Naachwa kisa ni Dini

Fazul

Member
Apr 2, 2012
82
9
Nimekuwa na mpenzi wangu wa mwaka mmoja,siku za hivi karibuni alianza kupuuza simu zangu na nilipochimbua zaidi na kuweza kumuhoji aliniambia ananipenda ila Dini ndio tatizo.mimi ni muislamu naye ni mkristo.na mimi siwezi kubadili dini,na kumuacha ni vigumu sana kwani nampenda zaidi ya sana.wakubwa nisaidieni maana sijui la kufanya.
 
Kwani hio dini yako imebadilika ghafla katikati ya mwaka ?

Akufukuzae hakwambii toka
 
Hapo inabidi uchague moja.
mhh napenda kufikiri kwamba kuna uwezekano wa kupata vyote na sio kuchagua moja (kwenye mapenzi kuna sacrifices, kuvumiliana na compromise) ukiona inashindikana jua kwamba mapenzi yenu are not strong enough.., after all we are all humans
 
usipobadili wewe, abadili yeye. Kama mna mipango ya kuoana na yote yameshindikana mtafunga ndoa ya kiserikali.
 
dah...kumbe wahanga wa haya mambo ni wengi eeh.....
jombaa.....we chagua kuchapa lapa......vinginevyo....oaneni ndoa ya bomani....
 
usipobadili wewe, abadili yeye. Kama mna mipango ya kuoana na yote yameshindikana mtafunga ndoa ya kiserikali.
naam hilo ndio jibu la wapenda nao, na kama unapenda mwenza wako hautapenda abadili imani yake kwa ajili yako (unless anataka mwenyewe) cha maana ikiwezekana ni kufunga ndoa ya kiserikali na kila mtu kuendelea na imani yake (am sure God will forgive kumpenda mtu wa imani tofauti) so long as mengine unatenda mema kwa imani yako.

Ni mengi yanaweza kutenganisha watu lakini hili sidhani kama ni kikwazo kivile kama watu mmeshibana
 
mhh napenda kufikiri kwamba kuna uwezekano wa kupata vyote na sio kuchagua moja (kwenye mapenzi kuna sacrifices, kuvumiliana na compromise) ukiona inashindikana jua kwamba mapenzi yenu are not strong enough.., after all we are all humans

Badili, ukishamuoa rudi kwenye imani yako!
I know a couple ambao wao walipendana ila wazazi ikawa issue, so mume alimfuata mke, wakafunga ndoa; then mke akamfuta mume na kufunga tena ndoa, baadaye kila mtu alibaki na imani yake!
 
usipobadili wewe, abadili yeye. Kama mna mipango ya kuoana na yote yameshindikana mtafunga ndoa ya kiserikali.
katika dini ya kiislam hakuna ndoa ya kiserikali, ya kimila wala ya mkeka. Pia msichana muislam hairuhusiwi kuolewa na asiekua muislam. So mwanaume ndie wa kubadilisha dini otherwise hapo hakuna sacrifise or compromise.
 
Badili, ukishamuoa rudi kwenye imani yako!
I know a couple ambao wao walipendana ila wazazi ikawa issue, so mume alimfuata mke, wakafunga ndoa; then mke akamfuta mume na kufunga tena ndoa, baadaye kila mtu alibaki na imani yake!
Yeah kinacho-matter ni mapenzi yenu wawili na mlivyoshibana hizi pressure za ndugu na jamaa sometimes kama kuna uwezekano wa kufanya mambo na kutowakwaza au kufanya wawatenge basi ni bora kufanya hivyo, ila sio kuridhisha watu wakati wewe mwenyewe unajinyima furaha.
 
Nimekuwa na mpenzi wangu wa mwaka mmoja,siku za hivi karibuni alianza kupuuza simu zangu na nilipochimbua zaidi na kuweza kumuhoji aliniambia ananipenda ila Dini ndio tatizo.mimi ni muislamu naye ni mkristo.na mimi siwezi kubadili dini,na kumuacha ni vigumu sana kwani nampenda zaidi ya sana.wakubwa nisaidieni maana sijui la kufanya.
mkristo wa dhehebu gani?
 
katika dini ya kiislam hakuna ndoa ya kiserikali, ya kimila wala ya mkeka. Pia msichana muislam hairuhusiwi kuolewa na asiekua muislam. So mwanaume ndie wa kubadilisha dini otherwise hapo hakuna sacrifise or compromise.

Thats why it comes kwa mtu mwenyewe au watu wenyewe walivyoshibana, na imani zao (I hate to believe kwamba mtu utakuwa umeishi maisha yako vema na kutenda mema yote.., ila mwisho wa siku unaambiwa unakwenda jehanam, kisa ulioa / uliolewa na mtu asiye dini yako).

Vile vile kum-force mtu abadilishe imani yake tangia utoto ili tu awe na wewe sio kumtendea haki na ni kama kumyima haki yako ambao yeye ndio anaamini ndio njia bora.
 
mwanamke siku zote hana dini, km unampenda mwenzio hacha kushikilia dini, unajua mkiwa na nia1 lengo1 njia1 inapendeza sana.
 
Lakini mnaependana akikuonyesha kua hakupendi tena kwa sababu moja au nyingine wewe kama unajiamini why should you force!
 
wewe usiwe mgumu wa kusoma alama za nyakati....
hapo hupendwi tena,keshapata mwingine....
dini asiione wkt anakutokea aje aione baada ya mwaka mmoja...mnh i doubt it....
ni kwamba kaona hamna chemistry,hayuko na furaha akiwa na wewe,kaamua kuchapa lapa...dini imekuwa kisingizio....hata ukibadili dini mwenzio huyo hakupendi tena,jua hilo!
 
katika dini ya kiislam hakuna ndoa ya kiserikali, ya kimila wala ya mkeka. Pia msichana muislam hairuhusiwi kuolewa na asiekua muislam. So mwanaume ndie wa kubadilisha dini otherwise hapo hakuna sacrifise or compromise.

hizi imani katika mapenzi ni mtihani mkubwa kwa kweli.
 
Nimekuwa na mpenzi wangu wa mwaka mmoja,siku za hivi karibuni alianza kupuuza simu zangu na nilipochimbua zaidi na kuweza kumuhoji aliniambia ananipenda ila Dini ndio tatizo.mimi ni muislamu naye ni mkristo.na mimi siwezi kubadili dini,na kumuacha ni vigumu sana kwani nampenda zaidi ya sana.wakubwa nisaidieni maana sijui la kufanya.

Achana nae tu kama huwezi kubadili dini.
Naimani kila mtu ana msimamo wake kiimani,
usitake kumpeleka kwingine kiimani kama usivyo
taka kwenda kwingine pia.

Jitahidi kumsahau,utapata mwingine.
 
Back
Top Bottom