Nahitaji kuwa Mjasiriamali, msaada wenu tafadhali

Yaani nimesoma hizi post, matatizo matupu; watu hawajui hata unataka kufanya nini.. wameshaanza kuongelea 3 Cs? motivations? outlets? storage? WTF?

Mrimi,

kitu cha KWANZA kabisa inatakiwa UJUE nini unataka kufanya; haya mambo ya 3 Cs, sijui website, sijui ofisi rent, sijui simu za biashara, sijui leadership na book keeping YATAFUATA! wewe tueleze kwanza unataka kufanya nini?

hawa watu wanaokupa ushauri hapa, wamesoma articles tu na sidhani kuna mtu hata mmoja hapa amefanya biashara; sasa kama ukiona hakuna tatizo (i am aware of patent issues and copyrights), tueleze ni biashara gani unataka kufanya alafu ndio tutaanzia hapo kukushauri!? you dont need to read any article at this very moment;

Wewe ndo mptoshajia namba moja na wewe ndo huju unacho sema, tuambie wewe unafanya biashara gani basi, Basi wewe mwambie afanye nini au ungekuja na maelezo yako hapa kinacho takiwa ni michango na si kupondea michango ya watu.

Na hapa jukwaani watu wanajitahidi kumweleza mtu jinsi ya kufanya biashara kitalaamu ili akafanikiwe, hata kama atakuja na aidea ya kufa mtu je kama hayuko Commited atafanya nini? niambie kama huko commited utafanya kitu gani. Je kama huna uwezo wa pesa/mtaji wa kufanya hiyo baish ara utafanya nini? si ndo kuishia kusema nini aidea nzuri lakini sina mtaji? Je kama ana uoga wa kufanya biashara atafanya vipi? atafanikiwa vipi akiwa ni muoga? hiyo aidea yake ataisimamia vipi?

Basi kama wewe umeshamfanyia hadi enveronmental analysis mwambie afanye biashara gani na si kuleta siasa hapa.

Na jambo jingine wakati wa sasa hivi sio wa miaka ya 90 wala 2000 mwanzoni, huu ni wakati wa ushindani wa hali ya juu na lazima unavyo ingia kwenye baishara uwe umejipanga, tunaishia kuwalalamikia wakenya kumbe sisi ndo tufanya mambo ya ajabu sana,

Wafanya biashara wengi waliofanikiwa ukiwachunguza wana hizo three Cs ingawahata wao wenyewe wanaweza wasizijue ni nini, na kuwa na three Cs si lazima uzifahamu ila kimatendo tu ndo unaweza fahamika kwamba wewe uko hivyo

Na mtoa maada amesema anahitaji aidea sasa watu si wanampa Aidia wewe unataka wampe nini?

Mkuu mimi nahitaji kufanya mradi wa kuniongezea kipato badala ya kutegemea monthly salary. Kiukweli sina idea yoyote ya maana juu ya mradi/biashara gani nifanye. Kusema ninataka nifanye nini ni ngumu kwa kuwa, kwa muda mrefu nimekuwa nikitegemea wengine(masomoni). Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba ndiyo sasa nataka kuanza. Nahitaji kusaidiwa nianze vipi na nini? Sijui kama nimeeleweka?

Mkuu siamini kwamba huko unako ishi huoni biashara yoyote ya kufanya, hao wengine wano ishi huko wanafanyaje? ushamambiwa ufanyeje sasa sijajua unataka nini zaidi,

Ila kuhusu kwamba huoni cha kufanya siamini ni kwamba hutaki kuangaisha kichwa chako ndo maana, hutaki kuumiza ubongo wako kufikilia mambo,

Na utasmaje unataka kuanza wakati hata aidea huna, eneway wewe hangaisha kichwa na aidea unazo nyingi tu na umetembea nchi hii, unaagalia TV, unasoma magazeti, unasoma vitabu
 
idea ya biashara inakuja kama vile mtu anavyompata mchumba mara nyingi mtu humpata ampendae sehem za ofisin mtaan hata shulen so na idea za biashara nazo ziko hvyo hvyo namna unavyojichanganya na watu ndo urahisi wa kupata ideas.halaf pia pendelea kusafiri sehem mbali mbali hii itasaidia sana
 
mkuu uko sahihi kabisa, na siku zote aidea nzuri ni ile uliyo ihangaikia mwenyewe hizi zingine ni just kukusapoti tu
 
