy was almost right. Sijui kaishia wapi, nammiso sana huyu ndugu na analysis yake. Huyu angalau alikuwa anaweza kuwatetea CCM kwa hoja, sasa hawa waliobaki humu kutetea CCM ni vioja tu, yaani tunakosa kabisa watu wa kupambana nao kihoja inapokuja katika mapambano ya vyama humu ndani. Eehee bwana Mugongo popote ulipo hebu rudi hapa tuendelee kumkoma nyani gladi, vijana wako uliowaacha hawana kitu kabisa, ni vioja na kubadilisha majina tu basi, hamna kitu kabisa.
 
Mkuu,

Hata mimi nammiss Mugongo Mugongo. Huoni umihimu wa mtu mpaka akiondoka.

FD anasema Mugongo bado yupo ingawaje ni muda sasa mimi sijaona maandishi yake au yhanayofanana na yake.
 
Mkuu,

Hata mimi nammiss Mugongo Mugongo. Huoni umihimu wa mtu mpaka akiondoka.

FD anasema Mugongo bado yupo ingawaje ni muda sasa mimi sijaona maandishi yake au yhanayofanana na yake.

Ni kweli kabisa, hujui thamani ya kitu mpaka kipotee.

Kwa vyovyote mugongomugongo hayupo humu ndani maana style ya maandishi na hoja zako tunazijua, tungeshamgundua. Hayupo!
 
Amekuwa kwenye misafara mingi na bado hajatulia hasa leading up to the election in Dodoma. Nadhani atakuwa ametulia sasa.
 
MIAKA miwili iliyopita, niliandika makala ile ya ‘Kuanguka kwa CCM unabii utatimia”. Katika makala hiyo nilisema ifuatavyo wakati nafungua tu hoja yangu.

“Nilikuwa natafakari maneno ya Mwalimu aliyoyatoa mwanzoni mwa miaka ya 90 mara baada ya vyama vingi kuruhusiwa tena nchini.

Baada ya Mwalimu Nyerere kutoa maneno makali ya Ikulu inanuka rushwa, watu wengi walianza kujiuliza mapenzi ya Mwalimu kwa chama alichokiasisi na kama anaweza kujitoa kwenye chama hicho.

Alipoulizwa kuhusu kujiondoa CCM, Mwalimu alijibu, “CCM si mama yangu.” Maneno hayo ya Mwalimu yamebakia mawazoni mwangu (na bila shaka ya wengine pia) kama unabii na kama wosia.

Hii leo kuna baadhi ya viongozi wa chama tawala ambao wanasisitiza maneno ya Mwalimu ya Bila CCM madhubuti Tanzania Itayumba na kusahau kabisa maneno hayo ya onyo kali kuwa hata kama mtu ana mapenzi kiasi gani na CCM, iko siku anaweza kuiacha na kujitahidi kuivunja! Ni rahisi kuiacha CCM kuliko kumuacha mama mzazi!

Niliongezea haya: “Siku hiyo ambapo chama hiki maarufu kitakapojikuta kiko katika kambi ya upinzani ndipo viongozi wake na mashabiki wake watakapotambua kuwa CCM si mama na Tanzania itaendelea na inaweza kuwepo bila CCM kuwa madarakani! Hiyo siku isiyo na jina, iko, yaja, na yafanya hima kufika!”

Niliposema kuwa hiyo siku “iko, yaja, na yafanya hima kufika” sikutarajia hata chembe kuwa dalili za siku hiyo zitaanza kuonekana mapema hivi. Sasa hivi naweza kuwa shahidi wa dalili za ujio wa siku hiyo kwani tunayoyaona yakitokea CCM bila ya shaka yanatuma ujumbe wa kutetemesha kwa ngozi na mifupa ya wale wanaoamini kuwa CCM ni kama mama yao, na kamwe hawawezi kuiacha, ije mvua au lije jua.

Zamani kulikuwa kweli na Chama Cha Mpinduzi; uongozi wake ulikuwa hauna utata, maamuzi yake yalikuwa yanaeleweka (hata kama hayapendwi), na mwelekeo wake kiitikadi ulikuwa wazi kabisa.

Chama hicho cha zamani hakikuona haya au aibu kusema kuwa ni chama cha kimapinduzi chenye kutaka kujenga taifa la ‘watu walio huru na sawa.’

