Nani amesema Mzee Dosa Aziz Ali alifirisika kwa kupigania uhuru?

Ni kweli kabisa mzee huyu ni mmoja wa mashujaa wetu ingawa kuna watu wanaongeza mawazo yao binafsi kwenye historia iliyotukuka ya mzee wetu (Mola amrehemu) katika kupigania uhuru wa nchi hii
 
Kuna kitu nimeanza kukifanyia kazi..I,e mali hata uwe nazo nyingi kiasi gani hazikufanyi uishi(jina lako liendelee kuishi japo umeshakufa)...ila hekima,upendo na ukweli ndio legacy ya kweli na ya kudumu.
Natangaza upendo wa kweli na haki kwa kila mtu kuanzia leo...ili tu nije niishi japo nimekufa...God bless me.
 
Namkumbuka mzee mmoja humu wa kuitwa mohamed SAID akiandika alichokiita historia ya wazee wake wa sijui Gerezani au Kariakoo ndiye aliyekuwa analalamika sana kuhusu Dossa Aziz kufilisika na kufa maskini akiishia kuzikwa kwao Bagamoyo bila aliowafadhili kuhudhuria.soon atakuja kukuparura ktk post yako hii maana waonyesha upo against nae....utaniambia!
 
yule mzee wa kizanaki ana fitna sana

vitabu vya historia haviwataji taji wenzake,ni yeye tu

Tena alipenda sana aitwe Mwalimu lakin sasa hao Wanafunzi wake Hahahaha hata Shetan anasubiri kila dili wamo hata ndege ya kuchukua Mwili wa Mwalimu kutoka St Thomas watu walichimba Mtaro wa kutiririsha fedha za Umma!
 
Ujue tu inatosha hakuna deni
kabla hajifilisika alikuwa na mali kiasi gani?alifilisika kwa kununua nini?alikuwa na biashara gani?alikuwa na watoto wangapi?..mambo mengine labda ni ya kifamilia mnalaumu wengine.
 
Mzee Dosa Aziz ni miongoni mwa mashujaa walio tukuka katika historia ya nchi hii.

Lakini maskini hakuwahi kupewa heshima stahiki.
".....Tenda yalo na thawabu pasi na watu kujua..."
Ipo siku ukweli utadhihiri.
 
Back
Top Bottom