mi_mdau
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,111
- 1,498
Eti linaitwa shirika la nyumba la taifa lililoboreshwa na lenye nguvu kazi mpya. Sioni kama linaendeshwa kwa manufaa ya watanzania wengi, kama nakosea mtanisaidia.
Walivyoanza kutangaza kuuza nyumba za ubungo nikawa na shauku ya kujua ntazipataje na pengine nikichukua mkopo wa miaka mingi ntajikomboa. Bei ikanikata maini kabisa. Leo naona tena wanaanza mchakato wa kuuza nyumba za mchikichini ilala. Ila nyumba 1 ya vyumba vitatu naambiwa itauzwa kwa shilingi milioni 168 na ushehe bila VAT.
Watazania wangapi wataweza bei hii?? Hapo hujakopa, ukikopa utaongeza na riba kwenye hiyo bei. Zipo nyingine kadhaa wameuza ikiwemo za dodoma. Wanamlenga nani?? Je NHC sasa ni shirika la biashara??
Kwa mawazo yangu, NHC si kwa manufaa ya watazania wengi ambao wana kipato cha kawaida sana. Nyumba hizo watanunua matajiri halafu nao watulangue kwenye kodi.
Hili nalo limeniskitisha