Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,496
- 52,135
NAMPELEKA MAHAKAMANI MWANAMKE NILIYEZAA NAYE KWA KUSHINDWA KUMHUDUMIA MWANAYE. HOJA NITAKAZOPELEKA MAHAKAMANI NI HIZI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Lazima naye ahudumie. Sikumtuma abebe mimba na anizalie mtoto. Wakati tunafanya alivyokuwa anajichetua, kujibinjua, kubiringita, kujipogoa na kunengua achimenengule kama Akudo band alikuwa akichekelea. Hakujua ikiingia mimba kuna majukumu ya kulea?
Anyway! Hizi ndio Hoja ambazo nimeziandaa kwa ajili ya kungurumisha kesi Mahakamani. Na lazima nipate pesa za matumizi ya mtoto kutoka kwa huyu Mwanamke niliyezaa naye;
1. Uroda tulipata Nusu kwa Nusu tena yeye ndiye alihitaji nyongeza.
Ndugu Mhe. Hakimu. Upatikanaji wa mtoto huyu ni matokeo ya uchu na tamaa zetu mbaya ambazo hata hivyo zilitufurahisha kwani tulistarehe. Na wote tulienjoy Hasahasa huyu Mwanamke yeye alihitaji nyongeza. Na aliipata.
Kama tulivyoshirikiana kupata uroda siku ileile nusu kwa nusu. Basi tushirikiane pia nusu kwa nusu kuwajibika na matokeo ya Uroda ule ambao ndio huyu mtoto wetu.
2. Jenetikali tumempa mtoto Nusu kwa Nusu vinasaba vyetu.
Tena Hakimu kama utakuwa unamacho yanayoona vizuri hutoshindwa kuona kuwa huyu mtoto kachukua sura kutoka kwa Mamaake zaidi. Sisemi kwamba hiyo itamfanya awe na Wajibu zaidi wa kumhudumia mtoto. Ila najaribu kueleza kuwa hata Mwanamke anatakiwa kutoa huduma kwa mtoto wake nusu kwa nusu kwa mwanaye kama alivyochangia chromosome 23 na Mimi chromosome 23 ambayo ndio imemfanya mtoto huyu awe na 46 chromosome.
Kila mtu atunze chromosome zake 23 alizompa huyu mtoto.
3. Haki Sawa .
Mheshimiwa. Hakimu. Kwenye haki Sawa huyu ni mtoto wetu sote. Hivyo ni wajibu wetu kutoa huduma Sawa kiwajibu na kwa Mujibu wa sheria. Kwa mfano kama matumizi na huduma ya mtoto ni 300,000/= kwa mwezi basi kila mzazi atoe 150,000/= kwa sababu ndio Haki.
Mtoto ni mali yetu sote.
Kama kuna atakayetaka kutoa zaidi kwa hiyari/mapenzi yake kwa mtoto hiyo isihusianishwe na sheria na isitajwe hapa Mahakamani kwa sababu ni hiyari na mapenzi ya mtu.
4. Hii itamfanya Mwanamke huyu atafute kazi ya kufanya ili awe na faida kwa taifa.
Mwanamke kumhudumia mtoto wake italisaidia taifa kuondoa utegemezi.
Ndugu Hakimu, nashukuru kwa sababu kwenye kesi hii wewe ni mfano wa wanawake wanaofanya kazi. Na kulitumikia taifa. Ninauhakika hata wewe unahudumia watoto wako. Na hii inapunguza utegemezi ndani ya nchi.
5. Itapunguza kuzaa bila mpango na itadhibiti idadi kubwa ya Watu wasio na tija.
Wanawake wengi wanaozaa watoto wengi ni kwa sababu hawawajibiki kuwatunza na kuwahudumia. Ni aidha wawapelekee Mama na baba zao(Bibi na babu). Au watakuwa wanasumbua wanaume waliozaa nao wawahudumie .
Mwanamke anayehudumia watoto wake ni ngumu kuzaa idadi ya watoto wengi asioweza kuwalea.
Hii itafanya watoto watakaozaliwa wawe na tija.
Mhe. Hakimu, kesi hii kama angekuwa mke wangu au mwanamke ninayeishi naye ingekuwa tofauti kidogo katika hoja zangu nilizotoa. Kwa sababu tungekuwa kitu kimoja yaani familia. Na mimi kama mwanaume ambaye ni mume ningebeba jukumu la Baba na Mume. Lakini kwa sasa sisi hatuishi pamoja hivyo nimebaki na jukumu la Baba na yeye kabaki na jukumu la Mama. Na sisi sio kitu kimoja, sisi sio familia. Ndio maana hii kesi ipo mahakamani.
Naomba hiyo pesa ya matumizi na huduma iingizwe kwenye akaunti yangu ya Benki au namba ya simu anayotumia kuwasiliana na Mimi.
Asante sana.
Sabato Njema.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam