Namba ya Simu ya Zitto katika TAMKO kuhusu kesi ya Lwakatare

Status
Not open for further replies.
Hili swala la Rwekatare linavyoendelea, kuna dalili zile za ndege mjanja kunaswa katika tundu bovu. Kutunishia mishipa namba yake ya simu ambayo labda katika masuala ya uchunguzi imeonekana kuhusika na yeye asema hajaitumia kwa muda kadhaa, kwa nini asiache uchunguzi ufanywe ili kubaini ukweli? Zitto anahofia nini kama namba hiyo haijatumika?

Bungeni Zitto hakuonyesha jitihada zo zote kutetea suala hilo, ni pale alipomwandikia tu Katibu Mkuu barua ya kuaka Rwekatare aachishwe ili kupisha uchunguzi.
 
Hili ni jukwaa la siasa sio la dini Zitto anasema 'asichaguliwe wala kufuatwa kwa sababu ya dini yake' haya ni mambo ya kina slaa tuwaachie tabia zao wenyewe chafu.

Sasa Pro - CCM mmekuwaje watetezi wa ZITTO?
 
Siku za mwizi arobaini sasa arrogance yake itamsaidia ataicha hali kwa public consumption
 
Zitto ulikuwa bega kwa bega na masalia au PM3 wamekisumbua chama na hata dakika za mwisho walipogundulika hapa JF hukustuka bali ukaonekana nao hata kwenye matamasha yako na mapicha yenu studio. Unafikiri nani atakuamini tena kakangu?

Unahisi unachukiwa lakini ni wewe ndio unajipaka kinyesi maana vijana hawahawa waliokuona wewe ndio role model wao leo wanakutukana wala si kwa kufundishwa kama mlivyowafundisha masalia kumtukana Dr. Slaa.

Hivi Zitto mpaka sasa unamfikia kitu Dr. Slaa? Umri, Elimu, ukomavu katika ni siasa na uongozi kwa ujumla? Inakuwaje sababu ya tamaa yako ndogo ushirikiane na wale katuni kumtukana unaona kabisa wanamtukana kiongozi wako mkubwa wako alafu unaandamana nao, leo hii unahisi kuna mwenye busara atakupenda Zitto?
 
Last edited by a moderator:
Baadae sana i cant buy your story...........Ukitembea na uwaridi(Rose Flower) lazima unukie,Msacky ni Gaidi,Kuna msemo wazungu wanasema "show me your friends the i'll tell what type of person you are"mie natumia Formula ya Pasco wa JF if X=Y,Y=Z then X=Z
 
Last edited by a moderator:
yuSidhani kama hii account ni ya Zitto.JF naomba tafadhali mtuwekee ulinzi kwenye account zetu.

Haiwezekani mtu afoji account ya kiongozi wa chama cha siasa ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu,Naibu Katibu Mkuu,Naibu Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni,Mjumbe wa sekretarieti wa chama kikuu cha upinzani na sisi tupo tu

Ikumbukwe mheshimiwa Zitto alijitolea tu kuwa humu JF na si lazima.

Mbona viongozi wengi CCM.hawapo kwa majina yao?

Suala la kumuona Msacky victim basi tatizo kubwa

Ushakunywa viloba unamtafuta Zitto umdedishe kwa sumu, najuta sijui kwanini mtela alikurudishia ile sumu.
 
Mbona wewe na watu wengine wa dini yako hampigi kelele USTAADHI ILUNGA akamatwe?!!

dini yangu ipi? Nyie wachaga mna matatizo sana ndio mana mtei alisema tume ya katiba ina waislam wengi, ndio mana hamumpendi zitto kwa sababu ni mwislam, ndio mana hamumpendi shibuda kwa sababu hatoki kaskazini
 
unaandika kama huna akili....ile video inamuonyesha nani akipanga mauwaji na mateso....kwa hiyo kwenu msaki si kitu ndio mana mnaona auwawe? Zitto hana lake chadema anajilazimishia tu, namshangaa kweli

Nyinyi mnaakili saana. Makanisa yakichomwa moto safi, mapadri wakiuawa kwa maagizo ya ustaadhi ILUNGA bila kukamatwa na DOLA poa!
 
