MWANZA: Jiji la Pili kwa Ukubwa lakini halipewi hadhi yake

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
414
877
Nikiwa raia na mwananchi wa kawaida mpenda maendeleo, naandika barua hii kwa ajili ya mkoa wa Mwanza, ningependa sana kama Raisi wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani ukapata ujumbe huu.

Basi hata kama kuna watu wapo karibu naye na wakasoma ujumbe huu basi wamfikishie. Au kama atabahatika kuingia mtandaoni akauona mwenyewe itakuwa vizuri zaidi.

Heshima yako mkuu, Raisi wa JMT,

Itifaki imezingatiwa.

Kabla ya yote naanza na salamu yetu pendwa, “Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Mheshimiwa Rais bila kupoteza muda niende kwenye mada.
Mwanza ni moja ya majiji yanayokua kwa kasi Africa. Ukuaji huu unatokana na mazingira safi ambayo yanawavutia watu kuhamia na kuwekeza. Pamoja na kuwa Mwanza ni mkoa wa pili kwa udogo wa eneo baada ya Dar es Salaam lakini pia ndiyo mkoa ambao unafanya mambo makubwa katika nyanja mbalimbali hapa nchini katika kuongeza pato la Taifa ukiwa nyuma ya mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya mambo yanayoubeba mkoa na kuufanya kuwa namba mbili Tanzania ni haya hapa baadhi yake.
  • Mwanza ni mkoa wa pili kwa wingi wa watu Tanzania baada ya Dar es Salaam. Pamoja na ukubwa huu serikali bado haijaanza kuupa thamani mkoa huu kulingana na ukubwa wake. Kwa sababu hiyo Mwanza ni mkoa potential sana kwa sababu ina watu wengi lakini eneo lake ni dogo. Kwa maana hiyo watu wapo karibu karibu, hata huduma za kijamii kusambaza ni rahisi, kufanya biashara pia ni rahisi sababu unapata watu wengi katika eneo dogo. Watu wake hawajatawanyika kama ilivyo mikoa mingine.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuchangia pato la taifa baada ya Dar es Salaam. Kwenye swala la uchumi Mwanza inafanya vizuri ikizidiwa na Dar es salaam pekee. Kwa maana hiyo shughuli za binadamu za kujiingizia kipato ni nyingi na biashara zinafanyika sana. Ndiyo maana Pamoja na kuwa ndogo kieneo lakini inakusanya mapato mengi kuliko mikoa ambayo ni mikubwa kwa eneo.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuwa na wasafiri wengi wa ndani wanaotumia usafiri wa Ndege kupitia uwanja wa ndege Mwanza baada ya Dar es Salaam. Kwa mantiki hiyo mkoa una fursa za kutosha ndiyo maana wasafiri wa ndege ni wengi wanapenda kutembelea mkoa huu.
  • Ni mji wa pili kwa kuwa na idadi kubwa wa mabasi ya mikoani baada ya Dar es Salaam. Pointi hii haitofautiani sana na namba 3. Hii ina maana kuwa wageni wengi wanaingia na kutoka ndani ya mkoa kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Idadi hii ya watu kuingia kwa wingi siyo bahati mbaya, bali ni sababu mkoa una mvuto na fursa mbalimbali.
  • Ni mkoa wa pili wenye vituo vingi vya kujaza mafuta ya Magari (Filling stations) pia ni mkoa wa pili kwa kuuza zaidi mafuta ya Petrol na Dizeli baada ya Dar es Salaam. Kwa takwimu hizi inaonesha Dhahiri kuwa sector ya usafirishaji na matumizi ya Magari Mwanza iko vizuri. Takwimu hizi zinavutia wawekezaji wa kuuza mafuta ya magari, hiyo ni fursa kwao.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuwa na watumiaji wengi wa line za simu (SIM card subscribers) nyuma ya Dar es Salaam. Kwa maana hiyo kwa Sector ya mawasiliano ina wateja wa kutosha kulinganisha na mikoa mingine.
Kwa takwimu hizo hapo juu nadiriki kusema kuwa Mwanza inazidiwa na Dar es Salaam pekee kwa mambo mengi sana pamoja na hayo niliyotaja ambayo ni baadhi tu kati ya mengi.
Baada ya kutaja sifa zinazoifanya Mwanza kuwa mkoa namba mbili, pia kuna fursa mbalimbali ambazo zinaifanya Mwanza iendelee kuwa namba mbili muda wote. Baadhi ya fursa hizo ni kama ifuatavyo.