Ndani yake kulikuwa na nidhamu ambayo ilitokana na kuelewa kuwa uongozi wake hauna utata na kama chama hawakuweza kuona haya kumchukulia hatua mtu yeyote ambaye alikuwa ni tatizo kwa taifa au kwa chama.

Hivyo tangu enzi za TANU maamuzi magumu yalifikiwa na mengine yaliwagusa watu ambao waliaminika kuwa wana nguvu.

Ilipotishiwa uhaini hakukuwa na utata hata marafiki walishukiwa! Tunawakumbuka kina Kambona na Bibi Titi Mohammed.

Tunaweza kubishana milele kama walistahili kuitwa wahaini au kushtakiwa, tunaweza kubishana hadi kucha zivunjike kama walichopanga kilikuwa ni uhaini au watu walitafsiri vibaya tu.

Ukweli mmoja unabakia kuwa ilipolazimika kuchukuliwa hatua hakukuwa na utata kuwa hatua zilichukuliwa, si tu za kisheria (kama inavyosisitizwa leo hii) bali pia za kichama.

Lilipokuja suala la muungano hawakuwa na utata hata Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar na baadaye Waziri Kiongozi wote hawakuonewa haya na kundi kubwa la wanasiasa maarufu ambao leo majina yao yanatajwa kwenye sentensi moja na demokrasia, uzalendo na mageuzi. Hakukuwa na utata.

Palipohitajika maamuzi ya mahakama uongozi wa chama kile haukusita watu walifikishwa mahakamani. Ndiyo maana wengine tunaangalia kesi za EPA na kucheka kuwa hata nusu hawajafikia kilichowahi kufanywa huko nyuma! Mashtaka yaliyowahi kuletwa na uzito wa mashtaka hayo.

Wengine wanataka tuamini kuwa hii ni mara ya kwanza kwa “vigogo” kufikishwa mahakamani, kumbe Tanzania tumeshuhudia si vigogo wa kisiasa tu bali hadi watu wa JWTZ wakisimama kizimbani! Hakukuwa na utata katika uongozi, ndani ya CCM au serikalini.

Yalipohitajika maamuzi ya kisiasa, wala hakukuwa na wasiwasi, wakati ule ukisikia ‘Kamati Kuu’ unatetemeka.

Ukisikia kiongozi wa CCM ameitwa kujieleza mbele ya kamati kuu ya chama unajua kumeiva huko.

Ni nani atasahau yaliyotokea mwaka 1997 kumhusisha Horace Kolimba? Nani atakuwa amesahau ponea chupuchupu ya John Guninita? Au jinsi Komandoo wa Zanzibar alimasura akione cha moto pale alipodaiwa kutaka kubadili katiba ili agombee kipindi cha tatu?

Chama kilikuwa kimoja, migongano yao ilikuwa humo humo ndani, “malumbano yao yalikuwa kwenye vikao vya CCM”. Leo hii hata mzee Malecela ambaye anajua taratibu zilivyo, anabakia kuita waandishi wa habari nyumbani kusema mambo ambayo angeweza kuyasema kwenye kikao cha CCM, lakini anaendeleza malumbano yale yale anayoyapinga! Maskini CCM!

Ati kuna watu wanalaumu magazeti kwa kuandika vibaya na kurushiana madongo wanasiasa. Mimi nimebaki ninacheka.

Hivi madongo wanayorushiana Watanzania wengine na kurasa zilizojaza uchafu wa kila aina na mapicha ya ajabu yenye kuchafua watoto wetu hawa wanasiasa walikuwa wapi?

Ni mara ngapi kuna mwandishi fulani dada kila siku anaandikwa kwa sababu tu anajipaka poda! Ni nani hajui jinsi mtu mzima anajikuta anasingiziwa mambo ya ajabu, tena yenye vichwa vya habari vya ajabu na hakuna mwenye kupiga kelele?

Leo wanasiasa wamegeukiana wenyewe kwa wenyewe, ndiyo, kuna mtu anathubutu kuzungumzia maadili ya vyombo vya habari?

Leo ng’ombe wanapigana pembe kwenye zizi lao ndiyo mifugo yote ilaumiwe! Wamepanda wenyewe na sasa wanavuna, maskini CCM!

