Wayahudi na wasabato wanaendelea kuabudu sabato ya Jumamosi ambayo hata Yesu aliiabudu, ni nani aliibadili iwe Jumapili

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
AMRI YA NNE: Ikumbuke siku ya Sabato uitakase, Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako

Tusiingie sana kwenye hizi dini na sheria zao bali tuzungumzie siku ya kuabudu.

Siku ya Jumamosi ndio iliyotengwa kuwa ya kisabato tangu zamani kwa wayahudi, nikimaanisha ya kwamba kina Musa hadi Yesu ndio waliiabudu hio siku na kuitakasa kuwa siku takatifu, Ni mpaka leo ukienda Israel siku ya Jumamosi maduka mengi na ofisi nyingi hufungwa kuruhusu watu waiabudu siku ya sabato.

Na hata kwa wasabato hata wa hapa kwetu, wengi wenye biashara huwa hawafungui jumamosi

Ilikuwaje ikabadilishwa kuwa jumapili ?
 
Hakuna sehemu yoyote ktk biblia iliposema sabato ni jumamosi ambayo mnaitumia leo hii kusema ni siku ya sabato.

Biblia ilisema siku ya 7, ikimaanisha siku yoyote unaweza kuifanya ya 7 tangu kuanza kwa majukumu yako ndani ya siku 6 na inayofuata uifanye sabato,na siku hiyo inaweza kuwa juma lolote lile iwe jumapili,juma3, j4 whatever.

Nyie wasabato na hao nduguzenu wayahudi wa uongo hapo palestina mnawezaje kuyakataa mafundisho ya mroma ilihali baada ya yeye mrumi kubadiri kalenda iliyotumiwa zaman akaleta mpya bado mnaifuata?.

Mujue kuwa kabla ya kubadiri kalenda, siku ya 7 haikuwa jumamosi wala jumapili, sasa nyie vilaza mnafuata mafundisho ya nani?.

Tumieni akili basi dini mmeletewa zikiwa na ukakasi badala mzichunguze nyie mnaziamini bila kuhoji, mtazidi kufarakana mpaka mwisho, maana mnaamini nje ya ukweli.
 
Sabath ni siku ya jumamosi
 
Sabato inayofuata matendo ya mwilini ilipitwa na wakati wake ikaja sabato ya rohoni. Agano la kale na agano jipya pambanua hapo. Ukisema ni warumi ndio walioanzisha sabato jumapili na ikapokelewa hivyo mpaka leo itakuwa haina maana kwani sabato ya sasa haiangalii siku
 
Hizi story huwa zinasikikq sana kwenye vikanisa vya mitume na manabii laghai.
 
vikanisa vya mitume gani? Kanisa ni la Yesu. Kanisa ni moja tu lenye watenda kazi wengi, hao wote ni wafuasi wa Yesu wanaihubiri injili, ila ole wake atakayeihubiri injili feki
 
Injili ni habari njema. Mapokeo haya ya kupindua maandiko ni habari feki. Paulo mwenyewe akiwa ulaya na waongofu wapya wasio wayahudi aliwapeleka kando ya mto suku ya Sabato wasali.
 
Hakuna sehemu yoyote ktk biblia iliposema sabato ni jumamosi ambayo mnaitumia leo hii kusema ni siku ya sabato.

Biblia ilisema siku ya 7, ikimaanisha siku yoyote unaweza kuifanya ya 7 tangu kuanza kwa majukumu yako ndani ya siku 6 na inayofuata uifanye sabato,na siku hiyo inaweza kuwa juma lolote lile iwe jumapili,juma3, j4 whatever.

Nyie wasabato na hao nduguzenu wayahudi wa uongo hapo palestina mnawezaje kuyakataa mafundisho ya mroma ilihali baada ya yeye mrumi kubadiri kalenda iliyotumiwa zaman akaleta mpya bado mnaifuata?.

Mujue kuwa kabla ya kubadiri kalenda, siku ya 7 haikuwa jumamosi wala jumapili, sasa nyie vilaza mnafuata mafundisho ya nani?.

Tumieni akili basi dini mmeletewa zikiwa na ukakasi badala mzichunguze nyie mnaziamini bila kuhoji, mtazidi kufarakana mpaka mwisho, maana mnaamini nje ya ukweli.

Mtoa mada una logic. Ni sahihi kabisa kuhoji je, ni wapi kwenye vitabu vya dini pameandikwa siku ya sabato ni Jumamosi? Majira na miaka hiyo hakukuwa na majina ya siku, hakukuwa Jumatatu, Jumanne,......Jumapili. Majina ya siku na mambo ya kalenda tunazotumia siku hizi yaliletwa na Roma miaka ya baadaye kabisa! Na zuri au baya zaidi wasabato wanasema kuwa wanafuata kila lililoandikwa kwenye biblia, kakini kwenye biblia hakuna siku imeandikwa sabato ni Jumamosi, bali siku ya saba! Siku ya saba inaitwaje maana kila siku ni siku ya saba kulingana na mtu alianzia siku gani kuhesabu!
 
Upo sahihi kabisa mkuu.
 
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako

Tusiingie sana kwenye hizi dini na sheria zao bali tuzungumzie siku ya kuabudu.

Fanya kazi siku sita, ya saba kipaumbele kiwe kuabudu na kupumzika.

Kwa wasabato hata wa hapa kwetu ni wengi wenye biashara huwa hawagungui jumamosi, lakini pia hata ukienda Israel huwezi kukuta maduka yamefunguliwa siku ya jumamosi wanayoiita shabaat

Ilikuwaje ikabadilishwa kuwa jumapili ?

Tafuteni muda wa kufanya kazi mjenge maisha yenu na familia zenu acheni mambo ya kusadikika haya, hayakusaidii lolote wala kubadilisha maisha yako na ukoo wako, walioanzisha na kuwabrainwash walishaacha kitambo wanakula tu maisha baada ya kuwachangia sadaka zenu (unaweza kugoogle their networth na familia zao) wakati we mjuaji unatafuta kujustify akili yako ilivooshwa kuprove wapuuzi wengine wrong na sijui ili upate nini? Ukifa ndo mwisho wa safari yako hata ukionyesha wengine hawajui J2 vs J1, that's nonsense! Ndo maana CCM imewashika ishajua akili zenu ni kusubiri miujiza tu
 
Sabato inayofuata matendo ya mwilini ilipitwa na wakati wake ikaja sabato ya rohoni. Agano la kale na agano jipya pambanua hapo. Ukisema ni warumi ndio walioanzisha sabato jumapili na ikapokelewa hivyo mpaka leo itakuwa haina maana kwani sabato ya sasa haiangalii siku
Ikumbuke SIKU ya sabato na uitakase, how comes unasema sabato Haina siku?
 
Ni sahihi kabsa kila mtu ahabudu siku yake kwa sababu mambo yote yametengenezwa na binadamu tu .

Hata wewe unauwezo wakubuni siku yako na Mungu wako kulingana na wazo lako tu.
 
Yes kabla ya hao wazungu hawajasema haya, babu zake walikuwa wanaabudu siku gani? Huyu mpare sijui mjita au mtanzania mwingine leo anajua sabato kuliko mzungu aliyemletea na kumpora utajiri wa babu zake na kumwambia ni upumbavu tu, anajuaje km babu zake waliabudu zaidi ya siku moja? Au kwa kuwa babu zake weusi anaona akili zao pia nyeusi yeye kaoshwa akili akajua weupe ndio wanaojua sabato zaidi na Mungu wao ana akili zaidi? Upuuzi tu na brain kuoshwa ikawa empty!
 
Back
Top Bottom