  • Ziwa kubwa (Victoria) linalounganisha baadhi ya nchi za jumuia ya Africa Mashariki, uwepo wa madini pamoja na ufugaji. Kwa hiyo kuna fursa nyingi za kiuchumi mkoa wa Mwanza kama vile uvuvi, ufugaji wa samaki, kilimo Cha umwagiliaji, uchimbaji wa madini, ufugaj wa mifugo, uendeshaji wa viwanda vya vinywaji, viwanda vyaSamaki na viwanda vya nyama.
  • Jiji la Mwanza ndilo Jiji pekee Afrika mashariki lipo karibu na miji (majiji) mikuu mingi ya wanachama wa Africa mashariki kama vile Kampala (km 722), Bujumbura (km 675), Kigali (km 540), Nairobi (km 682). Kutokana na kuwa karibu na majiji hayo ndio maana tukasema kuwa Mwanza ni kitovu cha Afrika mashariki. Niwapongeze serikali kwa ujenzi wa SGR na kuweka bandari kavu Mwanza. Hii itarahisisha usafirishaji wa mizigo na bidhaa mbalimbali kutoka Mwanza Kwenda wanachama wa Africa Mashariki.
  • Mkoa wa Mwanza unapakana na mbuga kuu ya Wanyama ya Serengeti. Kwa mtalii kutokea Mwanza atasafiri safari fupi kufika Serengeti kuliko aliyeshukia KIA au JNIA. Kuna mbuga zingine kama Rubondo na Kisiwa cha Saanane.
  • Wilaya za Mwanza zipo karibukaribu sana. Unaweza kupanda daladala moja na ukapita wilaya 4 za mkoa. Mfano daladala za KISESA-NYASHISHI unapita wilaya za Magu, Ilemela, Nyamagana na Misungwi. Hizo ni daladala za mjini. Ukaribu huu wa wilaya unaifanya Mwanza ivutie kwa uwekezaji sababu watu wanapatikana wengi katika sehemu ndogo ya eneo.
  • Mwanza ni jiji la miamba, miamba hii inaweza kuwa fursa kwa watalii kuja kujionea jinsi mawe yalivyobebana. Kule Ukerewe kuna jiwe huwa linacheza, ni utalii tosha kwa mkoa huu.
Pamoja na fursa zilizoorodheshwa hapo juu, bado kuna changamoto za kimiundombinu katika mkoa huu wa Mwanza. Nitataja baadhi tu.
  • Uwanja wa Ndege hauna hadhi
Uwanja wa ndege ni kero kubwa kwa sasa. Uwanja hauna hadhi ya ukubwa wa mji wa pili kwa ukubwa Tanzania. Huu uwanja upoupo tu, ni kama sio uwanja mkuu wa mkoa ambao pato lake linachangia taifa kwa nafasi ya pili. Majengo yaliyopo yanatia kinyaa hayatamaniki hata kuyaona. Jengo la abiria linajengwa nalo limekwama kwa muda sasa, haliendelei miaka nenda rudi lipolipo tu
Wafanyabiashara wengi wa viwanda vya Samaki na nyama ya ng’ombe na bidhaa zingine zinazosafirishwa nje ya nchi inawabidi wasafirishe bidhaa zao mpaka Dar es Salaam ambapo inachukua muda mrefu mpaka mzigo kuufikisha na kuusafirisha. Wenadai kuwa ubora wa bidhaa zao unaharibika sababu ya kukaa njiani muda mrefu. Kama uwanja wa kimataifa ungekuwepo basi bidhaa ingeweza kutengenezwa (processed) siku hiyohiyo na kusafirishwa siku hiyohiyo bila kupoteza ubora wake.
Ni aibu sana mkoa wa pili kwa ukubwa hauna uwanja wa ndege wa Kimataifa. Mkoa unakosa fursa ya kupokea wageni wa moja kwa moja kutoka nchi za nje. Uwepo wa uwanja wa kimataifa ungeimarisha utalii wa mkoa na kanda ya ziwa kwa ujumla. Kuna usemi mtaani kwamba uwanja wa ndege unahujumiwa na kucheleshwa kwa makusudi kwa hofu ya kupunguza wasafiri katika baadhi ya viwanja vya kimataifa nchini. Sina uhakika kama ni kweli, lakini wahenga walisema lisemwalo lipo.
  • Barabara mbovu
Nafikiri kwa majiji Tanzania, Mwanza ndiyo jiji lenye barabara mbaya kuliko zote. Hata baadhi ya Manispaa zina barabara nzuri kuliko jiji la Mwanza. Barabara ya Mwanza-Shinyanga (Kenyatta Road) ni mbaya sana. Ni aibu barabara kama hii kuwa ndani ya jiji. Barabara ni nyembamba mvua ikinyesha pembeni inaliwa na maji, barabara ina mashimo mengi sana katikati. Ni barabara ambayo kila mgeni anayeingia Mwanza lazima apite hapo.

