SoC04 Namna nilivyotaka kujiua baada ya kukata tamaa ya kuishi

Tanzania Tuitakayo competition threads

philantrhopist

JF-Expert Member
Jun 18, 2023
408
688
Hivi karibuni nyuzi zangu nyingi zimekuwa zikielezea hali halisi ya maisha yangu.

Moja wapo ya uzi uliokuja kuokoa maisha yangu ni ule wa.....www.jamiiforums.com/threads/hivi-ni-mimi-tu-haya-maisha-yanataka-kunikataa.2210301/.

Na hii ni baada ya kukuta watu wawili walionionea huruma na kunifuata PM (ujumbe wa siri) hadi tukapeana mawasiliano hapo ndipo nilipopata msaada na sasa jua lililotaka kwenda machweo likawiwa tena.

Mimi ni kijana mpambanaji sana niliyeajiriwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanganyika na Zanziba. Elimu niliipata kwa shida sana ambayo imenipa ajira ya ualimu serikalini kwa ngazi ya Daraja la 3 A (yaan certificate).

Nimeajiriwa miaka kumi iliyopita lakini hadi sasa sina mke wala mtoto wa kusingizia. Hii inatokana na majukumu niliyonayo katika familia kwa sababu mimi ndiye kijana pekee niliyehitimu elimu ya kidato cha nne.

Mshahara wangu ni mdogo sana haukidhi mahitaji vizuri, kwa hiyo inanihitaji kukopa mara kwa mara ili kusaidia wadogo zangu kusoma na pia familia kupata mahitaji maalumu. Asikuambie mtu nyumba ambayo wanaishi wazazi na wadogo zangu ni ya tope na imeezekwa kwa nyasi ambapo ni moja tu na kajiko kadogo kwa pembeni.

Yaani familia yetu ni maskini kwa ujumla hata mifugo na kilimo ni cha shida kwa sababu kama huna hela mifugo hutoweza kuwahudumia pia kilimo kinahitaji hela. Vivyo hivyo wazazi wangu ni wazee sana hata lile jembe la mikono kwao kwa sasa ni kuwachosha tu.

Wadogo zangu nao elimu ni ya shida na wapo tano mmoja kidato cha sita, wa pili cha nne, watatu cha pili, wa nne la saba na wa tano la nne. Kumbuka niliye na unafuu ni mimi tu na macho yote kwangu, ukianzia mavazi na madaftari shuleni na vinginevyo.

Ooh Maskini! hivi ni kweli ng'ombe wa maskini hazai. Majukumu yote kwa mtu mmoja. Yaani nawaza hadi ubongo unataka kupasuka. Kumbuka ni ndugu zangu siwezi kuwaacha ujue. Na ukiacha tena ndio hivyo unatengeneza ukoo wa walala hoi wote ambapo hakuna wa kumshika mwingine. Bora watu wapate hata hiyo elimu ili iwaondoe ujinga. Asikwambie mtu nainoea huruma familia na kizazi au ukoo unaotokana na wazazi wangu. Kwani nikipata shida sina kwingine pa kukimbilia tofauti na kuwaimarisha ndugu zangu.

Unaweza kujijali mwenyewe lakini ipo siku utahitaji ndugu zako kwenye jambo lolote ama la kijamii au kiuchumi. Ndivyo hivyo tena hata kama upo na marafiki unaogopa kuwatambulisha ndugu zako walivyo walala hoi hawana nyuma wala mbele.

Asalaalee! maskini kijana mmoja ninayetegemewa na familia ya wazazi wangu. Nimekopa hadi kadi ya benki imeshikiliwa mtaani. Nimeuza hadi vitu vya ndani nimebaki na godoro tu. Hadi wakati mwingine nashinda njaa. Ee Mungu nakulilia mbona huu mzigo mzito nimeshindwa kuubeba🧘‍♂️🧘‍♂️😭😭😭. Nilikopa ili kuwajengea wazazi lakini ujenzi si haba nimeishi kwenye lenta na ni vyumba viwili na sebule.