Ilipotishiwa uhujumu wa uchumi hakukuwa na utata wa nini kifanyike (japo baadaye baadhi ya kesi ziligeuzwa na mchakato kuboreshwa). Hakukuwa na utata hata hivyo wa nani atachkua hatua!

Enzi hizo chama kweli kilikuwa kimeshika hatamu ya uongozi. Leo hii chama hiki kipya kilichoko madarakani, hakina mwelekeo, hakina itikadi, hakina maono ya mafanikio na kimebakia kama picha ya zamani iliyojawa vumbi la ufisadi.

Kimebakia kuwa chama cha kuangaliana, kukodoleana, kubezena, kutukanana, na sasa imefika mahali kuwa chama cha kusakamana! Ndiyo, kuna mtu anatakiwa aseme ukweli huu.

Nilitarajia mzee wetu Malecela angeita kinachoendelea kwa jina lake lakini hakufanya hivyo; nimesubiri kusikia mzee wetu Kawawa angesema kwa jina lake naye hakufanya hivyo, na wapo wazee wengine wa CCM ambao wana kumbukumbu ya chama kile cha zamani ambao leo wamebakia kunung’unika pembeni na kulalamika chini kwa chini.

Hakina tena hatamu za uongozi isipokuwa utamu; hakina kujitegemea bali kimebaki na kujimegea, hakina ujamaa tena bali kimebakia na utamaa!

Ndiyo CCM hii, si ile ile, zimebakia rangi za kijani, njano na nyeusi! Uongozi wake butu, mwelekeo wake haupo, na malengo yake yamebakia vitabuni!

Ndiyo! Najua ni ukweli mgumu kusikia lakini kama tabibu mahiri ni lazima mgonjwa aambiwe ukweli! Kidonda hiki hakiponi kwa kupeana sifa na kuimbiana nyimbo!

Ndiyo, CCM haina uongozi tena unaoongoza, bali kinaongozwa na viiongozi wanaoongozwa na matukio! CCM hii haijui nchi yetu ni nchi ya mrengo gani na tunataka kujenga taifa la namna gani! Sasa hivi chini ya CCM hii ninachoshuhudia ni mambo kwenda mrama!

Taifa liko mashakani, hatima ya watu wetu matatani na kwa hakika toka mbali kama kwenye ukungu hivi naweza kuona mahali ambapo ule unabii nilioandika habari zake miaka miwili iliyopita unazidi kutimia kwa haraka zaidi.

Na wanaoutimiza ni wana CCM wenyewe! Ukweli ni kuwa unabii utatimia bila kujali kama wanajua upo au haupo!

Ninaiangalia CCM hii na kujiuliza, ni kitu gani kimeenda kombo? Ni wapi wameacha njia, ni wapi walipopotea tuwarudishe? Najiuliza kama kuna faida yoyote ya kuwarudisha au kuwaacha wapotee tu kwani hiyo ndiyo njia ya vyama vyote vilivyokaa madarakani muda mrefu.

Mwalimu aliliona hilo na alisema hilo. Kwa taarifa, CCM kukaa madarakani muda mrefu kumeiharibu!

Nani ataiokoa? Ni nani atasimama na kusema “sasa yatosha”? Yuko wapi mtu shujaa ambaye hataona haya ya kuwaita mafisadi walio ndani ya chama ‘wameguke’ badala ya kuwaita watu hewa ‘wameguke.’

Ni nani atasimama na kusema kuwa Tanzania kwanza na chama baadaye! Ni nani atasema kama Mwalimu bila kujiuma kuwa “CCM si mama yangu!”

Ndiyo! Najua wapo wana CCM ambao wanaamini kabisa katika mioyo yao kuwa Tanzania bila CCM haiendi. Wapo wanaoamini kabisa kuwa mafanikio yao yote ya kibiashara na kisiasa yamefungamana kama chanda na pete na utawala wa CCM.

Ndiyo! Wapo ambao wanajua kabisa kuwa siku CCM ikitoka madarakani na wao ndiyo utakuwa mwisho wao.

Hawa ndio ambao kwao CCM ndiyo mama, kwa hawa CCM haiwezi kufanya makosa; kwa hawa CCM haina ufisadi wowote “isipokuwa mtu mmoja mmoja”.

Kwa hawa “CCM yetu ni safi ila mtu mmoja mmoja”. Ndiyo, hawa wanaitukuza CCM kwa kufuata ibara ya 15:1 ya Katiba yao.

