Nanasi Linapandwa/oteshwaje?

Utamaduni

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
1,279
597
Wakuu heshima yenu.

Naombeni msaada kwa wale wenye kujua tunda hili la nanasi linapandwa au kuoteshwa vipi? maana embe inapandwa mbegu yake (kokwa), chungwa unapanda zile mbegu zake, ndivi najua unapanda machipukia yake yanayozidi kuchipua. lakini sifahamu

hili zao la nanasi mbegu yake ni nini?

Msaada plz
 
Kama ni nanasi hili hili tunalolijua linapandwa hivi;
Nanasi likisha toa tunda lake halifi,bali huto machipukizi (suckers),haya machipukizi hayatokei chini kama mgomba ufanyavyo bali yanatokea kama matawi kutoka ktk nanasi mama.Lile chipukizi huanza kutoa mizizi hata kabla halijaondolewa toka nanasi mama,lakini mizizi hiyo imefichwa na maganda.

Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kunyofoa chipukizi toka nanasi mama na kuondoa maganda yanayozuia mizizi isionekane, kisha unapanda ktk udongo kama tunavyopanda miche mingine.

Nisamehe bure kama nimetoa maelezo yasiyotosheleza swali lako.
 
Unalijua nanasi lilivyo likiwa either shambani au sokoni? hebu lielezee ili iwe rahisi kukuelewesha jinsi ya kuliotesha.
 
Back
Top Bottom