N. B. C LIMITED kuendelea kuibiwa mamilioni.

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Benki ya Taifa ya Biashara zinasema wizi mkubwa wa mamilioni ya shilingi ulioanza mwaka juzi hautokoma kwa kuwa benki hiyo imekuwa ikiwalipa watumishi wa ngazi za chini mshahara kidogo sana wakati wao ndio wana dhamana ya kutunza mabilioni hayo huku wale wafanyakazi wa ngazi za juu wanalipwa mamilioni ya pesa wakati wao sio wahenyaji.

Vijana wanaojulikana kwa jina la Vodafasta ambao ndio wanaongoza wimbi hilo la wizi na hujuma mbalimbali wanasema nia na dhamira yao kufanya uhalifu huo ni kujiongezea kipato na kujiandalia maisha mazuri, kwani wao vijana ndio wasomi, na wazee hawana elimu yoyote zaidi ya uzoefu walioupata kuanzia benki ikiwa chini ya utawala wa serikali ya Mwalimu Nyerere.
 
Uwizi ni uwizi tu!..hakuna mtu atakayewaunga mkono kwa vitendo hivyo, regardless ya mishahara wanayolipwa!...kama ikithibitika hivyo wafungwe waozee gerezani!...huh!
 
Back
Top Bottom