Maseto
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 944
- 545
Nilimsikiliza kwa makini jana Profesa Tibaijuka juu ya mradi wa Kigamboni.Aliposema juu ya kuwapeleka baadhi ya wananchi wa kigamboni kutembelea miji mbalimbali kujifunza juu ya miji bora,nilianza kuhisi kuwa kuna tatizo juu ya huu mradi.Mimi naishi kijiji fulani huku Mtwara lakini huwa nafuatilia mambo ya mjini.
Nilimsikiliza pia mbunge wa Kigamboni jana na leo.Lakini kilichonishitua zaidi ni maelezo ya Tibaijuka wakati wa majumuisho.Kwa kiwango fulani hakuwa yule mama ninayemfahamu.
Kuna mambo matatu hajaeleweka juu ya mradi wa Kigamboni:
1. Inakuwaje waziri kuwapeleka baadhi ya wananchi kujifunza nje wakati hilo si tatizo lao.Tatizo lao ni namna mradi utakavyowafaidisha wao.
2. Mchanganuo wa matumizi ya pesa iliyotengwa yakoje.Pesa shilingi 60 bilioni ni ndogo sana kwa mradi mkubwa kama ule.
Nimeshindwa kumuelewa Mama leo.Inatisha kuona kuwa mama aleyefanya mafanikio makubwa duniani anakuwa haeleweki hivi!
3. Suala la kuwaalika Madiwani hao wanne lilitakiwa kutolewa maelezo ya kina.
Mimi nasema kuna tatizo juu ya mradi huu wa Kigamboni.Pengine kuna mambo yaliyojificha ambayo hatuambiwi vizuri.