Ni aibu sana kwa mtu anayeingia Mwanza kwa mara ya kwanza aone barabara ya namna hiyo halafu umwambie Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania.

Barabara hii inatakiwa ijengwe njia nne au sita ili baadae isije sumbua na kuongeza gharama za kulipa fidia. Ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi (JPM Bridge) utaongeza jam kwenye barabara hii, hivyo bora ikajengwa njia sita mpaka Usagara, halafu ikajengwa njia nne mpaka Misungwi. Serikali isijifanye haioni huo uozo wa barabara hii, hata hivyo Mkoa haupewi hadhi yake ya kuwa mkoa namba mbili Tanzania. Pia barabara ya Kigongo (JPM Bridge) Kwenda Kisesa ijengwe njia nne.

Barabara nyingine ni barabara ya Mwanza-Musoma (Nyerere Road). Hii barabara angalau inajitahidi, ina njia tatu lakini nayo imezidiwa inahitaji kupanuliwa kuwa njia sita kama itakuwa ngumu basi ijengwe njia nne mpaka Nyanguge. Kuna barabara za kimkakati ambazo zinatakiwa zijengwe haraka iwezekanavyo Kwa mfano barabara ya Airport-Kisesa kupitia Kayenze. Barabara hii ikikamilika italeta fursa kwa wilaya za Ilemela na Magu na kuokoa muda. Mgeni akishuka Airport kama anakwenda uelekeo wa Musoma, hii barabara itakuwa shortcut nzuri kwake.

Pamoja na hayo kuna barabara nyingi za mitaa ambazo zinatakiwa kujengwa na kuboreshwa katika jiji la Mwanza. Baadhi yake ni Buhongwa-Igoma, Buswelu-Nyamhongolo, Buswelu-Coca-cola, Mkuyuni-Nyakato nk.
  • Maji ni Shida
Mwanza bado kuna kero ya maji sehemu mbalimbali za jiji. Mfano kata ya Buswelu maji yamekuwa adimu kama dhahabu. Maji yanaweza kutoka mara moja kwa wiki tena usiku wa manane. Tuna mabomba lakini yamekuwa kama mapambo hayatoi maji kabisa. Haya mambo yote yanatia aibu jiji letu la Mwanza.
  • Ucheleweshwaji wa miradi katika jiji la Mwanza
Kuna ucheleweshwaji mwingi sana wa miradi ya Mwanza. Miradi kama Soko Kuu, Stendi ya Nyegezi na Jengo la abiria la uwanja wa ndege, hii miradi imekuwa ikisuasua sana haieleweki inaisha lini. Viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ya uongo za tarehe za kufunguliwa au kukamilika miradi hii hasa stendi ya Nyegezi ahadi zimekuwa nyingi mpaka imekuwa kero. Kila mmoja anaahidi kivyake tarehe ya kufunguliwa stendi lakini muda ukifika hakuna kinachotekelezeka na ujenzi unakuwa bado unaendelea. Kwenye miradi mingine wanajitahidi hasa ule wa Daraja la JPM na Meli kasi inaridhisha, tatizo huwa mradi ukifika asilimia kuanzia 80 spidi huwa inapungua sana na mingine kusimama.

Hitimisho

Kwa changamoto hizo hapo juu yaani Uwanja wa ndege, Barabara na Maji zinatia doa, na aibu kwa nchi, serikali na viongozi kwa kutokujali mkoa ambao ni mkubwa namba mbili hapa nchini.
Nina imani nawe Raisi wetu mama Samia Suluhu Hassani, una nafasi kubwa ya kubadilisha mkoa huu na kuwa mji wa kisasa na mfano kwa kanda ya Africa Mashariki.

