Namna ya kupiga hesabu ya material kwa uhakika

Black Thought

Senior Member
Feb 25, 2015
160
406
Habari wakuu.
Nimekua nikiona members humu wakiulizia kuhusu idadi ya material kwa nyumba.

Sasa kwa ufupi ukitaka kupiga hesabu kwa uhakika unatakiwa kujua
1. urefu (running meter) wa nyumba (yani ukiikunjua nyumba kama kamba itakua na urefu gani). Hii itakusaidia kupata idadi ya tofali za msingi, mchanga na cement wa kuzijenga tofali hizo ,
na pia hii itakupa material yote ya zege la mkanda wa chini na wajuu (plinth beam na lintel). Tofali lina urefu wa inch 18 (kama 45.7cm) sasa ukiweka na mortar inakua around 47.7cm. Sasa hapo utachukua running meter utagawa kwa hiyo kupata kozi moja itachukua tofali ngapi. Na kwa kiwanja level ni wastani wa kama kozi sita msingi

2. Unatakiwa kujua surface area ya jengo (super structure) ukiwa umetoa areas za openings zote kwa maana ya milango na madirisha. Hii itakuasaidia kupata idadi ya tofali, mchanga na cement ya kujengea kuta za juu (boma). Kwa tofali za blocks- square meter moja kimahesabu ina tofali 9 (pamoja na wastage).

3. Roof surface area ya bati ikiwa katika angle husika ambapo hii itakupa idadi ya bati n.k kwenye kupaua. Utagawa kwa effective surface area ya bati moja (bati zinatofautiana upana)

4. Kwa urahisi kabisa utatumia perimeter ya jengo kupata idadi ya material ya kufanyia settingout ya jengo. Zingatia kuongeza angalau 1.5m kwaajiri ya kutoa setting (profile nje), mfano kama jengo lina mita 10X12 inakua ni mita 13x15 ndio unaitafutia mzingo
 

Attachments

  • IMG_6772.png
    IMG_6772.png
    717.3 KB · Views: 17
  • IMG_6777.jpeg
    IMG_6777.jpeg
    211 KB · Views: 12

Similar Discussions

Back
Top Bottom