WAKATI JUA LINATAKA KUCHWEA. Nimempata binti wa chuo mrembo mwaka wa kwanza nataka nimuoe na wazazi wamekubali nikalipe posa. Nilipojichanganya nimeenda benki NMB kukopa milioni tano. Nimechanganywa na umbo la binti na sura mtoto wa kirangi. Posa ni milioni moja na laki tano. Papara nikachukua wazee gharama zote nikalipa yaani ikakata milioni mbili na laki saba.
Majonzi mazito binti ameendelea na masomo kwa muda miezi mitatu tamaa zikamshika akabebeshwa mimba na jamaa mwenye mali na utajiri wake. Ee Mungu pamoja na vitisho niachane naye, nikazuiliwa hadi simu zangu kupiga 😭😭😭. Kumpata tena ni kazi Catherine umeua moyo wangu hadi kazini nashindwa kuhudhuria tena vizuri.
GIZA ZITO NDANI YA MACHO YANGU NA UBONGO UKAGANDA KAMA BARAFU
Baba kagongwa na boda na kufariki. Nimelia hadi makamasi yakachuruzika puani. Sivyo tu! hadi nikajikoloea. Nikienda chooni ni kuharisha, viungo vya mwili havina ushirikiano kabisa. Nani wa kuwezesha msiba? ni mimi....kwa hela ipi? iliyobaki baada kulipa mahari. Basi tukazika huku nikiwa nimebaki na vilio viwili vya kuachwa na mzazi pia mchumba wangu Catherine.
Mwili wangu umekuwa na mawazo kujiua tu baada kukutana na matukio hayo pamoja na madeni yasiyoisha huku nikikosa hadi chakula.

Kilichoniokoa ni baada ya kutuma uzi huku jf. Hivi ni mimi tu haya maisha yanataka kunikataa?.

MAWIO YA JUA, TABASAMU LINAANZA KURUDI.
Watu wamenifuata PM na kunitia moyo pia jumbe za watu (comments) za watu ndani ya uzi. Kuna jamaa mmoja amejitokeza na kunipa kazi ambayo baada ya kazi yangu ya ualimu jioni najishikiza hapo kupata hela ya chakula na kupunguza madeni. Asante Mungu Jamii Forum imeniokoa nimeanza kupata matumaini ya kuiona siku ya leo.

Ukipata changamoto leo kuna kesho usiyoijua. Wengi tupo sehemu ambazo hatujui tulifikaje na kufanikiwaje. KUNA JINA LENYE NGUVU LINALOSHINDA UWEZO WA KUFIKIRI. AMINI IPO KESHO YAKO BORA ZAIDI KULIKO LEO. UKIKOSA LEO KESHO HUKOSI AMA UTAPATA KIZURI ZAIDI.

Ujumbe kwako unayetaka kukata tamaa. Wapo watu ambao hawana viungo vyote lakini wanapambana ili kuilinda pumzi ya Mungu. Kamwe usijichukulie sheria mkononi. Yupo huyu atoae riziki bila uchoyo. Kazana kwa bidii na kuomba unayemuamini atakusadia yaani jina kuu linaloshinda majina yote. Amina.

Mungu awabariki nyote. Aiiimeeeni.
 
Haiya, sasa ukiachana na hali ya matatizo yako. Una maoni gan kwa Tanzania. Yaani nini kifanyike kama sehemu ya suluhisho la kusiwepo matatizo....

Tupe picja ya Tanzania tunayoitaka
Mimi kama mlipa kodi wa kwanza, kodi yangu isimamiwe ipasavyo ili ituletee maendeleo sote na sio watu wachache wafaidi kodi zetu.
 
Pole Sana

Ila Tanzania tuitajayo itafaidika vipi na watu Kama nyie ambao mmeamua kuwa sehemu ya kulalamika na kuteswa na hisia

Ebu tupe suluhisho - je ingefaa kuhimiza Elimu au matibabu ya kisaikolojia kuwa kubwa Sana kwa watu Kama nyie ambao mmekata Tamaa na maisha.
 
Pole Sana

Ila Tanzania tuitajayo itafaidika vipi na watu Kama nyie ambao mmeamua kuwa sehemu ya kulalamika na kuteswa na hisia

Ebu tupe suluhisho - je ingefaa kuhimiza Elimu au matibabu ya kisaikolojia kuwa kubwa Sana kwa watu Kama nyie ambao mmekata Tamaa na maisha.
usishangae anayetoa mawaidha ya mapenzi naye anateswa na mapenzi
 
Back
Top Bottom