Kwa nafasi yako uliyonayo kama Raisi wa JMT unayonafasi ya kuandika historia Kwa kufanikisha maono haya kwa vitendo ambayo yamekuwa yakisemwa na watangulizi mbalimbali waliopita kwamba wanataka kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara Africa Mashariki. Na unaweza kufanya hivyo ukaacha alama yako kwa wana Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla.

Pia mama yetu Raisi wa JMT nina ombi la nyongeza, nikuombe kitu kingine ila hakikuwa kwenye andiko langu, wana Mwanza tunaomba utujengee chuo kikuu yaani UNIVERSITY OF MWANZA. Tutafurahi kuona Mwanza inapata chuo kikuu chini ya Utawala wako. Ni mkoa mkubwa kihistoria na kiuzalishaji. Hakika hilo likifanikiwa utakuwa umeweka alama ambayo itakumbukwa sasa na vizazi vijavyo.

Nikutakie majukumu mema katika kulijenga taifa letu la Tanzania.

Wako,

Mwananchi
 
Mwanza ipo nyuma sana kwa kweli, hata watu wake wanaonekana wamechoka kwa shida na wamekata tamaa.... sijui shida ni nini ila nadhani serikali ikiweka nguvu zote kule litakua jiji zuri na kuvutia wageni wengi, muingiliano wa watu ukiwa mkubwa huo ushamba wa wazawa utaisha na wenyewe watachangamka.
 
Nikiwa raia na mwananchi wa kawaida mpenda maendeleo, naandika barua hii kwa ajili ya mkoa wa Mwanza, ningependa sana kama Raisi wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani ukapata ujumbe huu.

Basi kama kuna watu wapo karibu naye na wakasoma ujumbe huu basi wamfikishie. Au kama atabahatika kuingia mtandaoni akauona mwenyewe itakuwa vizuri zaidi.

Heshima yako mkuu, Raisi wa JMT,
Itifaki imezingatiwa.
Kabla ya yote naanza na salamu yetu pendwa, “Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Mheshimiwa Rais bila kupoteza muda twende kwenye mada.
Mwanza ni moja ya majiji yanayokua kwa kasi Africa. Ukuaji huu unatokana na mazingira safi ambayo yanawavutia watu kuhamia na kuwekeza. Pamoja na kuwa Mwanza ni mkoa wa pili kwa udogo wa eneo baada ya Dar es Salaam lakini pia ndiyo mkoa ambao unafanya mambo makubwa katika nyanja mbalimbali hapa nchini katika kuongeza pato la Taifa ukiwa nyuma ya mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya mambo yanayoubeba mkoa na kuufanya kuwa namba mbili Tanzania ni haya hapa baadhi yake.
  • Mwanza ni mkoa wa pili kwa wingi wa watu Tanzania baada ya Dar es Salaam. Pamoja na ukubwa huu serikali bado haijaanza kuupa thamani mkoa huu kulingana na ukubwa wake. Kwa sababu hiyo Mwanza ni mkoa potential sana kwa sababu ina watu wengi lakini eneo lake ni dogo. Kwa maana hiyo watu wapo karibu karibu, hata huduma za kijamii kusambaza ni rahisi, kufanya biashara pia ni rahisi sababu unapata watu wengi katika eneo dogo. Watu wake hawajatawanyika kama ilivyo mikoa mingine.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuchangia pato la taifa baada ya Dar es Salaam. Kwenye swala la uchumi Mwanza inafanya vizuri ikizidiwa na Dar es salaam pekee. Kwa maana hiyo shughuli za binadamu za kujiingizia kipato ni nyingi na biashara zinafanyika sana. Ndiyo maana Pamoja na kuwa ndogo kieneo lakini inakusanya mapato mengi kuliko mikoa ambayo ni mikubwa kwa eneo.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuwa na wasafiri wengi wa ndani wanaotumia usafiri wa Ndege kupitia uwanja wa ndege Mwanza baada ya Dar es Salaam. Kwa mantiki hiyo mkoa una fursa za kutosha ndiyo maana wasafiri wa ndege ni wengi wanapenda kutembelea mkoa huu.
  • Ni mji wa pili kwa kuwa na idadi kubwa wa mabasi ya mikoani baada ya Dar es Salaam. Pointi hii haitofautiani sana na namba 3. Hii ina maana kuwa wageni wengi wanaingia na kutoka ndani ya mkoa kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Idadi hii ya watu kuingia kwa wingi siyo bahati mbaya, bali ni sababu mkoa una mvuto na fursa mbalimbali.
  • Ni mkoa wa pili wenye vituo vingi vya kujaza mafuta ya Magari (Filling stations) pia ni mkoa wa pili kwa kuuza zaidi mafuta ya Petrol na Dizeli baada ya Dar es Salaam. Kwa takwimu hizi inaonesha Dhahiri kuwa sector ya usafirishaji na matumizi ya Magari Mwanza iko vizuri. Takwimu hizi zinavutia wawekezaji wa kuuza mafuta ya magari, hiyo ni fursa kwao.
  • Ni mkoa wa pili kwa kuwa na watumiaji wengi wa line za simu (SIM card subscribers) nyuma ya Dar es Salaam. Kwa maana hiyo kwa Sector ya mawasiliano ina wateja wa kutosha kulinganisha na mikoa mingine.
Kwa takwimu hizo hapo juu nadiriki kusema kuwa Mwanza inazidiwa na Dar es Salaam pekee kwa mambo mengi sana pamoja na hayo niliyotaja ambayo ni baadhi tu kati ya mengi.
Baada ya kutaja sifa zinazoifanya Mwanza kuwa mkoa namba mbili, pia kuna fursa mbalimbali ambazo zinaifanya Mwanza iendelee kuwa namba mbili muda wote. Baadhi ya fursa hizo ni kama ifuatavyo.
  • Ziwa kubwa (Victoria) linalounganisha baadhi ya nchi za jumuia ya Africa Mashariki, uwepo wa madini pamoja na ufugaji. Kwa hiyo kuna fursa nyingi za kiuchumi mkoa wa Mwanza kama vile uvuvi, ufugaji wa samaki, kilimo Cha umwagiliaji, uchimbaji wa madini, ufugaj wa mifugo, uendeshaji wa viwanda vya vinywaji, viwanda vyaSamaki na viwanda vya nyama.
  • Jiji la Mwanza ndilo Jiji pekee Afrika mashariki lipo karibu na miji (majiji) mikuu mingi ya wanachama wa Africa mashariki kama vile Kampala (km 722), Bujumbura (km 675), Kigali (km 540), Nairobi (km 682). Kutokana na kuwa karibu na majiji hayo ndio maana tukasema kuwa Mwanza ni kitovu cha Afrika mashariki. Niwapongeze serikali kwa ujenzi wa SGR na kuweka bandari kavu Mwanza. Hii itarahisisha usafirishaji wa mizigo na bidhaa mbalimbali kutoka Mwanza Kwenda wanachama wa Africa Mashariki.
  • Mkoa wa Mwanza unapakana na mbuga kuu ya Wanyama ya Serengeti. Kwa mtalii kutokea Mwanza atasafiri safari fupi kufika Serengeti kuliko aliyeshukia KIA au JNIA. Kuna mbuga zingine kama Rubondo na Kisiwa cha Saanane.
  • Wilaya za Mwanza zipo karibukaribu sana. Unaweza kupanda daladala moja na ukapita wilaya 4 za mkoa. Mfano daladala za KISESA-NYASHISHI unapita wilaya za Magu, Ilemela, Nyamagana na Misungwi. Hizo ni daladala za mjini. Ukaribu huu wa wilaya unaifanya Mwanza ivutie kwa uwekezaji sababu watu wanapatikana wengi katika sehemu ndogo ya eneo.
  • Mwanza ni jiji la miamba, miamba hii inaweza kuwa fursa kwa watalii kuja kujionea jinsi mawe yalivyobebana. Kule Ukerewe kuna jiwe huwa linacheza, ni utalii tosha kwa mkoa huu.
Pamoja na fursa zilizoorodheshwa hapo juu, bado kuna changamoto za kimiundombinu katika mkoa huu wa Mwanza. Nitataja baadhi tu.
  • Uwanja wa Ndege hauna hadhi.
Uwanja wa ndege ni kero kubwa kwa sasa. Uwanja hauna hadhi ya ukubwa wa mji wa pili kwa ukubwa Tanzania. Huu uwanja upoupo tu, ni kama sio uwanja mkuu wa mkoa ambao pato lake linachangia taifa kwa nafasi ya pili. Majengo yaliyopo yanatia kinyaa hayatamaniki hata kuyaona. Jengo la abiria linajengwa nalo limekwama kwa muda sasa, haliendelei miaka nenda rudi lipolipo tu
Wafanyabiashara wengi wa viwanda vya Samaki na nyama ya ng’ombe na bidhaa zingine zinazosafirishwa nje ya nchi inawabidi wasafirishe bidhaa zao mpaka Dar es Salaam ambapo inachukua muda mrefu mpaka mzigo kuufikisha na kuusafirisha. Wenadai kuwa ubora wa bidhaa zao unaharibika sababu ya kukaa njiani muda mrefu. Kama uwanja wa kimataifa ungekuwepo basi bidhaa ingeweza kutengenezwa (processed) siku hiyohiyo na kusafirishwa siku hiyohiyo bila kupoteza ubora wake.
Ni aibu sana mkoa wa pili kwa ukubwa hauna uwanja wa ndege wa Kimataifa. Mkoa unakosa fursa ya kupokea wageni wa moja kwa moja kutoka nchi za nje. Uwepo wa uwanja wa kimataifa ungeimarisha utalii wa mkoa na kanda ya ziwa kwa ujumla. Kuna usemi mtaani kwamba uwanja wa ndege unahujumiwa na kucheleshwa kwa makusudi kwa hofu ya kupunguza wasafiri katika baadhi ya viwanja vya kimataifa nchini. Sina uhakika kama ni kweli, lakini wahenga walisema lisemwalo lipo.

