Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 134
Udereva si tatizo, e ndugu yangu sikia
Fungua na masikio, hoja hujaipatia
Sio waja mbio mbio, dereva wanidhania
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu
Mabovu wayatetea, njiani kusafiria
vipi tatuelezea, safari kikudodea
Ni mabaya mazoea, vundo kuukodolea
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu
sindano mwana wa ganzi
Yakuonea wataka ligi,na kikombe kuchua.
Sio kama siiwezi,hilo kaa ukijua.
Nataka kui maizi,kindaki ndaki kujua.
Sasa nakupa mji,hoja kunifumbilia.