Kwao Tanzania inakuja baada ya CCM. Kama huamini kahesabu katika mazungumzo ya mzee Malecela ni mara ngapi anataja CCM, Chama Cha Mapinduzi, taifa na Tanzania; utashangaa!

Ndiyo! Wapo mashujaa CCM. Ninafahamu wapo watu wazuri CCM na wengine ni marafiki kweli. Lakini ukweli utabakia kuwa mapambano haya kwao yatakuwa ni magumu mno kwani mafisadi wamejipanga vizuri; silaha zao kali, majeshi yao yana uzoefu.

Mafisadi hawa hawakomi kwa kuzomewa au kuandikwa magazetini. Mafisadi hawa hawaachi kwa sababu wanaandikwa na kujadiliwa kwenye JamiiForums au Mwanakijiji.com! Hapana.

Kukoma kwa mafisadi hawa ni pale tu ambapo CCM itatolewa madarakani au kupoteza kwa kiasi kikubwa nguvu yake bungeni. Mpaka pale wananchi wa Tanzania watakapotambua kuwa Tanzania yenye mafanikio bila CCM madarakani inawezekana.

Hata hivyo najua swali linalokuja: “Sasa huko upinzani kuna uongozi gani wa kufuata?” Jibu lake nalijua. Nasema msiuangalie upinzani, iangalieni CCM kwani kuanguka kwa CCM hii ya sasa kutasababisha kuzaliwa kwa vuguvugu jipya la mwamko wa mageuzi ya kweli nchini.

Siku hiyo haiko mbali, iko karibu, na nimeiona ishara! Ningekuwa mimi wewe nisingeweka matumaini yangu yote ndani ya CCM, kwani CCM si mama yangu! Wale ambao wanaamini kuwa wana udugu wa damu na CCM hawa tuwaangalie tu, kwani siku hiyo kwao itakuwa ni ya kilio na kusaga meno watakapotambua kuwa yule mama waliyemdhania ni mama yao, kumbe ni yule bibi mbwa mwitu wa kwenye hadithi za utotoni, kavaa miwani, kajilaza kitandani, anasubiri walete chakula! Watakapofikiri wako salama ndipo watajua.

CCM ina kazi mbele yake ya kujumlisha tuliyojifunza tangu tupate uhuru na hasa baada ya Azimio la Arusha juu ya hatari zinazoweza kutokea kwa siasa ya chama na kwa taifa wakati, madaraka muhimu ya chama, serikali au mashirika ya umma wanakabidhiwa watu ambao kisiasa ni chui katika ngozi ya kondoo. (Mwongozo wa CCM, 1981).

Aidha, inapotokea kwamba taifa linakabiliwa na jambo kubwa linalokera, linaloweza kuhatarisha umoja na mshikamano wa nchi kama ufisadi, wananchi hutegemea mtu au taasisi ijitokeze kulipatia jambo hilo tata ufumbuzi kwa masilahi ya taifa zima.

Katika kipindi hiki kijacho, CCM iendelee kutegemewa na Watanzania kuchukua nafasi hiyo ya uongozi kwa taifa zima. (Mwelekeo wa Sera, 2000). Leo hii CCM imebakia pembeni bila kutoa kauli yoyote ya kulaani vitendo vya kifisadi, kujichunguza yenyewe na kuwakana wana CCM wanaotajwa kuhusika na ufisadi na ambao wao wenyewe wanawafahamu.

Leo hii, wanaokerwa na kupiga kelele dhidi ya ufisadi ni wapinzani na kikundi cha wana CCM wachache ambao sauti zao zinakuwa kama za Yohana Mbatizaji jangwani.

Nani anaiongoza CCM sasa?

CCM pole pole inaanza kusimamishwa kizimbani! Kizimba cha maoni na fikra za watu! Je itakutwa na hatia? Na ni nani anaiongoza! Je Kikwete ameishindwa?

Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?
 
