Nani aliwahi kupatwa na haya mambo utotoni?

raslimali

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,344
1,013
Habari wakuu,

Nilipokuwa mdogo kuna jambo lilikuwa linanitokea mimi pamoja na wadogo zangu na hata watoto wa majirani au ndugu wa karibu. Mara kwa mara unalala usiku ukiamka asubuhi unajikuta kuna alama kama umechomwa na moto (kovu jeusi) lakini husikii maumivu pale ulipochomwa.

Wazee wetu walikuwa wakituambia kwamba tumechomwa na mizimu usiku. Imenitokea mara nyingi sana utotoni nikiwa shule ya msingi. Kuna yeyote humu jamvini alishawahi kupatwa na jambo kama hili na labda kuna maelezo mengine ya kinachosababisha jambo hili?
 
Hiyo ya makovu haijawahi kunitokea,ila ile ya kukuta umenyolewa kichwani nywele na wameondoka Nazo ilikuwa kawaida,
 
Habari wakuu,

Nilipokuwa mdogo kuna jambo lilikuwa linanitokea mimi pamoja na wadogo zangu na hata watoto wa majirani au ndugu wa karibu. Mara kwa mara unalala usiku ukiamka asubuhi unajikuta kuna alama kama umechomwa na moto (kovu jeusi) lakini husikii maumivu pale ulipochomwa.

Wazee wetu walikuwa wakituambia kwamba tumechomwa na mizimu usiku. Imenitokea mara nyingi sana utotoni nikiwa shule ya msingi. Kuna yeyote humu jamvini alishawahi kupatwa na jambo kama hili na labda kuna maelezo mengine ya kinachosababisha jambo hili?
Usiku kuna mambo mengi ole wako kama husali kwa Mungu wa Kweli, utapigwa mihuri ya kichawi kwa ajili ya shughuli zao. Sikuwahi kuona hilo kwangu maisha yetu yote kwani ilikuwa ni lazima familia yote kusali kila siku. Ila kwa baadhi ya majirani nilisikia wakilalamika kuchanjwa na kukabwa usiku na majinamizi na hawa walikuwa hawasali. Hakikisha Yesu yupo pamoja nawe nje ya hapo unaibiwa maisha yako bila kujua.
 
Tulikuwa tunasali kila jioni. Nimelelewa kwenye familia ya kikatoliki.
 
Back
Top Bottom