Naibu Waziri Kagasheki ajibainisha yupo upande Gani wa Gamba ndani ya CCM

Mutabora

Member
Apr 29, 2010
45
4
Naibu wa mambo ya ndani Khamis Kagasheki amesema CCM haiwezi kujisafisha kwa wananchi kwa kung'ang'ania Chenge na Lowassa kufuata mkondo wa Rostamu Azizi.

Ameyasema hivi punde katika mkutano na wananchi wa Bukoba maeneo ya soko kuu.
 
Kalipwa pesa na hao jamaa ili akawasemee hoko kwao Bukoba. Kwa kifupi Muiran Rostam amekuwa mbuzi wa kafara.
 
Ni Leo hii jioni hapa Bukoba N/Waziri akihutubia wapiga kura wake alipoelezea kuwa hakuna cha GAMBA ccm tatizo ni akina Nape, Sita na wenzao katika kinyang'anyiro cha uraisi wa mwaka 2015. amesema hao watu ni hatari na kuwaomba wapigakura wake wasiwapokee wala kuwakaribisha pale tu wakifika Bukoba. Ametoka Bungeni kwa ajili ya kuwaeleza kuwa jimbo lake haina tatizo na Magamba. Lowasa ni safi na watu wa Bukoba hawatanufaika na lolote kutoka kujihudhuru kwa Rostam. Hivyo hakuna kusikiliza hawa wanaoneza siasa za chuki kwa masilahi binafsi, wazomee wakija.

Hotuba hii ilikuwa mbele ya soko kuu la Bukoba mjini ila alipotoa nafasi ya kuuliza maswali hapo ndo ngoma inogile.
 
andika hayo maswali ili yaliyoulizwa ili tujue kama bukoba kuna watu wenye akiri
 
Naibu waziri wa mambo ya ndani,Khamis Kagasheki ameibua mzozo mpya baada ya kudai kuwa matatizo ndani ya CCM yanatokana na Katibu wa itikadi nna uenezi Nape nauye pamoja na waziri wa afrika mashariki Samweli sitta wanao jiandaa kwa mbio za uraisi 2015,Kagasheki alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara ulio fanyika kwenye soko kuu la bukoba.
 
"Mimi kwa upande wangu naona kuwa matatizo ya ccm kwa sasa ni sitta na nape ambao wamejipanga kwa ajili ya mbio za uraisi alisema kagasheki"Wameenda mbeya badala ya kueleza jinsi ya kutatua matatizo ya wananchi wamebaki kwenye falsafa ya gamba ambayo binafsi sijui maana yake nini.Waziri huyo ambaye ni mbunge wa bukoba mjini alienda mbali zaidi kwa kuwataka nape na sitta kutofika bukoba mjini na kuwapotosha wananchi wa jimbo hilo kwa hoja zenye lengo za kuibua migogoro zaidi.CCM ya bukoba ni yangu kwani nilipoaanza harakati za kuwania jimbo hilo 2003 ccm ilikuwa hoi hapa na ndio maana jimbo lilikuwa la upinzani.Leo watakuja kuwaambia nini wananchi wa hapa,alihoji kagasheki.
 
CCM iwaruhusu watu wenye NIA ya kugombea Urais 2015 watangaze NIA zao hizo sasa. Tunataka Watanzania tupate muda wa kutosha kuwachambua. Tayari makundi mawili yako wazi. Lile la Sitta na lile la Lowassa makundi ambayo kwa maoni yangu hayana mtu anayestahili hata kuchukua fomu ya kugombea urais wa nchi hii.
 
