Nampenda rafiki wa dada yangu

BIF

Member
Aug 2, 2012
47
10
Kumtokea rafiki wa kike wa dada yako ni mbaya?.Coz nimetokea kmpenda rafiki wa dada yangu but naona noma kemtemea madini nahic sister anaweza nifikiria vibay,Nifanyeje wa kubwa.
 
How old are you son? Go for it son, afterall she'll not tell trust me. For the sis, she'll jump and roll with joy knowing that the bro is a man!
 
Jiandae na wewe kuwaita rafiki zako shemejiiii.
 
Zinakuwa ngumu sana hizo za kumtokea rafiki wa dada wengine huomba ruhusa kwa dada zao kabla ya kuanza rasmi mchakato. Wakati mwingine dada hutoa ruhusa na wakati mwingine huweka ngumu.

Kumtokea rafiki wa kike wa dada yako ni mbaya?.Coz nimetokea kmpenda rafiki wa dada yangu but naona noma kemtemea madini nahic sister anaweza nifikiria vibay,Nifanyeje wa kubwa.
 
haha wee ongea na dada bana...atakuelewa tuu...sii umempenda sasa tatizo nini
 
How old are you son? Go for it son, afterall she'll not tell trust me. For the sis, she'll jump and roll with joy knowing that the bro is a man!

Hujamshtukia tu? huyu dogo bwana! Ndo walewale under 18
 
Kwani huyo dadako ni mama wa huyo binti hata achukie, ikiwa nae binti kakuzimikia issue ya dadako ni ndogo sana to deal with
 
Sioni Mbaya .. jaribu bahati yako.
We umeashampenda na hujui kama atakukubali Duhhhh. Haya bana kazi unayo.
 
Katika tamaduni zetu ndugu ndiye anayeweza kuwa na mjadala, rafiki wa dada?

Najua kutegemea na mahusiano uliyo na dada yako, rafiki wa dada anaweza kuchukua muonekano kama wa dada, lakini si dada.

Mbona mara nyingi katika jithada za kupata mtu anayejulikana tabia yake vizuri huo uhakika wa rafiki wa dada unahusika sana, maana anakuwa mtu ambaye kashapata ukaribu na familia hata kabla ya kujua matunda ya mahusiano hayo, na hivyo kutoa nafasi ya kumjua tabia yake vizuri pasipo na tamalaki la mahusiano ya jinsia tofauti ambalo linaweza kuleta ubalozi usio na uhalisia.

Kuna nyumba nyingi sana ambazo dada akiona kaka anazembea au kashupalia habari nyengine, na kuna rafiki anayestahili kwa taadhima zote anaweza kabisa kufanya mambo yanayoshauriwa na makungwi wote werevu kuwaweka pamoja pasipo muonekano wowote wa kufanya hivyo.
 
Kwani huyo dadako ni mama wa huyo binti hata achukie, ikiwa nae binti kakuzimikia issue ya dadako ni ndogo sana to deal with

Sidhani kama mleta thread yuko serious sana..
Kuanza kuwa na wasiwasi na dada yake inaonyesha anataka ku'hit' and 'run'
 
Katika tamaduni zetu ndugu ndiye anayeweza kuwa na mjadala, rafiki wa dada?

Najua kutegemea na mahusiano uliyo na dada yako, rafiki wa dada anaweza kuchukua muonekano kama wa dada, lakini si dada.

Mbona mara nyingi katika jithada za kupata mtu anayejulikana tabia yake vizuri huo uhakika wa rafiki wa dada unahusika sana, maana anakuwa mtu ambaye kashapata ukaribu na familia hata kabla ya kujua matunda ya mahusiano hayo, na hivyo kutoa nafasi ya kumjua tabia yake vizuri pasipo na tamalaki la mahusiano ya jinsia tofauti ambalo linaweza kuleta ubalozi usio na uhalisia.

Kuna nyumba nyingi sana ambazo dada akiona kaka anazembea au kashupalia habari nyengine, na kuna rafiki anayestahili kwa taadhima zote anaweza kabisa kufanya mambo yanayoshauriwa na makungwi wote werevu kuwaweka pamoja pasipo muonekano wowote wa kufanya hivyo.

kiswahili chako kiko deep sana. Hongera nyingi
 
huyu mleta mada inaonekana ni wale wa kumega na kutupa na hii itasababisha mpaka huyo rafiki wa dada yako akorofikishane na dada yako potezea tu haupo serious mkuu
 
Rafiki wa dada yako anatokewa tu hakuna shida sema tatizo hapo ukiharibu tu unaweza ukaharibu na uhusiano wa wao wawili
 
  • Thanks
Reactions: BIF
Back
Top Bottom