ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,060
- 49,748
Kukua kwa teknolojia kumeyavuta makampuni ya Simu kuanza kufanya biashara ya huduma za kifedha ambazo hapo awami zilikuwa zinafanya na taasisi za fedha tuu kama benki.
Katika kufanya biashara hiyo makampuni ya simu yameanzisha huduma mbalimbali ya muda mfupi za kifedha ikiwemo kuwezesha miamala, kutunza fedha na kutoa huduma za mikopo.
Sina shida na wao kufanya Huduma hizo ila tatizo linakuja pale ambapo huduma hii hasa za mikopo kugeuka kuwa mnyonyaji na mkamuaji kwa wananchi Kwa kutoa mikopo yenye tiba kubwa ambazo zinajukioana kama mikopo ya Kausha Damu.
Miaka ya hivi karibuni kulitokea malalamiko ya kuibuka kwa utitiri wa taasisi za kifedha za binafsi ambazo zilikuwa zinatoa mikopo kwa riba za kijambazi na kupelekea malalamiko kwenye jamii na Serikali kuingiliwa kati. Kwenye kilele cha malalamiko walikuwepo walimu na wakinamama wa vikoba nk.
Serikali iliingia na kuja na kanuni ambazo zimepunguzwa kwa sehemu kubwa mikopo ya Kausha Damu ambayo ilipelekea watu kujinhonga na Ndoa kuvurugika au watu kufilisika Kwa Mali zao kupigwa mnada.
Sasa limejitokeza Wimbi jipya la mikopo ya kausha Damu Kupitia makampuni ya Simu mfano Vodacom wao Wana Huduma za mikopo kedekede na zote hizo ni kausha Mathalani;
Huduma zote hizo ni za kijambazi na kausha Damu kiasi kwamba imegeuka kuwa unyonyaji mpya kwa wananchi huku wao wakipatwa faida kubwa ambazo ndio hutoa sehemu yake kama gawio kwa Serikali na kuifumbia macho huu wizi.
Wanakuambia kiasi cha kukopa ukikopa wanakata pesa yao kabisa kabla ya matumizi, na ukienda kutoa wanakata tena kwenye salio na mbaya zaidi riba inaendelea kuongezeka kadiri mda wa kulipa ambao ni ndani ya mwezi mmja tuu. Huu ni wizi na haikubaliki.
Ukiacha wizi huu wa Kausha Damu, haya makampuni yamekuwa na wizi mwingine kwa wananchi kwa kutumia bando na dakika ambapo husisha mapema zaidi kabla ya mada ukiuliza unaambiwa ni matumizi yako.
Swali la kuniuliza, ni kwanini Serikali iko kimya kwa wizi huu wa wazi licha ya malalamiko ya mara kwa mara? Je, Serikali Imebariki wizi na kufukarisha Wananchi wake kwa maslahi ya Kikodi?
Tuwaombe Wabunge na baadhi ya watu ambao huwa wanasimama kutetea maslahi ya wananchi ili wakawakalie kooni Mawaziri Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba kwa kuifumbia macho ambapo kwa sehemu kubwa huenda wanapata 10%.
Shime Wabunge wafuatao chukueni hii hoja mkawapiganie wananchi Bungeni;
Piga kelele komesha wizi naamini Mh. Rais akisikia atawa summon wahusika na hatua zitachukuliwa kuliko kukaa kimya.
Pia soma 👇

- Songesha
- Nipige tafu
- Mgodi
- M Pawa
- M Koba
- Chomoka nk

- Mwita Waitara
- Getere
- Musukuma
- Festo Sanga
- Jumanne Kishimba
- Luhaga Mpina
- Hamis Tabasamu
- Civid 19
Piga kelele komesha wizi naamini Mh. Rais akisikia atawa summon wahusika na hatua zitachukuliwa kuliko kukaa kimya.
Pia soma 👇
DOKEZO - BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo Kisheria na zinalipa kodi?
YAH: MALALAMIKO JUU YA TAASISI ZA MIKOPO MTANDAONI Kama mnavyojua changamoto zipo kwa Kila mtu hasa upatikanaji wa fedha pale unapokuwa umepata shida ya ghafla yenye uhitaji wa pesa au changamoto kwenye Biashara, mara nyingi unatafuta sehemu kama kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ya kifedha ili...
www.jamiiforums.com