Akijibu swali la Mbunge Thea Ntara ambae aliuliza,
"Hili suala sasa hivi linatisha, mabinti wanatumia hizo P2 kama unavyotumia panadol yaani hakuna utaratibu, tutafika wakati mabinti hawa hawataweza kupata watoto, je serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa hao mabinti ili wajue matumizi ya P2 pamoja na hizo 'Energy drink'," - Mbunge Dkt Thea Ntara
Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molle amejibu swali hilo kwa kusema,
"Ni kweli matumizi ovyo ya P2 yanaleta madhara mengi, inasababisha akina mama kupata hedhi ambayo haina mpangilio na wakati mwingine kupata matatizo ya mifupa, sisi wote kwa pamoja tushirikiane kuhamasisha matumizi mazuri ya P2 yanayozingatia ushauri wa kitaalamu," - Naibu Waziri wa Afya
Mollel amesema P2 ni njia ya dharura ya vidonge vya uzazi wa mpango ambayo hutumika kuzuia mimba kwa Mwanamke aliyefanya tendo la kujamiiana bila kinga kwa mfano aliyebakwa au ametumia condom ikapasuka na anadhani anaweza kupata mimba asiyoitarajia wakati Sayana Press ni njia ya kuzuia kupata ujauzito kwa muda mrefu, hivyo matumizi ya kuzuia mimba kwa Sayana Press na P2 ni tofauti.
Nini maoni yako?
#Bungeni
Written by Mjanja M1 ✍️