Nimesahau kingine unatakiwa uanze kupenda kujisomea magazet na vitab vinavyohusiana na mambo ya biashara maana karibia siri zote za maisha ziko kwenye maandishi.si dhan kama ukiwa mvivu wa kujisomea utafanikiwa
 
Naweza kuonekana ni mvivu kutafuta elimu au kufikiria, ni sawa ila, ndio maana nimeweka wazi hapa hitaji langu ili wazoefu wa mambo haya wasaidie. Lakini pia sina hakika kama hili ni tatizo langu tu, naamini kuna watu wengi wenye shida kama yangu, so michango ya mawazo mnayotoa hapa ina manufaa kwa jamii nzima. Hii ni issue ya kuvumiliana tu mkuu.
 
Mwisho kama mwanzo. jamaa hajapata hata msaada alioomba. heri tukiri kwamba hatuwezi kumsaidia.
 
Ni wazo jema sana, cha muhimu ni kuamua tu. Funga macho, kazo roho, anza. Chochote utakachofanya utafanikiwa, Tanzania bado "virgin" kibiashara na ujasiriamali kaza buti, hakuna kisichowezekana.
 
Dr. Mrimi,

sasa nimekuelewa vizuri kabisa, baada ya hiyo post yako ya jana;

sifahamu vizuri unaishi wapi, lakini kama ni kijijini, unaweza kuuliza wanakijiji ni vitu gani wanavyohitaji; kwahiyo tuseme, kuna tatizo la maji kijijini, basi kwasababu una mtaji, unaweza either ukanunua lori au ukakodi lori la maji, alafu unauza maji;

note: always find the need to serve, usipeleke suti kuuza kijiji na watu hawavai suti, that wont work!

that is just an example, but i want you to understand how you can get an idea OR how a business idea can come about and what circumstances/environment can be used to form a business idea;
 
i like this post
 
Mrimi karibu kwenye ufugaji wa kisasa na kilimo cha kisasa kama utapenda. Siyafahamu vizuri mazingira ya tabora na mbeya kibiashara lakni najua tabora kuna ukame na hivyo kama utapenda kilimo cha kisasa ni bora uwe na irrigation plan pembeni in case of drought, vegetables huwenda zikalipa coz wandugu ni wavivu sana na pia sifahamu mahitaji ya maziwa, nyama (kuku, kiti) kwa maeneo hayo (peleleza).
nafahamu mbeya watu wengi wanalima na bei za vyakula huwa ni chee..
 
Haya ndo matatizo ya kuwa msomi. There is too much information and too many doubts.

The most important thing is commitment. Ndo maana hata mtu aliyemaliza darasa la saba anaanza kuuza karanga then ana move up kidogo kidogo.

By the fact that umekuja kuomba idea hapa, that shows u have not thought abt it clearly and therefore u are not commited. With commitment u will have passion (mapenzi makubwa) na biashara yako which will make u start the business ASAP.

Ukianza usimsahau kumwomba Mwenyezi Mungu akupe baraka na utuombee sisi wateja wako tupate hela ili tukuletee.
 
..tuambie wewe unafanya biashara gani basi, ...

Mimi natoa huduma za mikopo (Financial Services) kwa SMEs (Small and Medium Enterprises;) wewe mwenzangu unafanya biashara na ni biashara ipi unayofanya?

Nimeona, watu wengi wanatengeneza website, sijui hivi, sijui vile i always tell them GO AND DO SOME WORK first; haya mambo ya sijui nini, hayatakufikisha mahali popote; we anza kutoa huduma, ukishachanganya na biashara inakuwa then ndio utaweka mambo mengine; haya mambo ya sijui principle za business hizi ndio zinafanya watu wawe wazito sana;
 
Vizuri sana mkuu nitakutafuta unipe mkopo,

Mkuu sikiliza kwa sasa dunia imabadilika sana na tuko katika wakati wa ushindani, wewe unazan bila kufanya biashara kisasa tutaweza shindana na wachina wa kariakaoo? tutaweza shindana na wakenya?

