Naibu Waziri Kagasheki ajibainisha yupo upande Gani wa Gamba ndani ya CCM

Jairo, Jairo, Jairo, Jairo...................... Acheni kumuonea bure baba wa watu: kila alichofanya ni maagizo ya gvt, hata shelukindo alileta nyaraka za wizara kwa maagizo ya serikali ili wapinzani wasipatie umaaru hapo. Tuangalie issues kwa usahihi, mbayawetu ni JK.
 
Maswali yalikuwa haya:-
1. Kwa sasa kuna wimbi la majambazi wanaoua waendesha piki piki na kuwapora pikipki hapa mjini Bukoba, sisi tunawajua na polisi wako wanawajua lakini hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliye chini ya ulinzi wa polisi au kufunguliwa mashitaka mahakamani, je tuendelee kuwashugulikia sisi wenyewe au huko tayari kukaa na Polisi wako na kutuletea orodha yao kesho? Jibu:- Kama mnaona Polisi haifanyi kazi basi tuwape likizo ya saa 24 muone mji utakuwaje kwa muda huo.
2. Sukari kilo moja ni Tshs. 2,200/= na hii ni kutoka kiwanda cha Kagera Sugar, Je kuna uwezekano tukaachana na sukari hii na kutumia sukari ya Uganda? Hivi serikari inatutaka nini kwani ni juzi tu TRA Mpakani Mtukula wamekamata shehena ya sukari ya Uganda na kuitoza kodi kubwa kiasi cha kushindwa kuuzika kwani bei ilienda juu mno, vile vile iweje mkoa mzima awepo AGENTI mmoja, hii sio kwamba tunarudi enzi za kuhitaji AZIMIO LA ARUSHA?. Jibu:- Naenda Dar nitakutana na Bosi wa TRA na nitawaletea jibu.
3. Hivi tunahitaji maendeleo ya mji huu inakuwaji ushuru wa masoko manne makubwa ya mji apewe mtu binafsi na awasilishe mapato ya milioni 12.5 kwa mwaka ambazo ni milioni 1.04 kwa mwezi, laki kwa kila soko kwa mwezi na shilingi 8,680 kwa siku kwa kila soko. Mh. mbona mnatuhuza. Jibu:- Kuna watu hapa wana chuki binafsi na meya wa manispaa Dr. Anatory Amani, wanataka ionekani kama ni mkandamizaji, tafadhali acheni siasa za kupakana matope.
 
This Time 2014 ngoma itakuwa ishachanika tayari

Haya ni matokeo ya kazi nzuri ya CDM
 
amka2.gif

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Khamis Kagasheki, amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushughulikia matatizo yanayowagusa wananchi na si dhana ya kujivua gamba.
Balozi Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini, alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini hapo na kubainisha kwamba viongozi wa chama hicho wanatakiwa kutambua kuwa wananchi wanakabiliwa na matatizo mengi, hivyo ni wakati muafaka kuyashughulikia matatizo ya wananchi kwanza.
Akitoa mfano, mbunge huyo alieleza kusikitishwa kwake na kile kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM kama walivyoonekana katika baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni wakiwa Mbeya ambapo baadhi ya viongozi hao akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alizungumzia mambo mengi, likiwamo la watu kujiondoa kwenye nyadhifa zao ndani ya chama.
“La msingi ni kuangalia wanachama wa CCM na wananchi wa Tanzania ni kitu gani hasa kinawagusa, mbali na masuala ya kujivua gamba, naamini hapa Bukoba mjini matatizo yetu ni maji, sukari, mafuta ya taa, barabara na ugumu wa maisha, ambayo kimsingi hayana uhusiano na kujivua gamba,” alisema Balozi Kagasheki.
Alisema mtu wa Bukoba mjini kimsingi anatakiwa kuangalia matatizo yanayomkabili na si masuala ya magamba, kwa kuwa hayamgusi moja kwa moja mtu ambaye yuko kijijini na ambaye yupo mjini hapo.
Alisema CCM itanufaika zaidi iwapo itapanua wigo wa kujisafisha kuliko kung’ang’ania katika agenda moja ya ufisaidi, jambo ambalo kwa sasa haliwezi likajenga chama.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutowasikiliza wanasiasa watakaofika kwa lengo la kuelezea dhana ya kujivua gamba badala ya kuwasaidia wananchi kukabiliana na matatizo yanayowakabili.
“Hili nalizungumzia kwa uzito wa kipekee, kwa sababu jimbo hili ni jimbo la upinzani, isingekuwa busara kuwa na mapambano ndani ya CCM badala ya kuwa na mapambano na wapinzani ambao na wenyewe wana mikakati yao ya kutaka kupata dola,” alieleza.
Akielezea kuhusu kujiuzulu nafasi zote katika siasa alizokuwa nazo aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, alisema haliwezi kuwa suluhisho la wananchi kuwatatulia matatizo jimboni humo.
“Najua wengi watasema natetea watu ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali lakini nakuwa mkweli, kwa kuzingatia hali halisi ya jimbo langu, kujiuzulu kwa Rostam nataka nifanye utafiti na pia nitoe tathmini nione ni vipi kisiasa kumesaidia katika Jimbo la Bukoba Mjini, narudia Bukoba tupunguze siasa zisizo za maana, tatizo lililopo hapa ni kupambana ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na si vinginevyo,” alisema naibu waziri huyo. Alisema hata kama Rostam amejiuzulu nafasi zake zote na hata kama kutakuwa na viongozi wengine watafanya hivyo, lakini haitaweza kuwasaidia wananchi, lengo ni maendeleo.


 
Back
Top Bottom