Vyakula 16 venye kuongeza kinga ya mwili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,572
44,796
Chukua hiyo tuongeze maarifa juu ya tiba lishe

Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.

Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani kama umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu na ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula na mitishamba 16 inayoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

1. MTINDI (yoghurt).

Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza kinga ya mwili wako

2. MATUNDA.

Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Unaweza kuamua pia moja ya mlo wako katika siku kama ni wa jioni au wa mchana au wa asubuhi uwe ni matunda tu na si kitu kingine zaidi. Jaza kwenye sahani yako ndizi, embe, papai, nanasi, tikiti maji, parachichi nk, sahani iwe na matunda tu kula hadi ushibe matunda tu.

.

3. Tui la Nazi:

Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huwa na uwezo wa kuiimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali”.

Matumizi ya nazi kama tiba ya kuimarisha kinga ya mwili duniani yalishika kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii. Waathirika wa UKIMWI toka sehemu mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba.

Dozi yake ni rahisi, kunywaji glasi nne za tui la nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na kupungua kwa kinga ya mwili na pia hung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama kinga yako imepunguwa basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

4. VITUNGUU SWAUMU”.

Hupatikana kwa wingi Tanzania! Japokuwa vitunguu swaumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

Chukuwa kitunguu swaumu kimoja, Kigawanyishe katika punje punje, chukua punje 6 hivi, Menya punje moja baada ya nyingine. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu, Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2.

5. Mlonge:

Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu.

Taarifa zisizo rasmi zinadai Wachina hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatoweka wote Tanzania.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

MLONGE UNA:

Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI;

6. Asali yenye Mdalasini

Asali ni dawa kwa kila ugonjwa, zingatia tu unapata asali mbichi na nzuri ya asili kwani endapo utauziwa asali iliyochakachuliwa kuna hatari ya kuharibu afya yako zaidi. Katika kila lita moja ya asali ongeza vijiko vikubwa vya chakula 8 vya unga wa mdalasini na uchanganye vizuri kisha lamba kijiko kimoja cha chakula cha mchanganyiko huo kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja hivi kinga yako ya mwili itarudi katika hali yake nzuri.

7. UYOGA:

Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

8. SUPU YA KUKU:

Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

Mhimu ni kuwa supu hii ya kuku hakikisha ni ya kuku wa kienyeji tu.

8. Mafuta ya habbat soda
Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi. Mafuta ya habbat soda ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa muda mfupi.

Ukiacha hili la kuongeza kinga ya mwili, Habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo.

9. Ubuyu:

Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku (kumbuka uwe ubuyu halisi). Ubuyu una vitamini C nyingi zaidi kuliko ile ipatikanayo kwenye machungwa au maembe.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

11.VIAZI VITAMU(mbatata):
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu

12. KAROTI:

Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

13. SAMAKI:

Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

14. MATIKITI:

Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Faida 13 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake

15. MAJI YA KUNYWA:
Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunwya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau glasi 8 hadi 10 za maji kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.

Kila mtu ana kiasi cha maji anachohitaji kunywa kila siku kwa mjibu wa uzito wake.

16. Mbegu za Maboga:

Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida lukuki mwilini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.

Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu.
 
9f4a4437-a7e2-4725-a130-b6d0079be55d.jpg
 
Back
Top Bottom