MKJJ, uchambuzi wako makini nakupa BIG UP kwa sana!!! Naunga mkono kuwa ipo haja ya haraka kwa MWENYEKITI wa CCM Mh Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA. Je ajenda itatayarishwa na nani? Maudhui yake yawe nini? Hapo ni gumzo!!!
 
mkjj, uchambuzi wako makini nakupa big up kwa sana!!! Naunga mkono kuwa ipo haja ya haraka kwa mwenyekiti wa ccm mh kikwete kuitisha mkutano maalum wa halmashauri kuu ya taifa. Je ajenda itatayarishwa na nani? Maudhui yake yawe nini? Hapo ni gumzo!!!

agenda yaweza kuwa kama ifuatavyo:

A. Kubadilisha katiba hasa kufuta ibara ya 15:1

b. Kubadilisha itikadi ya chama toka ujamaa kwenda ubepari

c. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanachama wake wote wanaohusika na wizi wa fedha za umma na ambao kutokana na matendo yao wanaonekana kuhujumu taifa

d. Kuwatimua kwenye chama wale wote wanaohusika na uhujumu uchumi, wanaokabiliwa na tuhuma nzito

e. Kubadilisha utaratibu wa kumpata mgombea wa ccm wa kiti cha urais. Kuwe na mchujo wa kuacha majina mawili na mgombea atapatikana kwa kushinda kura za maoni katika mikoa. Anayepata mikoa mingi (siyo idadi ya watu) ndiye anakuwa mgombea rasmi.

F. Kuweka utaratibu wa kuwa na serikali ya mseto.

N.k
 
c. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanachama wake wote wanaohusika na wizi wa fedha za umma na ambao kutokana na matendo yao wanaonekana kuhujumu taifa

Duh! Nani katika top brass atasalimika?

d. Kuwatimua kwenye chama wale wote wanaohusika na uhujumu uchumi, wanaokabiliwa na tuhuma nzito

Heheheee...itabidi baadhi ya watu wajitimue wenyewe

e. Kubadilisha utaratibu wa kumpata mgombea wa ccm wa kiti cha urais. Kuwe na mchujo wa kuacha majina mawili na mgombea atapatikana kwa kushinda kura za maoni katika mikoa. Anayepata mikoa mingi (siyo idadi ya watu) ndiye anakuwa mgombea rasmi.

Kwa nini iwe kura za maoni? Kwa nini zisiwe kura za kweli baada ya wagombea kujinadi na kunadi sera na mipango yao kwa taifa?

F. Kuweka utaratibu wa kuwa na serikali ya mseto. N.k

Uamuzi kama huu ni bora ufikiwe na bunge la jamhuri kuliko chama kimoja cha kisiasa. Ni utaratibu ambao unatakiwa uwe spelled out kwenye katiba ili chama au yeyote yule atakayekuwa madarakani ajue wazi ni lini na wapi pa kuunda serikali ya mseto.
 
Kwa nini iwe kura za maoni? Kwa nini zisiwe kura za kweli baada ya wagombea kujinadi na kunadi sera na mipango yao kwa taifa?

Kura za maoni (primaries) zinawahusisha wana CCM tu. Wakishampata mgombea wao ndiyo wanamsimamisha dhidi ya wagombea wa vyama vingine. Utaratibu huu ni mzuri hata kwa vyema vingine. Lengo ni kuondoa utaratibu wa kikomunisti wa KAMATI KUU kumteua Mgombea wa Chama.

Uamuzi kama huu ni bora ufikiwe na bunge la jamhuri kuliko chama kimoja cha kisiasa. Ni utaratibu ambao unatakiwa uwe spelled out kwenye katiba ili chama yeyote yule atakayekuwa madarakani ajue wazi ni lini na wapi pa kuunda serikali ya mseto.

Ni kweli lakini CCM ndiyo chama chenye wabunge wengi na kwa muda mrefu kitabakia hivyo. HIvyo, wao wakitaka jambo litafanyika.
 
CCM haina wabunge wengi ila ina wezi wengi ,ndio maana yake.
 
Kwanza tukubalianae kanuni za vyama vya siasa kupata fedha za kujiendesha.

Pili; malengo ya chama cha siasa ni kushinda uchaguzi na kuunda dola. Kwa mfumo walionao CCM sasa hivi wanafanikiwa malengo hayo, na ndio sababu hawana haraka kufanya mabadiliko kama hayo unayomendekeza.

Wananchi wakiwa tayari, CCM itakuwa tayari watafanya mabadiliko sambasamba na alama za nyakati.
 
