Naibu Spika afafanua kuhusu Benki na Kampuni za Simu hukata pesa nyingi kuliko Serikali

Mkibadilisha mgawanyo kuna mawili:
1. Bei itabaki pale pale ila ukubwa wa bando utapungua zaidi kufidia gharama, ukumbuke Nape aliwahi kusema wao hawana nguvu ya kudhibiti bei za bando na huo ndio mlango wao wa kutokea.

2. Mitandao isiporidhika wanaweza kuanza kusitisha baadhi ya huduma kama Uber,Bolt walichofanya kwa kisingizio cha gharama za uendeshaji kuwa juu ili kuitia presha serikali warudi katika meza ya mazungumzo.

Vyovyote vile atakayeumia ni mteja wa mwisho, ngoja tuone mchezo utakavyokwenda !
 
Wewe na zungu wako mliwaho kuona wapi mtoa huduma anachukua kidogo au sawa sawa na serikali? Maana mabenk na mitandao ya simu ndio watoa huduma, wanarun systems, wanalipa wafanyakazi, ikitokea hasara kwa mteja wao ndio watailipa sasa inawezekanaje wagawane sawa au serikali ichukue zaidi?

Haya ni mawazo ya ajabu kabisa
Na hayo mawazo yake ya kuweka tozo kwenye mabundle ni mawazo ya ajabu.
Nchi hii inabidi iwahimize watu watumie internet zaidi maana dunia ndiko inahamia huko.

Sasa hivi walau na sisi ndio tunaanza catchup vijana wanajitengenezea kipato huko kwa kuzalisha contents, kufanya biashara wengine kupata maarifa lakini bado pia hatujafika mbali maana hatuna hata startups wala innovations za maana huko.

Kufanya internet ionekane ni anasa na mawazo mufirisi
Toeni tozo mambo yaende,serikali inahitaji pesa
 
  • Biashara ifanye benki, Ila mnufaika wa kwanza awe serikali.
  • Kwa nauli hizi, si rahisi kupata wawekezaji wa maana.
  • Viongozi wapime uzito na madhara ya kauli zao kwenye uwekezaji, usalama wa mitaji, maazimio ya kimataifa na kikanda, n.k
  • Haya maelekezo yanakwenda kuvuruga Biashara, tunarudi zama zile kwa kasi ya 4G.
  • Mh. Samia watch out!
Elimu ya ovyo ndio chanzo Cha yote haya watu wanatamka maneno bila hata kufikiria leo huyu kasema hivi kesho yule kasema vile ili mradi ni vurugu mechi ombwe la uongozi kwa Sasa ni kubwa mno
 
Tatizo la Naibu Spika huwa anaongea vitu ambayo hana tafiti au uelewa navyo.
Nimemsikia mara nyingi ktk upotoshaji mkubwa.
 
Hivi kumbe huyu Zungu ni mjinga kiasi hiki.
  • Kwa nini hagusii kabisa ma V8 wanayoendesha ambayo kila moja gharama yake ni karibia 600,000,000/= kila moja?
  • Kwa nini hagusii kabisa posho (300,000/= kwa siku) wanazolipwa kwa kutimiza wajibu wao kama Wabunge huku wakiendelea kulipwa mishahara ya mamilioni ya kodi zetu?
  • Kwa nini hagusii kabisa swala la wabunge kutolipa kodi licha ya kulipwa hayo mabilioni na mamilioni?
  • Je Zungu anataka kusema hizo kampuni hazilipi kodi?
Wananchi tuamke, tunaibiwa na watu ambao hawana akili wala huruma..hovyo kabisa watu hawa!
Ubinafsi wa wenzetu hawa hawawezi kamwe kuongelea haya Mkuu. Ni mambo ya ajabu kabisa!
 
Hiyo si ni biashara yao, kwani hawawalipi kodi......mnataka kunyonya kwa mrija kwenye biashara za makampuni, kwa kweli viongozi kama hawa wamefilisika akili kabisa.
 
Wewe na zungu wako mliwaho kuona wapi mtoa huduma anachukua kidogo au sawa sawa na serikali? Maana mabenk na mitandao ya simu ndio watoa huduma, wanarun systems, wanalipa wafanyakazi, ikitokea hasara kwa mteja wao ndio watailipa sasa inawezekanaje wagawane sawa au serikali ichukue zaidi?

Haya ni mawazo ya ajabu kabisa
Na hayo mawazo yake ya kuweka tozo kwenye mabundle ni mawazo ya ajabu.
Nchi hii inabidi iwahimize watu watumie internet zaidi maana dunia ndiko inahamia huko.

Sasa hivi walau na sisi ndio tunaanza catchup vijana wanajitengenezea kipato huko kwa kuzalisha contents, kufanya biashara wengine kupata maarifa lakini bado pia hatujafika mbali maana hatuna hata startups wala innovations za maana huko.

Kufanya internet ionekane ni anasa na mawazo mufirisi
Ndio yalele ya label ya WCB msanii anataka apewe share sawa sawa na Mmiliki wa label diamond
 
Hizi akili kweli kila mtu ana zake !!!!

Kwahio wanataka wakate kiasi gani ? (hawana overheads, research and development n.k.) By the way last time I checked hii ni biashara huria..., watumie bank zao zisicharge iwe bure kabisa ushindani na wenyewe watashusha tu !!!!!

Kwanini wasianze na TTCL na Airtel ambazo wanahisa na kutuonyesha hio business model ?, tena hata wakitaka wachukue 100% Tozo....

Bure Kabisa hawa watu wamesahau kwamba wanaowatumikia ndio hao mwisho wa siku wanaumia kwa hizo Tozo (Wazee wa Kuvuna wasipopanda)
 
Back
Top Bottom