Najuta kulipandia........

Yakuonea

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
601
276
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari hili lavutia, kwa hilo nakubalia
Rangi yake kahawia, machoni imetulia
Wengi wanaliwazia, na sifa kulisifia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kilitazama kwa mbele, pembeni limetanuka
Utapatwa na vipele, mwilini kusisimka
Natetemekwa vidole, nikipanda sita shuka
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kwa nyuma linapendeza, napenda wake mbinuko
Na mwendo likiongeza, lapepea kama puto
Ni kweli sijalikweza, gari hili moto moto
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Muda nilipo patia, gari hili nilipanda
Tena nikashikilia, katikati nikatanda
Kelele nilisikia, ila gari halikwenda
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari lilikakamaa, lilishindwa nifikisha
Pale nilipo tazama, mafuta linavujisha
Si kama nalisakama, mashineni kulitisha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Nimebaki na majuto, gari limekinaisha
Sina tena ule moto, wa gari kulipaisha
Mwili bado umzito, bora nisinge liwasha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Bora kupanda bajaji, popote wajipitia
Hazina mwingi mtaji, injini ni ndogo pia
Beteri ukisha chaji, wajitambia na njia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

KLORO na SPRINI, mwaonaje hii hoja
SHOSI naye WAKIJIJI, mchango wenu nangoja
MAGULU uko kundini, LIZZY pia tupamoja
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Na wote nisowataja, msiache kuchangia
Nipeni nyingi faraja, hoja sitapuuzia
Safari niloipanga, katu haikutimia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia


Malenga wenu

Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)
 
Gari hii was as good as new, angalia beti ya kwanza

Hilo gari used au brand new?? Natania bana

Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa
 
Hilo gari used au brand new?? Natania bana

Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa

DA, yeye kapanda gari service sio juu yake mydear! Ila pole mkuu gari rejeta, kiyoyozi kina maeneo yake.
 
Ni kweli ukuzingatia mimi sio mmiliki, sasa kwanini nifanye service kwenye gari isiyo yangu

DA, yeye kapanda gari service sio juu yake mydear! Ila pole mkuu gari rejeta, kiyoyozi kina maeneo yake.
 
Mkuu umechukua gari la mwaka 47 lazima lishindwe kukufikisha au ulipewa bure!!!
 
AD please try to be serious at times, mwenzio sikusafirika wewe unasema very nice

hahahahhahahahah lol
daahh haya bwana nilidhani utaniruka
mmhh

haya pole
kwa nini usitafute lingine
au kodisha mmmhh

maana kila mahali hili unalijutia
 
Back
Top Bottom