Nabii na Mtume Joseph Kibwetere, Aliyewachoma moto waumini wake nchini Uganda

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,064
13,732
Nimetumia muda ku-google ili nipate ‘maana ya neno imani’ bila kugusa vitabu vitakatifu. Kila maana ninayosoma kwenye mtandao naona ni nyepesi kuliko nachokifikiria, kinachosimuliwa na kinachotokea. Kabla sijaamua kuachana na Google, nikakumbuka, Mwalimu wangu Denis Mpagaze aliwahi kutuambia kwa lugha ya kigeni tukiwa darasani Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino, “google will make you stupid”! Hapo ni kama alitupiga kofi la uso, tukaona ‘maluelue’. Yeye alikuwa anasoma sana vitabu kwa nakala ngumu (hard copies).

Nikagoogle tena kujua kwanini alisema Google inaweza kutupumbaza!? Google nayo ikaleta nukuu ya mchekeshaji maarufu wa Uingereza John Marwood Cleese akisema, “kama wewe ni mpumbavu kweli, huwezi kujua kuwa wewe ni mpumbavu. Unapaswa kuwa mwelevu na mwenye akili za kutosha kugundua kuwa wewe ni mpumbavu.” Ebana eeh!

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule aka Profesa Jay kupitia wimbo wake wa Bongo Dar es Salaam, yeye anaamini wenye imani potofu ni wale wanaoamini msemo wa Wahenga ‘aliyeko juu mgojee chini’, anasema, “mtangoja milele na mtakufa bila kelele, kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetere.” Sasa huyu Kibwetere ni nani?

Joseph Kibweteere au ‘Kibwetere’ wa Uganda, alikuwa Mwalimu wa shule ya msingi. Lakini aliyejaribu siasa akashindwa kuwashawishi wananchi, akahamia kwenye dini akawapumbaza watu kwa kujiita ‘Nabii na Mtume’. Huko akateka mioyo ya wengi wenye shida akiwaahidi kuwapeleka peponi, lakini mwisho akawaua kwa kuwachoma moto akiwaaminisha kuwa mwisho wa dunia umefika. Aliwateketeza mamia kwa moto wa mafuta ya petrol, wakaonja adhabu ya jehanam waliyosimuliwa wakati wanaahidiwa kuingia ahera. Tukio hili baya kuwahi kutokea Afrika kwa imani iliyojaa udanganyifu, limeacha majonzi makubwa na kupewa jina la Mauaji ya Halaiki ya Kanungu (Kanungu Massacre).

Kibwetere yeye aliitumia Biblia hiyohiyo kupotosha, alisoma vifungu akavipindisha na vikawa kama vimenyooka. Unajua hata Shetani alitumia ‘Maandiko ya Mungu’ kumshawishi Yesu ajitupe kutoka mlimani. Lakini kwakuwa Yesu alikuwa na maarifa alipinga kwa maandiko hayohayo na akamshinda.

Biblia kupitia Methali 31 inasema, ‘mpe kileo aliye karibu na kupotea’ na divai aliye na uchungu nafsini mwake, anywe asahau umasikini wake. Kibweteere yeye akawapa masikini ujinga akijua wazi kuwa masikini na mwenye shida akilewa ujinga na kupumbazika lazima tu ataangamia. Alijua Maandiko ya Mwenyezi Mungu yanasema, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.” Akawanywesha maji ya mchele akiwadanganya kuwa ni maziwa, wakavutiwa na rangi, wakayabugia kisha akawaangamiza.

jina la ‘imani’.

Serikali ya Uganda haikulifumbia macho hili, ilichukua hatua haraka. Ikizingatiwa kuwa Kanisa la Kibwetere na wenzake lilikuwa limesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi zisizo za Kiserikali Mwaka 1997. Desemba 2000, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda, Moses Ali alimteua Jaji Augustus Kania kuongeza Kamati ya kuchunguza tukio hilo la mauaji, lakini ripoti hiyo haikuwekwa hadharani, na Serikali ilitangaza kuwa inaendelea na uchunguzi zaidi.

Kibwetere alipotea kusikojulikana. Alipotea kimiujiza? Je, alikuwa miongoni mwa majivu yaliyokusanywa kutoka kanisani, au alikuwa miongoni mwa waliofunga mlango na kumwaga mafuta ya petrol kwenye jengo la kanisa na kuwasha kiberiti? Ni Mungu pekee ajuaye.

Lakini kumbe hata Shetani hutuzwa! Utashangaa. Septemba 2011, Bi. Mwerinde alitunukiwa tuzo iitwayo Ig Nobel Prize eti kwa jinsi alivyopanga na kushawishi kuhusu siku ya mwisho wa dunia; eti alitoa funzo kwa dunia kuwa makini wakati wa kufanya mahesabu ya nyakati. Lakini tuzo hii iliyoanzishwa mwaka 1991 ililenga katika kufanya kinyume cha ile tuzo ya heshima ya Nobel. Ig Nobel hii huwatuza watu ambao wamefanya mambo yasiyo ya kawaida, na mara nyingi hutolewa kama kejeli/ucheshi.

Ndugu yangu katika imani, tuamini na tutafute maarifa sahihi tusije kuangamia. Tusiishi kwa kusubiri kupewa kila kitokacho kwa mtu yeyote kwa jina la ‘mtumishi wa Mungu’. Tuwapandiye juu ili tusome na kuelewa.

Nakuacha na kauli fupi ya Mchungaji Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, anasema, “wewe unaamini nini? Baki na imani yako, lakini usivunje sheria za nchi.”

 
Kama Una nia kumjuwa Kibwetele, basi Kibwetele halisi ni Museven

Kibwetele aliuwawa yeye pamoja na wafuasi wake hapo kanisani.

Tafuta Lord resistant Army ya Joseph Kony linatokea wapi na Tafuta uhusiano wa Joseph Kony na Kibwetele ukiweza kupata details ndio utaujuwa ukweli.

Hiyo report ya tume Kwa nini haikuwekwa wazi?

Kibwetele pia alikuwa anataka Uganda itawaliwe Kwa 10 commandments.

Ukiacha Kibwetele kuchomwa Moto yeye pamoja na wafuasi wake lakini kwenye uwanja wa kanisa liligundulika kaburi la kimbali waliuwawa watu wengi na Museven wakafukiwa humo.
 
Kama Una nia kumjuwa Kibwetele, basi Kibwetele halisi ni Museven

Kibwetele aliuwawa yeye pamoja na wafuasi wake hapo kanisani.

Tafuta Lord resistant Army ya Joseph Kony linatokea wapi na Tafuta uhusiano wa Joseph Kony na Kibwetele ukiweza kupata details ndio utaujuwa ukweli.

Hiyo report ya tume Kwa nini haikuwekwa wazi?

Kibwetele pia alikuwa anataka Uganda itawaliwe Kwa 10 commandments.

Ukiacha Kibwetele kuchomwa Moto yeye pamoja na wafuasi wake lakini kwenye uwanja wa kanisa liligundulika kaburi la kimbali waliuwawa watu wengi na Museven wakafukiwa humo.
Maelezo zaidi mkuu, hivyo vitabu vinapatikana wapi?
 
Ukishaona mtu mweusi anajipa mavyeo hayo.

1. Nabii na Mtume
2. Mtume na Askofu
3. Nabii na Askofu

Hapo kuna utapeli.
 
Back
Top Bottom