  • Thanks
Reactions: JGG
ZittoKabwe1.jpg

Zitto Kabwe Mbunge na
Makamu Katibu Mkuu Chadema

Hatua ya Zitto Kabwe kuweka mada hapa JF kulalamikia namba yake ya simu kuingizwa katika orodha ya simu ambazo jopo la wanasheria linataka kupeleka ombi mahakamani kufanyiwa uchunguzi wa kumbukumbu za mawasiliano katika kesi inayomkabili Rwekatare kufanya ujasusi haina msingi. Vinginevyo kuna kitu ambacho anahofia katika suala hili, si rahisi kuchomekwa tu bila utafiti wa kina ambao umefikia jopo la wanasheria wa Chadema kuomba kibali cha namba hizo kama ilivyotangazwa.

Utetezi wa Zitto kabwe haujajenga hoja ya msingi wala maana kamili ya kulinda namba hiyo kama kiongozi wa Chadema kitaifa, hali kadhalika kama ana uchungu wa kweli na chama chake, vinginevyo inajengeka dhana ya tafsiri nzito kwamba simu hiyo imetumika katika tukio hilo. Kama alimpa mtu mwingine kutumia namba hiyo aeleze, lakini anavyokazania kupeleka pingamizi mahakamani namba hiyo isichunguzwe kuna kiza kinene kwa Zitto Kabwe.

Tukumbuke kwamba katika maelezo ya Marando, amejipambanua kwamba yeye amesomea kazi ya ushushushu na hivyo kila anachokusudia kukifanya ameshakuwa na dukuduku na kinachoendelea na pengine moja ya simu hizo ni kile kirusi alichokisema Zitto mwenyewe kwamba kipo ndani ya Chadema.

Kwa nini wasimgeweka namba za Slaa na Mbowe kama wana shida na hilo?
 
unaandika kama huna akili....ile video inamuonyesha nani akipanga mauwaji na mateso....kwa hiyo kwenu msaki si kitu ndio mana mnaona auwawe? Zitto hana lake chadema anajilazimishia tu, namshangaa kweli
Zitto ni kama punching bag ndani ya chadema, wanamdunda mangumi kila kukicha lakini anawavumilia sana .
Lakini tukumbuke kuwa kila binadamu ana limit yake ya uvumilivu na iko siku ataamua kuondoka na ndio watakapojua umuhimu wake
 
Sasa Pro - CCM mmekuwaje watetezi wa ZITTO?

Tumevua gwanda tukavaa gamba baada ya ubabaishaji ndanimwe.
Ila still tumekunywa supu ya maagano na zito hakuna wa kumtoa moyoni mwetu haka akifa/kuuliwa kesho simply for what he did for Tanzanian's.
 
Mh. Zitto Sidhani kama uko sahihi kujaribu kumtetea Msacky, Hata kama angekuwa mzazi wako au kaka yako, sembuse rafiki yako tena wewe unakaa Kigoma yeye Dar kufahamu mambo yake yote?? Kibaya zaidi yanayohusu chama chako, mathalani kama msacky anajua unaipenda CHADEMA ile mbaya na ulishawahi kumuambia kuwa ndani ya CDM unapigwa vita, akaamua kutengeneza mapango w akuibomoa CHADEMA kupitia hiyo siri uliyomuambia ya kuwa unapigwa vita, unadhani atakuambia kwa vile wewe ni rafiki yake?? PIA umeshasema ulishaacha kutumia hiyo namba mwaka jana mwezi wa sita, sasa inawezekana kabisa kampuni ya simu kumgawia mtu mwingine namba hiyo baada ya muda wa kukaa idle kuwa mrefu. Zitto hiyo namba sio yako kwa sasa kwa vile inatumiwa na mtu mwingine na wewe ulishaacha kuitumia, ningekuelewa kama namba yako ambayo iko hewani sasa na unaitumia ingekuwa ndio imetajwa.
Kwenye hili suala Zitto kajichanganya, ametumia akili nyingi zaid ya ilivyotakiwa. Hapa ameabuse brain yake. Alitakiwa either aassume kuwa ni error, awasiliane na marando ili amueleze amearrive vipi hadi kuiweka ile namba pale kwenye tamko. Usikute ni information from vodacom na back up ipo, sasa hapo hata ukibisha had asbuh itakusaidia nn wakat info imetoka kwenye horsemouth???