  • Barabara mbovu
Nafikiri kwa majiji Tanzania, Mwanza ndiyo jiji lenye barabara mbaya kuliko zote. Hata baadhi ya Manispaa zina barabara nzuri kuliko jiji la Mwanza.
Barabara ya Mwanza-Shinyanga (Kenyatta Road) ni mbaya sana. Ni aibu barabara kama hii kuwa ndani ya jiji. Barabara ni nyembamba mvua ikinyesha pembeni inaliwa na maji, barabara ina mashimo mengi sana katikati. Ni barabara ambayo kila mgeni anayeingia Mwanza lazima apite hapo.
Ni aibu sana kwa mtu anayeingia Mwanza kwa mara ya kwanza aone barabara ya namna hiyo halafu umwambie Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania.
Barabara hii inatakiwa ijengwe njia nne au sita ili baadae isije sumbua na kuongeza gharama za kulipa fidia. Ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi (JPM Bridge) utaongeza jam kwenye barabara hii, hivyo bora ikajengwa njia sita mpaka Usagara, halafu ikajengwa njia nne mpaka Misungwi. Serikali isijifanye haioni huo uozo wa barabara hii, hata hivyo Mkoa haupewi hadhi yake ya kuwa mkoa namba mbili Tanzania. Pia barabara ya Kigongo (JPM Bridge) Kwenda Kisesa ijengwe njia nne.
Barabara nyingine ni barabara ya Mwanza-Musoma (Nyerere Road). Hii barabara angalau inajitahidi, ina njia tatu lakini nayo imezidiwa inahitaji kupanuliwa kuwa njia sita kama itakuwa ngumu basi ijengwe njia nne mpaka Nyanguge. Kuna barabara za kimkakati ambazo zinatakiwa zijengwe haraka iwezekanavyo Kwa mfano barabara ya Airport-Kisesa kupitia Kayenze. Barabara hii ikikamilika italeta fursa kwa wilaya za Ilemela na Magu na kuokoa muda. Mgeni akishuka Airport kama anakwenda uelekeo wa Musoma, hii barabara itakuwa shortcut nzuri kwake.
Pamoja na hayo kuna barabara nyingi za mitaa ambazo zinatakiwa kujengwa na kuboreshwa katika jiji la Mwanza. Baadhi yake ni Buhongwa-Igoma, Buswelu-Nyamhongolo, Buswelu-Coca-cola, Mkuyuni-Nyakato nk.

  • Maji ni Shida
Mwanza bado kuna kero ya maji sehemu mbalimbali za jiji. Mfano kata ya Buswelu maji yamekuwa adimu kama dhahabu. Maji yanaweza kutoka mara moja kwa wiki tena usiku wa manane. Tuna mabomba lakini yamekuwa kama mapambo hayatoi maji kabisa. Haya mambo yote yanatia aibu jiji letu la Mwanza.

