Nani anaiongoza CCM?

Mzee ES nakupa tano kwa data!! ila ni kweli membe kupelekwa foreign kumeleta msuguano ndani ya CCM?(Nje ya topic kidogo)
 
Mzee Kada,

Wewe weka ya kwako na wengine wataweka yao, wanachi wataamua nani ana pumba na nani ana mchele,

(1). BM alikwenda Dodoma, akiwa hana uhakika nani wa kumchagua, lakini alishaaamua kuwa jm hapiti, sababu, ni kwamba mwaka 2000 wakati wa uchaguzi wa ndani wa ccm viongozi wengi wakiongozwa na Ndejembi walimfuata BM Chamwino saa za usiku, na kumtaka asimchague tena jm kuwa Veep, kwa sababu atachukua fomu ya urais mwaka 2005, kinyume na matakwa ya baba wa taifa, na akichukua bm hataweza kumsimamisha, some of them kama Anna Abdallah were crying machozi kabisaa kumbembeleza bm amuondoe jm,

(2). bm akawajibu kuwa amewasikia, lakini anamuhitaji bado, lakini akawaahidi kuwa in case jm atachukua fomu ya urais yeye atakufa naye tena over his dead body, compromise ikawa jm aitwe kwenye kikao cha kamati kuu aseme ukweli kuhusu urais wa 2005, mzee alipokuja akasema kuwa hatachukua fomu na hana nia kabisaaa, tatizo la mtandao likawa ni sas, kwa hiyo wakamkaba koo bm amtwange sas, maana alishawaambia kuwa hakuna tatizo na jm.

Siku ya mkutano ilipofika wa kamati kuu na uchaguzi, bm aliwaambia wajumbe wapitie majina yote wamuachie la jm na bilali, they did akamuita jm na kumuambia hukubaliki wewe toa jina now! baadaye akamuita Bialli na kumuambia toa jina lako now, sitaki ubishi wala kusikia kitu! that was the end of the story!

(3). Baada ya Muuungwana kupita, aliwakimbia watu wote kwa siri na kwenda kilimani kwa jm, na kufanya makubaliano naye for two hours wawili tu! baada ya pale jm akaanza kumsaidia muugwana na kampeni, wakati mmoja jm alikuwa songea vijijini akisaidia kampeni ya muugwana, again muungwana akawakimbia watu wake wote na kumfuata jm kwenye guest house, wakakaa kwa masaa matatu!

(4). Baada ya uchaguzi, baraza la mawaziri kubwa mno, muungwana na el wakamfuata jm usiku, kumuomba opinion, akwaambia do not listen fanyeni kazi vijana, ikiwa nzuri wananchi watasahau kuwa kuna baraza kubwa, but, kuanzia sasa nikiwa na shida nitawatafuta mwenyewe, sitawasubiri mnitafute!

(5). Mtandao wakaanza vijembe na bm, bm akaaanza kulia lia kwa jm kuwa mtandao wanamuonea, jm akawafuata el na muungwana na kuwakaripia kuwa waache mara moja, jm akajaribu kmuomba bm asijiuzulu ccm, lakini akagoma kuwa ni aibu kakwe kukaa chini kumsubiri muungwana kwenye vikao vya ccm, ambaye huchelewa makusudi kila kikao, since then bm hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha ccm, jm akawafuata muungwana na el, na kuwakaripia kuwa waawambie watu wao waache kumlima bm, enough! wakaacha.

(6). Chuo kikuuu kipya cha Dodoma, Muuungwana alimfuata jm na kumuomba aamue kijengewe wapi, ni jm ndiye aliyeamua kijengwe hapo kinapojengwa sasa, na pia kusiamamia pesa zake zote, na hapo hapo akampa sillingi millioni 20 za kuanzia!

(7). Viongozi wa ZNZB, wakaanza kampeni za urais, again jm akamfuata muungwana na kumpa clear kuwa the best mgombea huko ni bilali, muungwana kwenye kamati kuu, akatukana viongozi wengine wote kina shamuhuna na nahodha kuwa waache kampeni na kumtishia shamuhuna kuwa atamnyang'anya vingora kama ndio inampa jeuri!

(8). Walipochaguliwa kina makamba, jm akamwambia muungwana kuwa ninataka kutoka sasa, mungwana no wait nipe more time!

I can go on and on bro, maamuzi ya ccm hufanywa na muungwana na jm tu! maamuzi ya serikali hufanywa na muungwna peke yake!
 
Mzee Es, hayo uliyoyasema kama yana ukweli basi nafikiri umepunguza vigogo toka wanne... hadi mmoja! JM akiikemea CCM hadharani atasikilizwa?
 
Mzee ES

Much respect....duh, naona kama 2010 haifiki.

MKJJ

Kwa jinsi alivyo na access ya Muungwana na EL sidhani kama ana haja ya kuwafokea hadharani...hata hivyo JM hana hulka hiyo au niseme jeuri hiyo.

Mzee ES

Kwa maelezo yako inaonyesha JM ana "influence" kubwa sana...sasa hebu nijulishe kwa nini yeye awe na sauti nene hivyo na sio vikongwe wa chama wakina Kingunge, Mzee Kawawa n.k?

Je...ni hela, anaukaribu na jeshi, wana usalama au...ni nini hasa. Tunajua kwa nini JKN alikuwa na sauti...lakini JM zaidi ya kuwahi kuwa PM na sasa N.ccm Bara...naomba siri yake tafadhali.
 
jeshi, idara, salimin, hawezi kusema anything kwenye public kutokana na makubaliano na muungwana, the matter of fact hukwepa sana sehemu yoyote alipo muungwana, maana mzee anamjua muungwana kuliko watu wote wa bongo, kila anapomuita kwenye public jm hukataaa!

akiwa pm mzee alifanya kampeni kali sana ambayo mpaka leo mizizi bado kukatika, halafu kuna wazeee mandela na obasanjo washikaji wake wa karibu, ambao siku zote humpigia simu muuungwana kumuulizia kwa makusudi kuwaa mzee jm anaendeleaje,

halafu the best of all alivunja azimio la arusha, viongozi leo wakawa matajiri, nguvu za kina kingunge ni kwenye ishu kama hizi za ac, kwa mfano mahita alipoitwa na kamati kuu wakati ule hataki kutoka, kingunge aliongea sana kumponda mahita na kumtaka muungwana aende public kuomba radhi wananchi kwa vitendo vya mahita, alipomaliza muungwana alimuambia

"......kaa chini umeongea vya kutosha nimekutana na mahita kwa masaaa mawili amenieleza ukweli wake na nimemsikia, nani kati yetu hapa hajawahi kuteleza...., na ninasema mimi na jm tumeamua kuwa tutampa nafasi amalize vizuri na aondoke anapotaka na atapewa heshima zote za kiserikali......"

kawawa na kingunge hutumika tu kama rubber stamp, na hasa kingunge hutumika zaidi bungeni kuwatishia wabunge wa ccm kupitisha ishu za ccm, msuya nguvu yake ilimalizwa na kisumo, ndejembi anadaiwa na ra hela alizompa za uchaguzi wake uliopita wa mwenyekiti wa ccm wa mkoa, kwa hiyo hana nguvu tena, warioba yupo tu lakini hahusishwi kabisaaa na anything wao humuita msema hovyo, almeir hana ubavu mbele ya salimin ila hutumika kwenye kuwatishia wabunge wa ccm visiwani, mwinyi hana sauti kabisaaa ila hutumika sana kuwaweka sawa wa-Islam na pia mzee kk, bm ana kasifa kwenye wafadhili kwa hiyo hutumika sasa kama njia ya kuwafikia wafadhili wasiofikika!
 
sawa nimekukubali mzee es, lakini angalau na kuandika mineno kibaooooooo ukidhani kuwa yote ni FACTS basi naomba uache kujiongopea, mie naweka brifu tu hapa, hayo unayasema wewe lakini jua kwamba malecela has no say ndani ya chama na hakubaliki tena which means he is good to go simply bikozi ccm haimhitaji !! ( muda wake umekwisha ) !! JK kushauriwa na malecela sasa hivi hizo ni propaganad tu za kumfanya malecela yupo hai kisiasa wakati alishauzimwa tokea zamani. Mbona kuna maneno meeeeengi kuhusu malecela mara kafanya hivi mara vile, mbona hayawekwei hadharani kama ya jk, na lowassa ? au una maana hapati proper credit au blame juu yake ??

by the way, i bring the point straight to ur face, na siandiki magazeti hapa !!
ooh, yeah keep in mind again malecela has no say in the chama au in the nchi !!
 
duh ! halafu umesema walifanya makubaliano yao ( yaani bm na jm ) wawili tu !!!! sasa wewe hizo info umezipata wapi ? una maana malecela ni ropoka ropoka au ? haya endelea kutupa tabia za huyo mzee wako !! tunasikiliza
 
kwenye safari ya kwenda tunduru, jm alikataa kwenda na mama zakia,akasema over his dead body, na mama akatemwa!

nilijua tu kuwa utaishia hapo ulipo na hoja za mzee wako, otherwise huna kitu wewe labda unaujua upinzani lakini chama changu ninakijua ndani nje, halafu i like the fact kuwa inabidi utumie hili jina kwa unayoyasema sasa, halafu unabadili tena unaposema mengine, mwendo mdundo bro either unazo data au huna alisema hakusema sio ishu, umesema unazo data zimwage hapa wacha filimbi!

unajua I can see clear sasa kwa nini mwalimu alikuwa akilalamika kuwa akienda likizo Butiama, alikuwa hawezi kupumzika kwa amani maana ni kesi kibao za jamaa kupiga wake zao!
 
kijana kama unazo data ziweke hapa acha hadithi, mimi niliahidi kuweka data ndio hizo ninazimwaga, utachambua mwenyewe. kama unazo weka data hapa!
 