Taratibu tutaanza kuwatambua waliopo kwenye kambi ya El na waliopo kwenye kambi ya akina 6. Mwisho tutawatambua waliopo kwenye kambi ya JK. Comedy itakuwa tamu pale atakapoibuka Katibu mkuu akatangazia umma kwamba chama hakina makundi wala mgawanyiko wowote. Kisha hao wagombea watajitokeza na kuanza kuchafuana. Mtoa rushwa mzuri na mwenye mtandao mkubwa atashinda kisha atatangazwa mgombea akiwa ameshachafuliwa sana na wenzie. Kama atagombea na Dr Slaa, atashindwa na kura hazitawezekana kuchakachua! Ugomvi mkubwa utaibuka kati ya polisi na wananchi, wakurugenzi wa wilaya na wagombea. Mwisho ccm itaanguka na kuwa chama cha upinzani.
Ni mtazamo tu!
 
kalipwa pesa na hao jamaa ili akawasemee hoko kwao bukoba. Kwa kifupi muiran rostam amekuwa mbuzi wa kafara.

naomba utoe hiyo avetar yako haraka, unatutia uchungu saaaaaaaana sisi wanawake na hata wababa, please take it out
 
Natamani sana mnyukano huu ndani ya ccm uendelee kwa manufaa ya ustawi wa nchi yetu.
 
CCM iwaruhusu watu wenye NIA ya kugombea Urais 2015 watangaze NIA zao hizo sasa. Tunataka Watanzania tupate muda wa kutosha kuwachambua. Tayari makundi mawili yako wazi. Lile la Sitta na lile la Lowassa makundi ambayo kwa maoni yangu hayana mtu anayestahili hata kuchukua fomu ya kugombea urais wa nchi hii.
makundi yaliyoonesha nia ni mengi: kundi la wazanzibari(Husen Mwinyi+shein), kundi la vijana(Januari makamba) kundi la wabara(Mr Maige), makundi ni mengi tu na yote yanastahili kuchukua fomu ili ngoma iwe tamu.
 
Kalipwa pesa na hao jamaa ili akawasemee hoko kwao Bukoba. Kwa kifupi Muiran Rostam amekuwa mbuzi wa kafara.

Umemkadiria vibaya. Mh. Kagasheki ana hela iliyo "reserved" vijisenti vya kutosha tena vikiwa katika currency isiyo ya madafu. Si chenge wala EL wanaweza kufika "Bei" ya Mh.
 
Well, how united CCM is, or rather, how this party's solidarity and strength's will hold not to fall apart?
Kagasheki'd better see the bold signs on the wall that magamba's time is over, we need sustainable developments in our constituency - siyo blah blah za kutetea mafisadi.
 
Naibu wa mambo ya ndani Khamis Kagasheki amesema CCM haiwezi kujisafisha kwa wananchi kwa kung'ang'ania Chenge na Lowassa kufuata mkondo wa Rostamu Azizi.

Ameyasema hivi punde katika mkutano na wananchi wa Bukoba maeneo ya soko kuu.

YES haya ndiyo na sisi tumekuwa tukisisitiza. Mfano mdogo tu juzi bungeni lile GAMBA la Jairo je ni kati ya hawa mapacha 3? Kagasheki yupo sahihi kabisa.
 
taratibu tutaanza kuwatambua waliopo kwenye kambi ya el na waliopo kwenye kambi ya akina 6. Mwisho tutawatambua waliopo kwenye kambi ya jk. Comedy itakuwa tamu pale atakapoibuka katibu mkuu akatangazia umma kwamba chama hakina makundi wala mgawanyiko wowote. Kisha hao wagombea watajitokeza na kuanza kuchafuana. Mtoa rushwa mzuri na mwenye mtandao mkubwa atashinda kisha atatangazwa mgombea akiwa ameshachafuliwa sana na wenzie. Kama atagombea na dr slaa, atashindwa na kura hazitawezekana kuchakachua! Ugomvi mkubwa utaibuka kati ya polisi na wananchi, wakurugenzi wa wilaya na wagombea. Mwisho ccm itaanguka na kuwa chama cha upinzani.
Ni mtazamo tu!

asante sana,hivi mritji wa shehe yahya yupo?maana nona unaelekea huko
 
naibu wa mambo ya ndani khamis kagasheki amesema ccm haiwezi kujisafisha kwa wananchi kwa kung'ang'ania chenge na lowassa kufuata mkondo wa rostamu azizi.

Ameyasema hivi punde katika mkutano na wananchi wa bukoba maeneo ya soko kuu.

maswali tupe.....
 
Back
Top Bottom