Zamani kulikuwa na chama cha mapinduzi; uongozi wake ulikuwa hauna utata, maamuzi yake yalikuwa yanaeleweka (hata kama hayapendwi), na mwelekeo wake kiitikadi ulikuwa wazi kabisa. Chama hicho cha zamani hakikuona haya au aibu kusema kuwa ni chama cha kimapinduzi chenye kutaka kujenga taifa la "watu walio huru na sawa".

Ndani yake kulikuwa na nidhamu ambayo ilitokana na kuelewa kuwa uongozi wake hauna utata na kama chama hawakuweza kuona haya kumchukulia mtu yeyote ambaye alikuwa ni tatizo kwa Taifa au kwa chama. Hivyo tangu enzi za TANU maamuzi magumu yalifikiwa na mengine yaliwagusa watu ambao waliaminika kuwa wana nguvu.

Ilipotishiwa uhaini hakukuwa na utata hata marafiki walishukiwa!

Ilipotishiwa Muungano hawakuwa na utata hata Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar na baadaye Waziri Kiongozi wote hawakuonewa haya.

Ilipotishiwa uhujumu wa uchumi hakukuwa na utata wa nini kifanyike (japo baadaye baadhi ya kesi ziligeuzwa na mchakato kuboreshwa). Hakukuwa na utata hata hivyo wa nani atachkua hatua!

Chama kweli kilikuwa kimeshika hatamu ya uongozi. Leo hii chama hiki kipya kilichoko madarakani, hakina mwelekeo, hakina itikadi, hakina maono ya mafanikio na kimebakia kama picha ya zamani iliyojawa na vumbi la ufisadi. Kimebakia kuwa chama cha kuangaliana, kukodoleana, kubezena, kutukanana, na sasa imefika mahali kuwa chama cha kusakamana!

Hakina tena hatamu za uongozi isipokuwa utamu; hakina kujitegemea bali kimebaki na kujimegea, hakina ujamaa tena bali kimebakia na utamaa! Ndiyo CCM hii siyo ile ile, zimebakia rangi za kijani, njano na nyeusi! Uongozi wake butu, mwelekeo wake hupo, na malengo yake yamebakia vitabuni!

Ndiyo, CCM haina uongozi tena unaoongoza, bali kinaongozwa na viiongozi wanaoongozwa na matukio! CCM hii haijui nchi yetu ni nchi ya mrengo gani na tunataka kujenga taifa la namna gani! SAsa hivi chini ya CCM hii ninachoshuhudia ni mambo kwenda mrama!

Taifa liko mashakani, hatima ya watu wetu matatani, na kwa hakika toka mbali kama kwenye ukungu hivi naweza kuona mahali ambapo ule unabii niliondika habari zake miaka mitatu uliyopita unazidi kutimia kwa haraka zaidi. Na wanaoutimiza ni wana CCM wenyewe!

CCM pole pole inaanza kusimamishwa kizimbani! Kizimba cha maoni na fikra za watu! Je itakutwa na hatia? Na ni nani anaiongoza! Je Kikwete ameishindwa?

Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?

Ahsante sana kwa mchango wako mzuri sana na umeuleta wakati muafaka. Kwa maoni yangu CCM haina kiongozi ndiyo maana mambo ndani ya chama hicho yako hovyo hovyo tu kama tunavyaona na kuyasikia. Kiongozi hawezi kuendelea kukaa kimya wakati anaona chama anachokiongoa kinaenda mrama kila siku iendayo kwa Mungu. Atafanaya kila awezalo ili kuhakikisha chombo hicho kinakaa sawa na kuendelea na safari yake bila purukushani yoyote. Lakini kukosekana na kiongozi aliye jasiri kuhakikisha chombo chake hakiendi mrama ndiyo matatizo yote ndani ya CCM na hali kadhalika ndani ya nchi yetu.
 
agenda yaweza kuwa kama ifuatavyo:

A. Kubadilisha katiba hasa kufuta ibara ya 15:1

b. Kubadilisha itikadi ya chama toka ujamaa kwenda ubepari

c. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanachama wake wote wanaohusika na wizi wa fedha za umma na ambao kutokana na matendo yao wanaonekana kuhujumu taifa

d. Kuwatimua kwenye chama wale wote wanaohusika na uhujumu uchumi, wanaokabiliwa na tuhuma nzito

e. Kubadilisha utaratibu wa kumpata mgombea wa ccm wa kiti cha urais. Kuwe na mchujo wa kuacha majina mawili na mgombea atapatikana kwa kushinda kura za maoni katika mikoa. Anayepata mikoa mingi (siyo idadi ya watu) ndiye anakuwa mgombea rasmi.

