Naibiwa gari na agent?

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,498
605
Niliagiza gari kupitia agent wa hapa Dar es Salaam tangu mwezi wa tatu, ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto TRA ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake?
Ananiweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa, km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono
 
Niliagiza gari kupitia agent wa ha pa dar es alaam tangu mwezi wa tametatu ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto tra ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake? Aniweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa.km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono

Muibukie ofisini.mguu wako mguu wake mpaka tra we huilon ni uongo huo maana navofaham.mm mzigo ukiendelea kukaa bandarini unalipiwa zaidi
 
Manfirst inapatikana siku1 au 2 kabla meli haijafika, anakwambia manifist au deliverd order(DO)

Lazima itakua (DO)In any case inaweza kuwa kweli.

Agent hawezi kuiba gari

halafu mtu unaagiza gari kupitia ku clearing agent? Au huyo ni Agent wa kuagiza magari na clearing at the same time?
 
BTW kuna ma agent wahuni,jitahidi kutafuta agent mwenye historia nzuri.
Hakikisha unapata taarifa zake kutoka kwa watu unao waamini sana.
 
Clearing agent ndio anaweza kukuibia gari maana process zote anafanya yeye na release order anapewa yeye na funguo anakabidhiwa yeye cha msingi angalia gari yako imepelekwa wapi? Kama ipo Farion mchicha mtafute ben atakusaidia kwa maelezo zaidi ni PM.
~ ukishathibitisha kama kaipiga ilipoti hyo kampuni ya huyo agent then wanaisuspend mpaka walipe fine ndio wataiachia ifanye kazi na kila kampuni ina mtu m1 tu ambaye amepewa authority ya kutoa gari yard ila kulog docs any1 can log.
 
Niliagiza gari kupitia agent wa ha pa dar es alaam tangu mwezi wa tametatu ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto tra ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake? Aniweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa.km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono

Kwani makubaliano yenu yalikuaje?

Kama yeye ndio anaagiza kwa jina lake halafu ikija ndiyo akuuzie hapo kunaweza kuwa na tatizo la kutrace.

Kama ameagiza kwa jina lako basi katika hatua hii atakua ana shipping documents tayari. Akikupa nakala kama yeye ndio analitoa bandarini, ni rahisi kufuatilia mwenendo wake huko TRA kwa sababu itaonekana kwenye systems za TRA imefikia position gani. Na kwa ushauri tu huwa inatokea kuwa meli imefika lakini haijashusha mzigo iko bado kwenye kusubiri nafasi. Huwa kuna ucheleweshaji kidogo. Huo muda wa tangu umelipa hadi sasa si muda wa kutosha kuamini kuwa amekurusha. Nadhani utakuA na mkataba wa mauziano, au risit ya malipo n.k. Hivyo ikitokea ni rahisi kuchukua hatua stahiki. Kwa sasa hebu muamini kama ulivyoamini mwanzo kuwa atakuletea gari na ukampatia mapesa yote hayo.
 
sorry kabla sijatoa ushauri,kuna document inaitwa BILL OF LADING,alikupa hiyo?
 
Jamani mimi nataka kuagiza gari uk,na jamaa wamenitumia proforma invoice, niwalipe,sasa nakwazika na usalama wa hela yangu isije ikawa kilio cha mwaka,
wanavyoeleza benki za ulaya kwa hela zote zinzoingia lazima udhibitishe unatumia kwa shughuli gani, kwa maana ya kuwapelekea document.
 
Niliagiza gari kupitia agent wa hapa Dar es Salaam tangu mwezi wa tatu, ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto TRA ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake?
Ananiweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa, km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono

ndugu kama agent amekuahakikishia gari iko kenye meli uwe na amani...kaa pata maji ya bariiidiii usubirie kitu yako. Unanikumbusha mwaka 2007 nimeagiza gari yangu ya kwanza, nimeenda kwa agent samora akaniambia imefika mombasa, nkarudi siKu mbili Badae akaniambia meli imefika ila haijaanza kupakua mizigo, dah nkajua nimeliwa ,sana sana niliona nabaki na makaratasi mkononi ila gari ndo ishakwenda, nlipanda ghorofa la ppf towers japo niione meli uku roho inauma , siku ya tatu, ya nne , ya saba , ya nane, aaah nkajisemea hapana, naenda kufa na agent, nlipofika akaniambia imeshushwa ila bado iko yard mpaka ikagul;iwe tena ndo ipate gate pass, dah nkaoona sasa uyu jamaa sijui nimfanyeje...ikabidi nimtafte mshikaji wa bandari aniingize nicomfirm kama kweli gari ipo...nkaigia kijanja mpaka kwenye yard, dah nkakuta machine iko na makaratasi, kuifungua inanukiiiiiiiiiiaaaaaaa, dah yani nkaenda kulala kwa amani.
....furaha yangu ilipunguzwa na ushuru kuwa uplifted. Ila nlifurahi sana,by the way, meli zamani zilikuwa zinatumia muda mrefu iko apo bandari salama hata siku 20 bila kushusha mzigo, ila juzi bungeni mh mwakyembe amesema meli sasa zinasubiri hardly siku 9 mpaka 10 ndo zinashusha mizigo. So mwanaJf mwenzangu uwe na amani, agent ambaye yuko registerd hawezi kukuingiza mkenge kiivo,be patient iyo kitu unapata. ALL THE BEST.
 
lazima itakua (do)in any case inaweza kuwa kweli.

Agent hawezi kuiba gari

halafu mtu unaagiza gari kupitia ku clearing agent? Au huyo ni agent wa kuagiza magari na clearing at the same time?
mkuu, hata ukiagiza mwenyewe lazima at end point umpe registered clearing and forwarding agent amalizie.
 
Niliagiza gari kupitia agent wa hapa Dar es Salaam tangu mwezi wa tatu, ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto TRA ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake?
Ananiweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa, km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono

Mkuu pole na jakamoyo,
Ila kutoka tarehe 21 mpaka leo kwa pale bandarini sio siku nyingi,,
kama walivokushauri wadau hapo juu,kuwa mtulivu,..
isitoshe akiiba unaweza ukafuatilia gari inavyohamishwa umiliki TRA...

Unanikumbusha agent mmoja aliniagizia gari 2012 mwanzoni..
ilikuwa nusu nimlaze polisi..baada ya kunicheleweshea na hatimaye kunifojia risiti za storage charges za ziada...
siku hizi nimepata agent anayeeleweka asiye na makuu kwa hivyo huwa nalala usingizi...
ni vizuri walau ukafahamu ofisi ya agent ilipo kabla hujamtumia..na pia hakikisha kodi unalipa mwenyewe..
 
Subira huvuta heri.
Chako ni Chako.
Haraka Haraka haina baraka.
Kuwahi sio kufika.
Mwenda tezi na omo huishia ......
Hii ni misemo tu ya kiswahili ila ina maana.
 
Back
Top Bottom