Na hii sio siasa na dini??????????

kyemo

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
570
718
Mzee wa upako aibuka akimfagilia JK



Na Edmund Mihale

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kuwa wanaompinga, Rais Jakaya Kikwete katika utawala
wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.

Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha.

Kauli za Mchungaji Lusekelo zimekuja kukiwa na malalamiko ndani ya jamii, kuhusiana na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne, hasa kushindwa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kupunguza umaskini.

Lakini yeye alisema, "Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura. Hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.

"Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Jakaya Kikwete anavyotaka. Hapana. Hili jambo halipendezi mbele ya Mungu," alisema Mchungaji Lusekelo.

Alisema imejengeka tabia kuwa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, utamaduni ambao ni mbaya.

"Hatupo tayari kumpongeza kiongozi akiwa hai, watu wanasifu maiti kuliko mtu akiwa hai hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa.

"Mfano Mwalimu alipokuwa hai hakuwa na sifa hizi tunazoziona sasa, walisema wazi wamechoka na 'unyerere' leo hii tunamasifu kwa kila nderemo. Watu wamebadilika wanasifu viongozi wanapotoka ndani ya madaraka.

"Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza. Hili linatokana na wachache wanaomsaidia rais kukiacha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa na nguvu na kikaacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa dhaifu. Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa rais," alisema

Alisema kuwa ana imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete hivyo aachwe atekeleleze mchakato wa katiba kupunguza mfumko wa bei na kujenga barabara za hewani.

Source:majira newspaper,30th march,2011


Jamani na hii sio siasa katika dini au kwa kuwa kafagiliwa mkuu wa kaya,Ingekuwa imefagiliwa CDM ungesikia,"hooo! siasa na dini" mara "si mnaona hichi chama cha wakristo"
Haya na huyo mkemeeni basi asiingize dini katika siasa tuone hiyo fair ground!
 
Back
Top Bottom