F. Kuweka utaratibu wa kuwa na serikali ya mseto.

N.k

Kama ni Kikwete huyu huyu tunaomjua wote, hana uthubutu wa kufanyia kazi wala kuzungumzia agenga yoyote kati ya hizo ulizoorodhesha. Wala hiyo analysis uliyofanya haielewi wala hakubaliani nayo. Mtu wa kuanzisha hiyo debate lazima awe mwinginewe.
 
Labda Mzee Mwanakijiji ni vema pia ukajiuliza,"Tanzania inaongozwa na nani?"Maana jibu lake ni moja!

Zamani kulikuwa na chama cha mapinduzi; uongozi wake ulikuwa hauna utata, maamuzi yake yalikuwa yanaeleweka (hata kama hayapendwi), na mwelekeo wake kiitikadi ulikuwa wazi kabisa. Chama hicho cha zamani hakikuona haya au aibu kusema kuwa ni chama cha kimapinduzi chenye kutaka kujenga taifa la "watu walio huru na sawa".

Ndani yake kulikuwa na nidhamu ambayo ilitokana na kuelewa kuwa uongozi wake hauna utata na kama chama hawakuweza kuona haya kumchukulia mtu yeyote ambaye alikuwa ni tatizo kwa Taifa au kwa chama. Hivyo tangu enzi za TANU maamuzi magumu yalifikiwa na mengine yaliwagusa watu ambao waliaminika kuwa wana nguvu.

Ilipotishiwa uhaini hakukuwa na utata hata marafiki walishukiwa!

Ilipotishiwa Muungano hawakuwa na utata hata Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar na baadaye Waziri Kiongozi wote hawakuonewa haya.

Ilipotishiwa uhujumu wa uchumi hakukuwa na utata wa nini kifanyike (japo baadaye baadhi ya kesi ziligeuzwa na mchakato kuboreshwa). Hakukuwa na utata hata hivyo wa nani atachkua hatua!

Chama kweli kilikuwa kimeshika hatamu ya uongozi. Leo hii chama hiki kipya kilichoko madarakani, hakina mwelekeo, hakina itikadi, hakina maono ya mafanikio na kimebakia kama picha ya zamani iliyojawa na vumbi la ufisadi. Kimebakia kuwa chama cha kuangaliana, kukodoleana, kubezena, kutukanana, na sasa imefika mahali kuwa chama cha kusakamana!

Hakina tena hatamu za uongozi isipokuwa utamu; hakina kujitegemea bali kimebaki na kujimegea, hakina ujamaa tena bali kimebakia na utamaa! Ndiyo CCM hii siyo ile ile, zimebakia rangi za kijani, njano na nyeusi! Uongozi wake butu, mwelekeo wake hupo, na malengo yake yamebakia vitabuni!

Ndiyo, CCM haina uongozi tena unaoongoza, bali kinaongozwa na viiongozi wanaoongozwa na matukio! CCM hii haijui nchi yetu ni nchi ya mrengo gani na tunataka kujenga taifa la namna gani! SAsa hivi chini ya CCM hii ninachoshuhudia ni mambo kwenda mrama!

Taifa liko mashakani, hatima ya watu wetu matatani, na kwa hakika toka mbali kama kwenye ukungu hivi naweza kuona mahali ambapo ule unabii niliondika habari zake miaka mitatu uliyopita unazidi kutimia kwa haraka zaidi. Na wanaoutimiza ni wana CCM wenyewe!

CCM pole pole inaanza kusimamishwa kizimbani! Kizimba cha maoni na fikra za watu! Je itakutwa na hatia? Na ni nani anaiongoza! Je Kikwete ameishindwa?

Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?
 
sasa hivi nimeanza kuwacancel watu ambao nilidhani wanaweza wakasema kitu kikaeleweka. Nadhani ni bora wakae kimya tu maana wakifungua makanwa yao wakati mwingine najiuliza "how on earth did we ever get such leaders". Wakati mwingine naanza kuamini kuwa labda Nyerere kwa kweli alikuwa amezungukwa na "siongozi" wengi!
 
Back
Top Bottom