Nafasi za ajira utumishi wa Umma 38432,

Mtumsafi

Member
Jun 1, 2012
90
64
May 28 Serikali kupitia sekretariet ya utumishi wa umma imetoa nafasi za kazi kwa watu.ni jambo jema na la kupongeza,lakini kinachonishangaza ni suala la kutaka vyeti.kwanini nashangaa?serikali hiyo hiyo hivi karibuni ilisema imefuta kigezo za kutaka "experience"kwani kigezo hicho kimetumika mara nyingi kuwanyima kazi wahitimu wengi wa vyuo vikuu,na hivo kimefutwa ili kutoa fursa sawa kwa wote..kwanini nahusisha hiyo na vyeti?

kwa waliomaliza vyuo vikuu mwaka jana,mpaka muda huu cheti hakijatoka ila transcript tayari,sasa serikali kwanini itoe tangazo halafu idai ni lazima uambatishe vyeti ilhali inajua mfumo wa nchini kuwa baada ya mwaka ndio vyeti hutoka?je wanataka kuwapa kazi kweli wahitimu hawa ama kuna watu wanawafikiria?mnisaidie,maana watu wanaona nafasi lakini wanashindwa ku aply kutokana na icho kisehemu CHETI.
 
First Graduate First Employed (FGFE). Wewe unataka kuajiriwa kabla ya waliokuwa mbele yako? Subiri upate cheti ndio na wewe uanze kuomba kazi huko tume ya ajra
 
Ndachuwa hujajibu hoja. Hili swali nami najiuliza sana sipati jibu.Wenye vyeti ni wangapi kwa muda huu? Hivi m2 aliyesoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu haaminiki? Ni ajabu
 
kwakweli hili ni tatizo,na cha ajabu,kwenye application,m2 anakuwa ameambatanisha copy ya transcript,na kwenye usaili anaitwa!hapa ngoma ndipo inapoanzia,wanaanza kudai cheti original,kama huna huingii kwenye chumba cha usaili!bora wawe wanakuondoa mapema,kuliko kuharibu nauli then wanakuondoa!!na wanajua kabisa kuwa sio tatizo la muhitimu ni mfumo,mf.chuo cha uhasibu(tia)cheti ni baada ya miaka 2!!
 
nimeudhunika sana nilipokutana na neno transcript not accepted yani post zipo nyingi ninazoweza kuomba tatizo kutaka cheti sasa kazi ya transcript ni nini? Zisiwe basi zinatolewa tusubiri hiyo miaka 2 cheti kitoke natamani niombe hivyo hivyo kiubishi labda watanifikiria home nimekaa sana toka mwaka jana daaaa! Mkiruhusu tu transcript mtanikuta mlangoni asubuhi nimemaliza diploma ya ICT
 
hellow.
jamani mimi ni mwanachama mpya wa JamiiForum mpya naomba kupokelewa ili nami niwe mwanafamilia na kutoa mawazo kama mnavyochangia katika mada zetu za maendeleo. asante.
 
kuhusu suala la ajira ni kama tunaonewa kwa sababu wanaohitimu vyuo hawapewi vyeti hapohapo kama zilivyo baadhi ya shule ila kuna utaratibu wa kusubria ndiyo maana watoa transcript ili wale watarajiwa katika ajira waweze kupata. sasa wanaposema hakuna kuja na transcript bali vyeti original hapa wanabagua umati unaokuwa umetoka vyuoni. bora tuvumiliane kwani transcipt na cheti havina tofauti ila huzidiana ubora tu.
 
May 28 Serikali kupitia sekretariet ya utumishi wa umma imetoa nafasi za kazi kwa watu.ni jambo jema na la kupongeza,lakini kinachonishangaza ni suala la kutaka vyeti.kwanini nashangaa?serikali hiyo hiyo hivi karibuni ilisema imefuta kigezo za kutaka "experience"kwani kigezo hicho kimetumika mara nyingi kuwanyima kazi wahitimu wengi wa vyuo vikuu,na hivo kimefutwa ili kutoa fursa sawa kwa wote..kwanini nahusisha hiyo na vyeti?

kwa waliomaliza vyuo vikuu mwaka jana,mpaka muda huu cheti hakijatoka ila transcript tayari,sasa serikali kwanini itoe tangazo halafu idai ni lazima uambatishe vyeti ilhali inajua mfumo wa nchini kuwa baada ya mwaka ndio vyeti hutoka?je wanataka kuwapa kazi kweli wahitimu hawa ama kuna watu wanawafikiria?mnisaidie,maana watu wanaona nafasi lakini wanashindwa ku aply kutokana na icho kisehemu CHETI.

Jifunzeni ujasiliamali,wahitimu wa vyuo wako lundo mtaani. Ajira za serikali hazitoshi kwa kila mtu.
 
hellow.
jamani mimi ni mwanachama mpya wa JamiiForum mpya naomba kupokelewa ili nami niwe mwanafamilia na kutoa mawazo kama mnavyochangia katika mada zetu za maendeleo. asante.

mkuuu karibu sema kuwa makini na maada zako, hii sio fb wala twitter
 
Back
Top Bottom