Naamini hata wewe lazima uweke malengo ili hata siku mojo utoe mikopo East and Central Africa, tuko katika kipindi kibaya sana na lazima tujipange kisasa kuweza kushindana,

Hatuwezi fanya biashara kama tuko miaka ya 90 mkuu, kuna ushindani mkubwa sana, Mimi niko huku Arusha nawaona wakenya wanavyo kuja kwa wingi na kuanzisha kampuni zao huku, mimi kwa kweli siwalaumu na nawapenda sana, na wanafanya biashara kisasa zaidi tofauti na sisi watanzania
,
 
Dr.
Kama ungekua na mtaji ulioshiba ningekushari biashara ambayo mie naifanya sasa hivi na nakula kilaini sana bila hata buguza,lakini kwa mtaji huo haitawezekana.
 
Mrimi karibu kwenye ufugaji wa kisasa na kilimo cha kisasa kama utapenda. Siyafahamu vizuri mazingira ya tabora na mbeya kibiashara lakni najua tabora kuna ukame na hivyo kama utapenda kilimo cha kisasa ni bora uwe na irrigation plan pembeni in case of drought, vegetables huwenda zikalipa coz wandugu ni wavivu sana na pia sifahamu mahitaji ya maziwa, nyama (kuku, kiti) kwa maeneo hayo (peleleza).
nafahamu mbeya watu wengi wanalima na bei za vyakula huwa ni chee..

Yaah, ni kweli mkuu hapo kwenye red. Ila hapo kwenye blue, nahisi watakutaka uwaombe radhi! OK, ngoja nijaribu kufanya utafiti juu ya hili.
 
Dr.
Kama ungekua na mtaji ulioshiba ningekushari biashara ambayo mie naifanya sasa hivi na nakula kilaini sana bila hata buguza,lakini kwa mtaji huo haitawezekana.

Inaonekana hupendi kutoa maelezo hapa, ila sio mbaya, nakufuata mwenyewe huko uwani.

Thanks.
 
Dr. Mrimi,

sasa nimekuelewa vizuri kabisa, baada ya hiyo post yako ya jana;

sifahamu vizuri unaishi wapi, lakini kama ni kijijini, unaweza kuuliza wanakijiji ni vitu gani wanavyohitaji; kwahiyo tuseme, kuna tatizo la maji kijijini, basi kwasababu una mtaji, unaweza either ukanunua lori au ukakodi lori la maji, alafu unauza maji;

note: always find the need to serve, usipeleke suti kuuza kijiji na watu hawavai suti, that wont work!

that is just an example, but i want you to understand how you can get an idea OR how a business idea can come about and what circumstances/environment can be used to form a business idea;

Asante mkuu sana nimeanza kufunguka, ngoja nijaribu kutafakari, ntakuja hapa na optins nitakazokuwa nimezipata.

Tupo pamoja boss.
 
Vizuri sana mkuu nitakutafuta unipe mkopo,

Mkuu sikiliza kwa sasa dunia imabadilika sana na tuko katika wakati wa ushindani, wewe unazan bila kufanya biashara kisasa tutaweza shindana na wachina wa kariakaoo? tutaweza shindana na wakenya?

Naamini hata wewe lazima uweke malengo ili hata siku mojo utoe mikopo East and Central Africa, tuko katika kipindi kibaya sana na lazima tujipange kisasa kuweza kushindana,

Hatuwezi fanya biashara kama tuko miaka ya 90 mkuu, kuna ushindani mkubwa sana, Mimi niko huku Arusha nawaona wakenya wanavyo kuja kwa wingi na kuanzisha kampuni zao huku, mimi kwa kweli siwalaumu na nawapenda sana, na wanafanya biashara kisasa zaidi tofauti na sisi watanzania
,

Nimeongea na baadhi ya Watu Dar, tunaangalia jinsi ya ku expand, ila kuna matatizo machache ambayo ina bidi tuyatatue kabla hatujafungua ofisi zetu hapa; nitakufahamisha kisha tuonane tuangalie tukusaidiaje; kwanini wewe unamiliki biashara na unafanya biashara gani?

Ubarikiwe;
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom