Najitoa mhanga, najenga Kigamboni liwalo na liwe!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimesubiri miaka 4, walituzuia kujenga nyumba kwenye maeneo/viwanja vyetu ati kuna mradi wa kuiendeleza Kigamboni . Wamepita na kuchukua majina kwa ajili ya tathmini lkn majina yetu wengine hayakutoka. Wakatuambia tupeleke majina na picha lkn bado hakuna kilichofanyika. Ukizingatia si wote ni tunaishi Dar na utendaji mbovu wa watendaji serikalini, kufuatilia kila wakati inakuwa ngumu sana.
Sasa najitoa muhanga, nimeamua kujenga vivyo hivyo, LIWALO NA LIWE, TUTAJUANA SIKU WAKIJA KUTUBOMOLEA NYUMBA ZETU.
 
kigamboni wapi huko kibada ,mjimwema .gezaulole,kibaoni ,ungindoni,mikwambe,where esle we we ni wapi
 
Hela hakuna man, mradi bado! Ila Karibu gizani, umeme ni imbombo inkafu k'mboni, hv nnavoongea washauchkua!
 
Ndugu yangu naomba nikushauri kuwa jenga tena kwa bidii zote,kwani mradi wa ujenzi
wa mji mpya Kigamboni umekufa,Lakini tatizo nani wa kumfunga paka kengele kutangaza
hilo ndiyo hakuna,huko wizarani wanahaha wafanye nini ,kwani waliwasimamisha
wananchi kuendeleza maeneo yao bila kuwalipa na bila idhini yao,sasa mradi unapokufa
na je wakishtakiwa na wananchi inakuwaje!Hali halisi ndiyo hiyo kwa taarifa za ndani ya
wizara ya ardhi,hivyo wananchi wa Kigamboni mkae tayari juu ya hilo.
 
Nimesubiri miaka 4, walituzuia kujenga nyumba kwenye maeneo/viwanja vyetu ati kuna mradi wa kuiendeleza Kigamboni . Wamepita na kuchukua majina kwa ajili ya tathmini lkn majina yetu wengine hayakutoka. Wakatuambia tupeleke majina na picha lkn bado hakuna kilichofanyika. Ukizingatia si wote ni tunaishi Dar na utendaji mbovu wa watendaji serikalini, kufuatilia kila wakati inakuwa ngumu sana.
Sasa najitoa muhanga, nimeamua kujenga vivyo hivyo, LIWALO NA LIWE, TUTAJUANA SIKU WAKIJA KUTUBOMOLEA NYUMBA ZETU.
Mafisadi watakubolea nyumba yako unayotaka kujenga wewe ngojea mpaka Uchaguzi mkuu ujao wa Mwaka 2015 uishe salama ndio unaweza kujenga usijenge sasa hivi mkuu mimi pia nina kiwanja changu huko sijajenga naogopa Mafisadi wasije kubowa kisha usilipwe chochote kile mkuu kuwa makini sana na hii Serikali............. Ibrah
 
Last edited by a moderator:
Tibaijuka amesema mradi wa mji wa KG unaanza mara moja..
source: Mkutano wa CCM Jangwani leo
 
kigamboni wapi huko kibada ,mjimwema .gezaulole,kibaoni ,ungindoni,mikwambe,where esle we we ni wapi

Mjimwema/ Salanga, Mkuu. yaani barabara ndo imenitenganisha na ule mradi wa viwanja elfu ishirini. Kwa hiyo ni jirani kabisa na viwanja vilivyopimwa, wakati wakipima viwanja walimega sehemu ya shamba langu na kupitisha barabara na wakanilipa vizuri tu. Nataka jenga sehemu iliyobakia.
 
Jenga tu mkuu usiogope,mradi ushakufa si umeona wanazidi kuipima kigamboni kwa makazi,we jenga tu mie nipo mikwambe na changanyikeni pia nina kiwanja kibada na toangoma vyote vinne vya kupimwa!!!
 
Mafisadi watakubolea nyumba yako unayotaka kujenga wewe ngojea mpaka Uchaguzi mkuu ujao wa Mwaka 2015 uishe salama ndio unaweza kujenga usijenge sasa hivi mkuu mimi pia nina kiwanja changu huko sijajenga naogopa Mafisadi wasije kubowa kisha usilipwe chochote kile mkuu kuwa makini sana na hii Serikali.............

Nimeamua kujilipua Mkuu, nasikia hata benki sasa wanakopesha kwa wenye hati za viwanja Kigaomboni. Na bado watu wengi wameamua kujenga kwenye mashamba yao.
 
Ni lazima kujenga kigamboni?, utabomolewa nyumba na sheria itakubana. Mahakama ndio utakapokimbilia na wao hawaangalii swala la kuchelewa au kuwahi utekelezaji wa mradi. Kitakachoangaliwa ni kama utaratibu ulifuatwa kukuzuia kujenga na kama ulifuata utaratibu wa sheria kujenga.

Kama umejiridhisha hutavunja sheria, endelea. Vinginevyo, tutakuona unalia bara barani kama wazee wa Africa Mashariki au wale watu wa Kipawa.
 
Hata hivyo viwanja vinavyouzwa na manispaa naogopa kununua
mji wa bush,lazima tahadhari
 
basi nakushauri utafute kiwanja sehemu nyingine.

St. Ivuga, wanaotulazimnisha kutojenga ndio wanatakiwa watupatie viwanja vingine. Kama waliwapa viwanja wakazi wa Jangwani kwa dharura baada ya mafuriko, sisi wanatusubirisha miaka 4 kivipi?
Huu mradi utawatokea puani CCM 2015, hata wachakachue kivipi itawagharimu tu, labda wawategee wana Kigamboni hadi uchaguzi wa 2015 ndio watukurupushe tena.
 
Tibaijuka amesema mradi wa mji wa KG unaanza mara moja..
source: Mkutano wa CCM Jangwani leo

Alikuwa akifanyia marketing CCM, hakujua kama kuna wengi kutoka Kigamboni ambao hawakufurahia hiyo kauli.
Natamani Mbunge wa Kigamboni atake kauli ya Waziri Mkuu wakati wa kikao cha bajeti kuhusu mradi huu.
 
wewe jenga tu, viwanja vyevyewe wakipima wanajigaia wenyewe, mfano hivi viwanja 1800 vya gezaulole si wangewapatia? Lakini utashangaa vyote wanapewa mawaziri na wachache watakaofanikiwa kuoenyeza kitu kidogo....
 
uSIJENGE WANGU SUBIRI UPEPO CZ MWISHO WA CKU HASARA KWAKO..Dnt say i didnt warn u/ u werent warned.
 
Back
Top Bottom