Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
sasa mama............
is it PRACTICAL?
Mkuu ukiwaza kama JK hiyo si practical hata kidogo ila ukitafuta walau data kidogo na kukuna kichwa unaweza kugundua kuwa inawezekana. Kwanza hiyo figure ilianza kutajwa karibia miaka 10 iliyopita, ambapo sasa hivi ingekuwa ni karibia asilimia 500 (kwani KCC ilikuwa chini ya 50000). Kama viongozi wetu wangekuwa na akili basi wangechukua uamuzi wa kufikia kiwango hicho kwa miaka walau 10 kama Kenya. Si ajabu sasa hivi tungekuwa tunaongelea KCC ya laki 5. Hebu tujiulize kidogo; Kwani mishahara ya vigogo na wabunge kwa kipindi hicho imepanda kwa asilimia ngapi?
Kuna jamaa alikuwa anapata 156000 mwaka 2003, na sasa anapata karibia 1.5m. Hizo ni asilimia ngapi? (mimi napata karibia 800%). Wakati huo KCC ilikuwa nadhani kama 35000, kwa sasa nadhani ni 104,000 (202%). Hebu basi angalia na kada nyingine ndo utagundua kuwa kweli watu wa KCC wanonewa na JK haweza kukwepa lawama.