Yeye Zitto ana kifaa gani kinachomfanya adetect kama hiyo namba inakuwaga hewani au lah???Kwani namba ikiwa inatumika ni lazma iwe on muda wote???? Inashindikana nn mtu kuiweka kwenye simu pale anapoitumia tu na akimaliza anaitoa????Hili unawezaje kubisha???Kwan ukiacha kuitumia namba yako unawakataza voda wasimpe mtu mwingine hadi uweke maapizo kuwa haitumiki tena au haijawah kutumika toka uiache???

If i were you, kesho ningeanzana na voda kujua last time hiyo namba imewasiliana lini. Kama ni muda ule ule toka ulipoiacha. Basi unatulia zako tulliii as long as unajua ww sio mhusika. Ila km ilitumika recently basi omba kumjua anayetumia then ukisha mjua utaconnect dots na kilichoandikwa kwenye Tamko, kama hakiusiani basi ndo uje utueleze kitu, kwa kujitokeza sasa hvi bila any fact ni tatizo inawezekana kabisa hiyo namba anaitumia Zoka.
 
Kwa nini wasimgeweka namba za Slaa na Mbowe kama wana shida na hilo?

Katika uchunguzi hizo namba za simu zingeonekana zimetumika sina shaka zingewekwa. Lakini shida nini kwa Zitto wakati namba hizo zinajulikana zimetumiwa na Zoka badala ya yeye Zitto. Vinginevyo anatumia majina kadhaa katika shughuli zake kwani Zitto wengi twamfahamu ni TISS. Huenda alimpa bosi wake aitumie, au bosi wake alimpa Zitto atumie simu hiyo kikazi kwama mwanamtandao wa ushushushu.
 
Hii thread sasa imekuwa vurugu tupu.

Watu badala ya kujadili sababu za namba ya Zitto kuwekwa kwenye kesi ya ugaidi wanajadili historia za kutungwa.

Badala ya kujadili kwanini tamko la chadema litolewe bila kumhusisha kiongozi wa juu mnajadili chuki binafsi.

Tumanini Makene ndiye anyetakiwa kutoa majibu kwa niaba ya chadema...
 
dini yangu ipi? Nyie wachaga mna matatizo sana ndio mana mtei alisema tume ya katiba ina waislam wengi, ndio mana hamumpendi zitto kwa sababu ni mwislam, ndio mana hamumpendi shibuda kwa sababu hatoki kaskazini

Hata DINI yako nikutajie USTADHI? Kwa hiyo mnampenda zitto kwa sababu ni mwislam.. Ndiyo maana mnatoka CUF kwenda kumsapoti mwislamu mwenzenu JK KULE ccm na ZITTO kule CDM!!!.. UAMUZI MZURI!!

Hivi shinyanga ni kusini?
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Namba hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012.

Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye business card yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

Zitto, wakati mwingne unakuwa hueleweki kwa sababu kama hizi. Wewe kama Naibu Katibu Mkuu lipi lingekuwa rahisi na sawa kwako? Si kwamba ulipaswa haraka kuwasiliana na alotoa tamko ili arekebishe hapo kama kuna makosa? Unapohoji motive uelewekeje? Wewe ni wa kulia jf na tamko toka ndani ya chama chako. Ningekuwa mwenyekiti ningeshakufukuza siku nying. LIWALO NA LIWE
 
Last edited by a moderator:
Hii thread sasa imekuwa vurugu tupu.

Watu badala ya kujadili sababu za namba ya Zitto kuwekwa kwenye kesi ya ugaidi wanajadili historia za kutungwa.

Badala ya kujadili kwanini tamko la chadema litolewe bila kumhusisha kiongozi wa juu mnajadili chuki binafsi.

Tumanini Makene ndiye anyetakiwa kutoa majibu kwa niaba ya chadema...

Kwa
hiyo mnatetea zitto kwa sababu ni mwislam?.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Namba hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012.

Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye business card yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.

Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu.

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.

Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.

Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.

Ili kutenda haki naomba Zito athibitishe huu ujumbe ni wake na Mods tuthibitishieni kuwa hakuna mtu ametumia account ya Zito kabla hatujatoa michango yetu.
 
Halafu wewe Froida ulisema unaenda kulala, lakini naona hata kulala umeahirisha ili tu uharibu mjadala uliokusudiwa.

Haifai namna hiyo...
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: JGG
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom