Najiandaa kugombea urais 2030

Wana JF,

Nawasalimu.

Kwa wale mnaokumbuka kwamba nimetangaza nia yangu ya dhati ya kuomba ridhaa ya wananchi ili kuwa rais (mtumishi) wa Tz mwaka 2030. Nashukuru kwa kuwa wengi hasa wa hapa jamvini wameunga mkono nia yangu hiyo na wametoa ushauri makini. Nawashukuru sana.

Ndugu wana JF,
Baadhi ya watu wamehoji kwamba 2030 ni mbali sana na kwa nini nitangaze nia yangu sasa. Jibu langu ni hili hapa.

Kupata kiongozi mzuri si jambo la mzaha na halihitaji kukurupuka. Rais wa kwanza wa TZ hayati JK Nyerere aliwahi kusema 'ikulu ni pa kuogopwa kama ukoma...., pia alisema..kwa mtu msafi kabisa, ikulu sio mahali pa kukimbilia'. Inawezekana alitoa kauli hizi baada ya kuona dhuluma na ukiukaji wa taratibu unaoendelea katika eneo la uongozi katika Tz. Hivyo kama rais mtarajiwa niwezaye kuona ugumu na gharama ya uamuzi nitakaouchukua, lazima nianze mapema kujiandaa ili nitakapoingia ikulu ni pafanye mahali huru ambapo 'ukoma' haupo tena, badala yake ikulu pawe nyumbani pa kila mtanzania na sio pa wachache yaani mafisadi.

Ndugu zangu, nchi ikiwa na viongozi wabovu huendelea kuwa maskini. Mfano, kilichosababisha Mexico iwe maskini ingawa ina rasilimali kadhaa iko karibu eneo moja kijiografia na Marekani (ambayo inahesabika kuwa nchi tajiri duniani) ni tofauti ya kimisingi, mitazamo na mipango ambayo huwa miongoni mwa mambo ya msingi yanayotofautisha 'viongozi kutoka kwa watawala'. Kuna uwezekano mkubwa kiongozi akawa mtawala pia, ila sio kila mtawala huwa kiongozi.

Wana Jf,
Nimetangaza nia yangu hii mapema sio kwa mzaha ili kwa nia ya dhati ambayo nimeamua sio tu kwa sababu ni haki yangu kama raia wa Tz, ila kwa sababu naamini nina uwezo (kwa msaada wa Mungu) wa kujenga Tz yenye watu wazalendo, wanaoheshimiana, wasiodhulumiana, wanaotenda haki, wanaochukia rushwa, wanaopenda kufanya kazi, waliokombolewa kifikra na watakaojivunia utaifa wao usiku na mchana hivyo kulinda heshima ya nchi yao na kutumia rasilimali za nchi yao katika njia endelevu kwa manufaa ya nchi vizazi hata vizazi. Kazi hii sio lelemama, inahitaji vitendo badala ya maneno matupu ambayo wahenga wanasema 'hayavunji mfupa'. Kazi hii pia inahitaji mtu msafi aliyeanza kufahamu jambo hilo kabla ya kunajisika ili ajijenge katika usafi huo na hatimaye atumie usafi wake huo kurekebisha na kuondoa uchafu ndani na kwenye kingo za uongozi nchini TZ.

Wana JF,

Leo naishia hapa, maoni yenu yana thamani kubwa sana, karibuni kwa maoni zaidi.
 
Kaka utatumia CHAMA au MGOMBEA Binafsi?
nakushahuri Utumia Mgombea Binafsi hope katiba mpya itaruhusu hilo kwani vyama kwa sasa ni Majungu na kuchafuana kwingi!

Pia kumbuka kuanza na Srekali ya MTAA MTAANI KWAKO 2013,
Udiwani kwenye KATA yako 2015,
Ubunge kwenye Jimbo lako 2020,
Then miaka 10 ya ubunge yani 2020 mpaka 2030 inatosha kabisa watanzania kukutambua wewe ni nani!
 
Kaka utatumia CHAMA au MGOMBEA Binafsi?
nakushahuri Utumia Mgombea Binafsi hope katiba mpya itaruhusu hilo kwani vyama kwa sasa ni Majungu na kuchafuana kwingi!

Pia kumbuka kuanza na Srekali ya MTAA MTAANI KWAKO 2013,
Udiwani kwenye KATA yako 2015,
Ubunge kwenye Jimbo lako 2020,
Then miaka 10 ya ubunge yani 2020 mpaka 2030 inatosha kabisa watanzania kukutambua wewe ni nani!

Itategemea katiba mpya itakavyokuwa kama ulivyosema
 
mbona mimi pia nina nia hiyo? okay kazi itakuwa ngumu kwako aise,ikiwa utatoka chama kimoja nami haahahhaaa hauna chako, na ikiwa chama chako kitakupitisha huko ukutane nami jukwaani pia hauna chako.
democracy iko huru karibu, ila usinichukie.
 
mbona mimi pia nina nia hiyo? okay kazi itakuwa ngumu kwako aise,ikiwa utatoka chama kimoja nami haahahhaaa hauna chako, na ikiwa chama chako kitakupitisha huko ukutane nami jukwaani pia hauna chako.
democracy iko huru karibu, ila usinichukie.

Tumia haki yako kikatiba, karibu uwanjani, watz wataamua
 
Wait a minute: Unataka Urais wa Tz mwaka 2030 wakati tunataka kuvunja muungano na kubaki na Tanganyika kabla ya 2015, I am afraid you need to start laying a proper philosophical stand concerning this Union, as for us Tanganyikan new generation you are either for us or against us!!!
 
Wait a minute: Unataka Urais wa Tz mwaka 2030 wakati tunataka kuvunja muungano na kubaki na Tanganyika kabla ya 2015, I am afraid you need to start laying a proper philosophical stand concerning this Union, as for us Tanganyikan new generation you are either for us or against us!!!

Usihofu, hilo halibadili nia yangu ya kuwatumikia watu wangu hata kama jina la nchi lingebadilika.
 
Salamuni wanaJf,

Kama rais mtaraji wa Tz (2030), natanguliza pole kwa watz wote kwa vifo vya wapendwa wetu mabalimbali vinavyotokana na ujinga, umaskini na maradhi. Naumia sana moyoni mwangu ninapoona nchi yangu inaharibiwa mbele ya macho yangu.

Naangalia kwa undani sana jinsi ya kuondoa utando wa kutojiamini akilini kwa watz, hasa wale wailoenda shule. Utando wa kutojiamini umewafanya watz wengi kunung'unika na kufikiri kazi ya kuleta mabadiliko sio yao ila ni ya viongozi wa jamii.

Sikatai, viongozi wanatakiwa wawe sehemu ya usimamiaji wa maono ya taifa. Lakini labda tujiulize swali hili la kawaida sana ambalo kwa hali halisi pengine haliwezekani.

Je kama kila mtz angekuwa kama wewe, nchi yetu ingekuwaje? Kwa maana nyingine tunaponung'unikia ubovu wa utawala, mmomonyoko wa maadili, udhaifu katika michezo, ubabe wa dola, ufisadi, ubinafsi, zinaa, uongo, uvivu, tamaa ya uongozi, ubabaishaji, ugandamizaji, ubaguzi, uchochezi, unafiki, uchakachuaji, uropokaji, nk; wajibu wako ni upi katika kukomesha au kukataa hali hizo?


Mimi kama rais mtaraji wa 2030, nimejipanga sawa sawa. Sio tu kwamba nayatamka mambo hayo, au kuyachukia, au kunung'unika, bali nachukua hatua ya kuanza kujijenga kimaadili na kimtazamo ili hayo niliyotaja yasionekane hata kwa harufu maishani mwangu.

Tanzania mpya, huru, ya amani na baraka imezaliwa. Mimi nimeanza kutekeleza uzalendo kwa kujiahidi kwamba nitakuwa muadilifu mbele zangu mwenyewe, jamii yetu na mbele za Mungu.

Kama wewe unania kama yangu, karibu tuahidi pamoja, na kama ulikuwa bado hujafikiri hivyo fahamu leo ndio siku ya kujiwekea ahadi hiyo ya uaminifu na kuitekeleza. Tukifanya hivyo, mwaka 2030, tutakuwa na watu wasiopungua milioni 10 kati ya milioni 60 (kadirio la idadi ya watz mwaka 2030) waadilifu kwelikweli (kama wewe utafanikiwa kumuelimisha ingawa mtu mmoja kwa mwaka na mwisho wa mwaka wewe na uliyemwelimisha kila momoja atamwelimisha mwingine...nk.

Na kama nusu ya ya watu watakaoelimishwa watajitwika uadilifu). Miongoni mwa watu hawa nitaunda baraza la mawaziri wasiozidi kumi na tano.

Baraza hili likiwa la kizalendo na lenye sifa njema basi ndipo tutashuhudia mambo mengi na sio ajabu wakati huo kuanzisha mipango ya jinsi ya kutengeneza mitambo, mashine mbalimbali, vipelezi vya angani (satelite), utafiti hadi wa kwenda mwezini (lakini yote yatalenga ukombozi wa fikira na utatuzi wa matatizo ya mtz kwanza), nk.

Tunaweza kuifanya tz yetu ikawa nchi inayojiongoza kwa haki na inayoongozwa na utashi mkuu wa kisayansi na tukapita hata mataifa mengi duniani. Maisha ya watu wetu yataboreka, uvivu hautakuwepo, na tutakuwa tumeushinda ujinga, umaskini na maradhi ya akili miongoni mwa watz.


Rasilimali tunazo, watu tunao, uwezo tunao, lazima tujiamini, tutaweza. Niko pamoja nanyi kwa Tanzania yenye baraka. Sina mashaka na nia yangu wala utashi Mungu alioonijalia.

Mungu ibariki nchi yetu.
 
Sasa wewe unazungumzia uvivu gani? Nani mvivu nchi hii? Watu wanafanya kazi kwa kila hali ngumu iliyopo wewe unakuja kuleta habari za uvivu. Ulisha wawezesha watu wangapi na wakashindwa kutokana na uvivu? Acha kutusi watu ni wavivu bana.
 
Ndugu Onambali, sijui ni mimi tu naona ingefaa angalau kuanza kuweka wazi baadhi ya mambo; Mfano hadi sasa pamoja na kwamba umepost mara nyingi, hujaona haja ya kuweka umri wako hapa!! Vinginevyo kila la heri..
 
Ndugu Onambali, sijui ni mimi tu naona ingefaa angalau kuanza kuweka wazi baadhi ya mambo; Mfano hadi sasa pamoja na kwamba umepost mara nyingi, hujaona haja ya kuweka umri wako hapa!! Vinginevyo kila la heri..

Sawa mkuu,

Umri wangu ni miaka 35
 
Back
Top Bottom