Mzee ES,
You have finally solved the puzzle that has troubled me for so long.Kumbe Mzee JM ndiye aliyevunja Azimio la Arusha na kutuletea uoza huu tunaoshuhudia leo katika serikali yetu ya viongozi kujitajirisha kwa kuuza haki za Watanzania? No wonder Mwalimu aliandika kile kitabu. Now I understand. Duu! Tanzania, Mungu aibariki.
 
Duuuuuhhhhhhhhhhhhh,

Hii kali! Hivi haya mambo yalikuwa yakifanyika for public consumption ama? Na bado tunadhani "reduplication of elite" sio tatizo katika nchi yetu. Anyway ndio demokrasia hiyo kila mtu ana mchango wa aina yake katika jamii na Mzee Es anatekeleza majukumu ya nafasi yake.

Mungu inusuru Tanzania yetu
 
Es,

Yuo have been long enough in these forums to understand people. Sometimes U dont even need to reply.
 
Mzee Jasusi,

Heshima mbele mkuu, pamoja na kitabu bado bongo tunahangaika je Mwalimu angekuwepo leo angeandika vitabu vingapi?

maana ingebidi aandike kuhusu bm na ubinfsishaji, richmond, iptl, radar, angeandika vingapi?

kwenye viongozi kuwa na njia za halali kujitajirisha sina noma isipokuwa tu kama njia hizo ni za wizi kama za Mahalu, then ni tatizo, lakini si kweli kwamba viongozi wote wanapata hela kwa wizi wa hela za serikali hapana! na mambo ya siasa ya ujamaa yaliisha pale tu Mwalimu aliponga'tuka.

Alipoandika kile kitabu alituambia kuwa BM ndiye anyefaaa na malaika, na kweli tumejionea ndugu yangu!

Mzee FD,

Heshima mbele mkuuu, haogopwi mtu hapa na wala hatishwi mtu hapa, wote ni watu wazima hapa hakuna mtoto wala mjinga anyway they come tutajibu mapigo wala usiwe na wasi!
 
Es,

Yuo have been long enough in these forums to understand people. Sometimes U dont even need to reply.

And,you have been long enough in these forums to understand people.Sometimes U dont even need to ADVISE some people

.....Nakutania tu Mzee FD!Naafikiana nawe kwa asilimia 100.Wahenga husema mtu sober akibishana na mlevi inaweza kuleta tafsiri kuwa wote ni walevi,japo haimaanishi kuwaacha walevi wafanye watakayo lest one ends up looked at as a mlevi too simply bcoz they argued with them (walevi).

PEOPLE VARY BECAUSE WE DIFFER!
 
Mzee ES,
Nilishawahi kusema kuwa BM is Iskariot. Tanzania hakuna kiongozi aliyetajirika kihalali. Akina EL, akina Karamagi, na sasa akina Diallo wote wametajirika kwa kuhujumu nchi. Na ndiyo maana watu wanakimbilia ubunge wa CCM (Masha) hata kama mtazamo wao haujawahi kuwa wa Ki-CCM ili nao wapate nafasi ya kujitanua.
 
Vigogo ni hawa hapa:
1.Rashidi Kawawa.
2.Ally Hassan Mwinyi.
3.Salmin Amour.
4.Kingunge Ngombale Mwiru.

Joseph Warioba naamini ameburuzwa tu kushiriki masuala ya CCM kwasababu amepata kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu. Huyu Mzee siyo mwanasiasa hata kidogo. Yeye anapendelea mambo ya sheria-sheria tu.

Wakati Mwalimu ni mwenyekiti wa CCM kulikuwa na kura za wajumbe wa halmashauri kuu wakiziita "kura za kikapu." Mtindo huo ulitumika kuwapa nafasi za ujumbe wa halmashauri kuu wanachama ambao walikuwa hawawezi kupitishwa kwa kura za kawaida. Cleopa Msuya aliwahi kutumbukia ktk hilo kundi la "kura za kikapu." Kwa msingi huo huyu hajawahi kuwa "kigogo" wa CCM.
 
Joka Kuu, swali langu haswa kwenye hii mada ni kujaribu kufikiri kama hao watu wanne uliowataja wakisimama hadharani na kusema "CCM hapa imekosea" na "kuikemea hadharani" kama alivyofanya Mwalimu wanaweza kusikilizwa na wananchi? Je wakifanya hivyo wanaweza kubadilisha mwelekeo mzima wa CCM?
 
Back
Top Bottom