  • Ucheleweshwaji wa miradi katika jiji la Mwanza
Kuna ucheleweshwaji mwingi sana wa miradi ya Mwanza. Miradi kama Soko Kuu, Stendi ya Nyegezi na Jengo la abiria la uwanja wa ndege, hii miradi imekuwa ikisuasua sana haieleweki inaisha lini. Viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ya uongo za tarehe za kufunguliwa au kukamilika miradi hii hasa stendi ya Nyegezi ahadi zimekuwa nyingi mpaka imekuwa kero. Kila mmoja anaahidi kivyake tarehe ya kufunguliwa stendi lakini muda ukifika hakuna kinachotekelezeka na ujenzi unakuwa bado unaendelea.
Kwenye miradi mingine wanajitahidi hasa ule wa Daraja la JPM na Meli kasi inaridhisha, tatizo huwa mradi ukifika asilimia kuanzia 80 spidi huwa inapungua sana na mingine kusimama.

Hitimisho
Kwa changamoto hizo hapo juu yaani Uwanja wa ndege, Barabara na Maji zinatia doa, na aibu kwa nchi, serikali na viongozi kwa kutokujali mkoa ambao ni mkubwa namba mbili hapa nchini.
Nina imani nawe Raisi wetu mama Samia Suluhu Hassani, una nafasi kubwa ya kubadilisha mkoa huu na kuwa mji wa kisasa na mfano kwa kanda ya Africa Mashariki.

Kwa nafasi yako uliyonayo kama Raisi wa JMT unayonafasi ya kuandika historia Kwa kufanikisha maono haya kwa vitendo ambayo yamekuwa yakisemwa na watangulizi mbalimbali waliopita kwamba wanataka kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara Africa Mashariki. Na unaweza kufanya hivyo ukaacha alama yako kwa wana Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla.

Pia mama yetu Raisi wa JMT nina ombi la nyongeza, nikuombe kitu kingine ila hakikuwa kwenye andiko langu, wana Mwanza tunaomba utujengee chuo kikuu yaani UNIVERSITY OF MWANZA. Tutafurahi kuona Mwanza inapata chuo kikuu chini ya Utawala wako. Ni mkoa mkubwa kihistoria na kiuzalishaji. Hakika hilo likifanikiwa utakuwa umeweka alama ambayo itakumbukwa sasa na vizazi vijavyo.

Nikutakie majukumu mema katika kulijenga taifa letu la Tanzania.

Wako,

Mwananchi
Jiongezeni watu wa Mwanza kwa taarifa yenu Magufuli alishakufa tangu mwaka juzi!
 
Pia wasukuma wanapenda sana kuiga mambo. Jambo likitokea Dar lazima wao waige.

Mfano.
1. Kina Masanja walipoanzisha Ze Comedy Show na wao wakaja na Futuhi

2. Wakiona wasanii wamevaa mavazi ya kisanii yale ya kung'aang'aa basi watauza hata ng'ombe ili wakanunue, ndio maana nguo za dukani za ajabu ajabu zinauzika sana Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. Hii imefanya wasukuma kuwa na uvaaji mbovu kuliko kabila lolote nchini.
 
Pamoja na kuwa wachapakazi lakini uchapakazi wao huendana na uharibifu wa mazingira. Wanatumia loophole ya ulegevu wa sheria kuvamia mapori na kukata miti kwa ajili ya kuni, mkaa na mashamba. Mwisho wa siku wanasababisha mabadiliko hasi ya tabia nchi hali inayopelekea ukame sehemu nyingi.
 
Kwa ujumla katika watu wenye miili mikubwa ila akili kisoda mojawapo ni wasukuma, nguvu nyingi akili kidogo. Wao hawaamini sayansi zaidi ya uchawi na ushirikina.
 
Pia wasukuma wanazaliana ovyo bila kuangalia resources kama zinatosha au la. Unaweza leo kukuta msukuma ana ng'ombe mmoja na mke mmoja ila baada ya miaka mitano unakuta yeye ana watoto 9 lakini yule ng'ombe wake ana watoto 6. Yaani anashindana na ng'ombe kuzaa.
 
Miaka mitano watoto 9

Khaaa hizo mimba zinatungwa na kukomaa na kuzaa ndani ya mwezi mmoja ama

Sent from my SM-N950U using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kuwa wachapakazi lakini uchapakazi wao huendana na uharibifu wa mazingira. Wanatumia loophole ya ulegevu wa sheria kuvamia mapori na kukata miti kwa ajili ya kuni, mkaa na mashamba. Mwisho wa siku wanasababisha mabadiliko hasi ya tabia nchi hali inayopelekea ukame sehemu nyingi.
Kwani hicho kichwa Cha habari kimezungumzia kabila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom