Nabii wa Wasabato Mama White adai aliambiwa na malaika sabato ni amri ya kipekee kuliko zote ni muhuri wa Mungu na haikupigiliwa misumari msalabani

Wadau hamjamboni nyote na Sabato njema

Siyo maneno yangu bali ya Nabii Hellen G White kupitia ziara yake ya kinjozi aliyoifanya mbinguni

Nimeweka nukuu zake:

(1.) ”Naliziona zile mbao za mawe zilizoandikwa juu yake zile Amri Kumi. Nilistaajabu nilipoona amri ya nne katikati kabisa ya zile amri kumi ikiwa na nuru laini ya nuru ikiizunguka(halo light). Malaika akasema, 'Ndiyo amri pekee kati ya zile kumi inayomfafanua Mungu aliye hai aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo."' (Life Sketches of Ellen G. White, Page 95-96, chapisho rasmi la Waadventista)

(2). "Yesu akavifungua, nikaona zile amri kumi zimeandikwa kwa kidole cha Mungu. Katika ubao mmoja kulikuwa na Nne, na ubao mwingine sita. Na zile nne katika ubao wa kwanza ziling'aa kuliko zile sita. Lakini ya nne, amri ya Sabato, iling'aa zaidi ya zote, kwa maana Sabato ilitengwa ili itunzwe kwa heshima ya jina takatifu la Mungu.Sabato takatifu ilionekana kwa utukufu wa mg’aro ulioizunguka pande zote(halo light).Niliona ya kwamba amri ya Sabato haikupigiliwa misumari msalabani." (Maandishi ya awali ya Ellen G. White, ukurasa wa 33, chapisho rasmi la Waadventista)

(3) .Amri ya Sabato kwa hiyo inaweza kuchukuliwa kuwa muhuri kwa sababu "ndiyo pekee kati ya hizo kumi ambazo zinapatikana jina na cheo cha Mtoa Sheria. Ndiyo pekee inayoonyesha sheria imetolewa kwa mamlaka ya nani. ina muhuri wa Mungu, uliobandikwa kwenye sheria yake kama ushahidi wa uhalisi wake na nguvu inayofungamana nayo” (Patriarchs and Prophets, p. 307).

Wadau je kuna ushahidi wowote wa kimaandiko kuthibitisha madai hayo?

Je ni amri zipi za Mungu kati ya zile kumi zilizopigiliwa misumari pale Golgotha?

Karibuni tujadili
Mkuu Uzalendo
Nakupa kudo sana. Endelea kutuletea mafundisho na tafakari juu ya hii dini ya uongo ya Ellen G. White.


Naona na wewe inakuudhi kama inavyoniudhi hasa kutokana na kuonekana kwa nje kama dini ya kweli huku ikiwa imebeba upinga Kristo wa kina cha juu kabisa.

Niweke wazi nawapenda wasabato nawaombea sana wamjue Kristo lakini nachukukia sana dini wakuu wa dini yao wanaowapumbaza pasipo kujua lolote.
 
Mungu analikusanya Kanisa lake pamoja Ili linyakuliwe.

Wote tutarudi kuabudu na kuitunza sabato ya BWANA,

Wanaojiita wasabato, watafundishwa na Roho kunena Kwa lugha mpya, pia watatabiri.

Tupo katika msimu na majira mapya.

IBADA kuu ya Wana wa Mungu itafanyika siku ya SABA.

Amen
Hii mada sijui ilinipitaje! Kama kuna siku wanafunzi walinena kwa roho kweli kweli hakuna inayoizidi siku ile kuu ya PENTEKOSTE siku ile Roho Mtakatifu alipowashukia wakamwona waziwazi!

PENTEKOSTE ni siku ya 50 baada ya ufufuo wa BWANA na zote zilikuwa JUMAPILI.

Siku ile ya PENTEKOSTE, Jumapili ile ya ajabu KANISA la kwanza likazaliwa na kuanzia siku ile INJILI ikahubiriwa kwa nguvu zote kwa kila kiumbe sawa na agizo la BWANA.

In short kuabudu katika ROHO na KWELI kulianza siku ya Jumapili kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Uzalendo wa Kitanzania, Saint Anno II
 
Back
Top Bottom